Jaribu kujiweka katika nafasi ya Samuya, ungefanyaje kutuliza upepo?

Ila mkuu, kujaa barabarani gen Z, sidhani sababu si watatumia vitisho kama vya 7/7 na wote tutaishia kukaa ndani tuu.

Lissu atatumia njia gani labda, sabbu watu gen Z si ni walewale tuu wa 7/7 na lisu ndio haohao
Lissu aliyekuwa kabla ya kuingia Ukongo sio atakayetoka
Lissu ashajijengea fame najua akitoba hotuba yake 1 itatoa watu machozi.
Itakuwa rahisi kushawishi Gen Z
 
Yupo kwenye a point of no return na ni mtu kipofu ambaye hawezi kuona, toka uteuzi wake kwenye chama hadi reactions zake baada ya oct 29, kuna watu nyuma ya uwepo wake kwenye kiti na sidhani kama watamruhusu aache.

Sadly wengi ni watanganyika ambao wapo radhi nchi iangamie kuliko kuwazuia wao kutengeneza dynasties and generational wealth.

Wasichokijua, umaskini unavyoongezeka na vijana wanakuwa more frustrated. Mbaya zaidi kuna social media ambayo imetengeneza alternative bunge na mikutano ya wananchi.

Kwa hiyo hasira ambayo ipo sustained and ignored muda mrefu lazma ipo siku itaripuka. Na mbaya zaidi ni ngumu kuliona hili kwa sababu layer ya uongozi inamea machawa ambao hawawezi kuwaambia viongozi ukweli kwa sababu hawashiki vyeo vyao kwa merit ila kumfurahisha boss kwa kumpa sifa na matumaini hewa.

This isn't even about Samia ila system nzima
 
CCM haina tena watu weledi. Mkapa angekuwa hai haya yote yasingetokea. Kimama kinaweza kutumia njia hii: ajiuzu na kumwachia Nchimbi. Pia atow gerezani watu wote aliowabambikia kesi. Yanayobaki amwachia Nchimbi i.e katiba mpya, watuhumiwa wa mauaji ya 29/10 na hatua za kuchukuwa.
 
1. Kuwatoa watu wazito kafara kuwawajibisha kwa watu waliopotezwa, kutekwa na mauaji
Hisia zangu akifanya hivyo naona hatamaliza masaa 240 anaweza akaondolewa kwenye kiti chake na wasaliti.
Unajua amezungukwa na wahalifu waliyo mtengenezea mtego ili abaki ajikinge kushitakiwa na awalinde na wao.
Wanajua akitoka watashitakiwa.
Kuna uwezekano 2030 wakamshawishi au kumtishia asiondoke madarakani.

Nahisi hii kitu ndiyo ilimuweka Mugabe madarakani muda mrefu na ndiyo iliyo muondoa. Waliomshinikiza kuachia madaraka haikuwa lengo la demokrasia au maendeleo. Si unamuona Mnangagwa anachofanya sasa?
 
Je, Bunge la haki litamlinda? Au limuondoa baada ya wiki 1 Kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais?
Bora hata Sasa ana bunge ambalo analiendesha kama dondocha
Hata katika bunge la haki theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar hawawezi kupiga kura ya kumuondoa madarakani Mzanzibar mwenzao.
 
Hapa anajinasua vipi?
 
Hata katika bunge la haki theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar hawawezi kupiga kura ya kumuondoa madarakani Mzanzibar mwenzao.
Bunge lina wabunge 400 sijui ni idadi Gani inatoka Zanzibar
Na kura ya kutokuwa na Imani na Rais inatakiwa idadi gani
 
Dawa atundike daluga kwa hiari yake mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…