Jaribio la kwanza nimekosa visa ya Marekani, Waafrika tunabaguliwa

Mh..hiyo labda upitie bahamas au uingie mexico alafu uiflash passport then utoboe kwa boat uitafute miami florida. Sema yote ya nini hayo utatumia gharama nyingi sana kuwalipa human traffickers kuliko kupata visa. Bora upate visa tu uingie ukishaingia ndio bas tena michongo ya papers ni mwelele
 
Kwanza ACC yako inasoma sh ngapi?

Kamwe huwezi pata viza ya marekani kama ACC yako bank inasoma sh 3500/
 
Kweli kabisa mkuu hata hiyo ukiiipata ni bora zaidi
Unajilipua huko huko ila watu waoga tu
Hakuna kinachoshindikana chini ya jua
 
Nakusifa kwa kuweza ku attempt. Kama signals zako hazikamati bongo usiweke usiku, ondoka.
Kuhusu kukataliwa Visa acha malalamiko ya kwamba mnabaguliwa, just review documents zako na jinsi ulivyoijaza DS-160 form, pia jinsi ulivyojibu maswali yao wakati wa Interview.
Wakati unaendelea kujaribu, hakikisha maisha yako ndani ya bongo hayasimami kisa unapambania Visa uondoke.
 
Mie niliomba wakaniuliza first question what is your name . Nikasema age please nikasema , wakaniuliza unandugu huko nikasema ndio nikamtaja . What is your purpose to go there , ?? Nikasema kusalimia na kubadili mazingira ,unaka miaka mingapi?? 3 montsh , there utakuwa unajihusisha nanini kusaidia jamii , how kuwaelekeza wadogo kuhusu usafi wa mazingira , kusoma na kufanya vizuri katika masomo yao, kingine najua kuimba nakudance nitaperfom nakuwa fundisha kudance nakucheza kimasai . Na tamaduni zetu akaniambia sing for me one song nikaanza oh laleyo ha mmh ! Nilimwimbia akapenda akanipanvisa ya miezi minne maana kweli nitakuwa assets kwao sasa wewe uliulizwa nini
 
Ilikuwa Visa ya Congo hiyo eti
 
Mbona watu hamuendaga Urusi? Wakati viza ya kwa Putin ni simple tu tena ukizingatia wajukuu wa Nyerere...
Urusi watu wanaipenda sana mdomoni lakini kwenda kutafuta maisha mnakwepa,twendeni na urusi jamani ukienda ubalozini visa nje nje unarudi nayo.
 
Ungepata iyo VISA mgekua ambaguliwi?
 
Haha pale huwa ni bahati yako tu ..nilishanyimwa twice 2017 nikapotezea nikaja kurudi mwaka jana VO hata hakuomba documents ni maswali mawili tu nikaambiwa karibu USA. Jaza ds160 kwa umakini utatoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…