Jasmine Razack: Feitoto amekwisha fungua kesi CAS dhidi ya TFF na sio Yanga!

Wanawazuga tu hapo kesi feisali dhidi ya yanga na sio tff subiri mje muone
 
Hapa ndo kuna mtego. Ni kweli Fei hakwenda Yanga baada ya kuambiwa na TFF?

Au walizungumza masaa 6 akapewa sharti la kurudi amalizie mkataba, kurudi aboreshewe maslahi, timu inayomtaka ije?
Hilo la kuzungumza masaa 6 nani ana ushahidi nalo?
 
Mara nyingine usikurupuke tuu kuanza kuropoka, mchezaji akivunja mkataba bila kufuata taratibu Tff walipaswa wamuadhibu mchezaji kwa kosa alilo fanya, na hapo ndipo palipo na msingi wa kesi
Mashabiki wa yanga mna matatizo gani [emoji848][emoji848]
Hii loophole ikitumiwa na kila mchezaji kutakua na ligi?
 
Mchezaji anataka kuvunja mkataba na timu.

Chama kinachosimamia mpira kinahusikaje?

Arsenal kavunja mkataba na Willian, Guendouz

United kavunja mkataba na Ronaldo

Na sikuona wakiwa wamekimbilia kwenye chama


Walikaa wakakimbilia wapi?
 
Hayo unayosema ni sawa na umbea hayana ushahidi
 
Anaruhusiwa, ila kwa makubaliano/mazungumzo
Hiyo unayoisema wewe kwenye sheria za FIFA "ni mutual agreement" ambayo ipo kwenye "termination of contract with just cause"

Kuna kipengele hapo kingine kinafuatia kipo article ya 17 ya sheria za FIFA kinasema " unilateral termination of contract without just cause"

Ambacho hakihitaji kuwe na hayo mazungumzo/makubaliano ya pande zote mbili.

Ila consequences zake ndio zinazofanya watu wengi waogope kutumia kipengele hicho kwasababu ya ukali wa adhabu.

Adhabu ni faini kulingana na mkataba unavyosema, lakini pia kufungiwa na shirikisho lako la soka kwa kipindi cha muda wa miezi minne. Baada ya hapo upo huru kucheza popote.

Na rekodi za kesi kama hizi zipo mfano kuna mchezaji ambaye alifanya kama alivyofanya Feisali anaitwa Hakan Çalhanoğlu unaweza ukasoma kesi yake CAS.

Sasa inavyosemekana kwenye mkataba wa Feisali kiasi cha faini kilichoandikwa endapo mkataba huo ukavunjwa kiholela, pesa yake ni ndogo ambayo haiendi kuinufufaisha Club.

Hivyo wanaona watampa urahisi sana na Club haitafaidika, ila ingekuwa kiwango cha pesa ya faini ni kikubwa basi kwa Club ingekuwa ni sherehe na hata yeye mwenyewe Feisali asingejaribu kuvunja mkataba.

Na kupitia sakata hili naskia wachezaji wanaosaini mikataba mipya wanawekewa faini za pesa nyingi ili kuwafanya washindwe kuondoka.
 
Mkuu wanaingilia kati kama kwenye mkataba kuna utata kama hio double signing sio kuvunja au kuandika
Double signing ni kosa unafungiwa. Ila kwakuwa kuna kuwa na maslahi ya simba au yanga basi sheria inapindishwa
 
Hapa ndo umemaliza kila kituuu.
 
Wewe jamaa ni mjuaji na haujui Hakan alifanya maridhiano na timu yake ila sababu umejaa ujuaji endelea kukaza shingo
 
Si kweli.
Mkataba wake unaruhusu mchezaji kuvunja mkataba.Kilichofanyika ni ubabe tu kukataa kutumika kifungu hicho.Yanga walichemka kuweka kipengele kinachomruhusu kuvunja mkataba kwa kulipa milioni 100 na mishahara mitatu.

Suala la makubaliano ni siasa za mpira tu kwani ukweli upo katika mkataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…