Jarida la Inside the Nation lamtaja Rais Samia kama Rais aliyefanikiwa kuifungua nchi zaidi Kidiplomasia na Kiuchumi

Jarida la Inside the Nation lamtaja Rais Samia kama Rais aliyefanikiwa kuifungua nchi zaidi Kidiplomasia na Kiuchumi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku M Bwanku.

Jana Jumatano Februari 23, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua hatua ya Jarida kubwa la Marekani la Inside the Nation kumtaja Rais Samia kama Rais aliyefanikiwa kuifungua nchi zaidi Kidiplomasia na Kiuchumi na kufanikiwa kuokoa fedha nyingi sana ambazo Tanzania ingekosa kwa sababu ya hali yake ya kisiasa huko nyuma.

Baada ya mwishoni mwa mwaka Jana, Majarida makubwa ya Afrika na Dunia kuanzia Avance Media la Ghana kumtaja Rais Samia kama moja ya Wanawake 10 wenye nguvu na ushawishi mkubwa Barani Afrika na baadae Jarida linalosomwa zaidi Duniani la Forbes nalo kumtaja Rais Samia kama moja ya Wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi mkubwa Duniani aliyefanya mabadiliko makubwa.

Sasa Jarida lingine la Inside the Nation la Marekani limemtaja Rais Samia kama shujaa kwenye eneo la Diplomasia na Rais aliyefanikiwa kuifungua nchi zaidi Kidiplomasia, kiuchumi na uwekezaji. Pata NAKALA sasa ya Gazeti hili la TANZANIA LEO usome mwenyewe Makala hii iliyosheheni hatua mbalimbali anazoendelea kuchukua Rais Samia mpaka kufanya Majarida makubwa kama haya ya Duniani kukunwa na kazi yake.

IMG-20220223-WA0028.jpg
 
Mama ana meremeta na kuimeremetisha Tanzania, Jarida la The Economist ndio wa kwanza kulianzisha

P
 
Tumshauri yule M'beleji mweusi ajiandae tu kuja kugombea ubunge mwaka 2025, kuhusu ndoto za uraisi asahau au aendelee kuota mpaka atapoamshwa na wenzake.
 
Na ukiona hakusifii ujue ana mpango wa 'kukuua'. Sasa hapo utaamua mwenyewe kipi bora kwako. Usifiwe uishi au Upondwe ufe?

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
Kwa akili zako sifiwa tuu uishi, ila kwa binadamu anaejitambua huo ni utumwa kushindwa kusimamia unachokiamini kisa kuogopa kifo.
Kwahiyo Samia ataishi milele maana mabeberu yanamsifia!
 
Kwa akili zako sifiwa tuu uishi, ila kwa binadamu anaejitambua huo ni utumwa kushindwa kusimamia unachokiamini kisa kuogopa kifo.
Kwahiyo Samia ataishi milele maana mabeberu yanamsifia.!
Shida sio kufa. Shida kufa huku hujatimiza maono yako. Halafu anayefuata anavuruga ya kwako anaanza yake. Hapo ni kutwanga maji kwenye kinu. Hatua 5 mbele kisha 5 nyuma.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Better attend to a wise man’s reprimand than listen to a song sung by a fool.
 
Ni kawaida beberu kusifia likisha fanikisha linachokitaka.

Hata kwenye zizi la mbuzi beberu humramba ramba mbuzi jike likisha timiza haja zake.
 
Ulikuwa ni uamuzi sahihi kumuweka Mama Mulamula kama waziri wa mambo ya nje. Anaongea kingereza kama vile anaongea kiziba.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Huko kwenu munauona huo uchumi?

Mi huk hari ni balaa. Kila kitu bei juu
 
Mama ana meremeta na kuimeremetisha Tanzania, Jarida la The Economist ndio wa kwanza kulianzisha

P
Nani aliifunga nchi?
 
Back
Top Bottom