Jaydee anastahili heshima lakini asipewe sifa za uongo

Jaydee anastahili heshima lakini asipewe sifa za uongo

I am a music producer, sound engineer, and vocalist.

Waimbaji wa zamani watabaki kuwa bora wakati wote. Nasema hivo kwa sababu;
1. Waimbaji wa zamani hawakuwa wanategemea sana effects za studio kwa ajili ya ku-tune sauti zao. Sauti zao zilikiwa ni hivo hivo zilivyo.

2. Waimbaji wa sasa hivi ukiwavua "Autotune" sauti zao ni mbaya mbaya tukizitoa huko kwenye platforms mtawachukia. Hata baadhi yao huwa wanajistukia. Ukimaliza tu kumrecord anakuambia niwekee Autotune.

3. Waimbaji wa zamani walikuwa sio wavivu kiuandishi, na walikuwa wakiandika kwa kufuata sheria za uandishi wa nyimbo.

Of course wapo waimbaji wa kike wazuri ila ni wale waliopita THT au waliotokea makanisani au waliokuwa wanaimba Kaswida.

4. Wasanii wa hivi sasa hata ukimuuliza Bridge/daraja katika music ni nini? Hajui.

Mi ni hayo tu machache, sitaki nimfukuze Zuchu bado sijaruka naye duniani. 😂
Kumbe producer Studio unatusifu, ukifika JF unatuponda hivyo. Kwel ww n snitch
 
Wapo wasanii kwa uchache wa wanawake kwenye Sanaa walijitoa na kukubalika haraka na sasa tunawatazama kama "icons" kwenye Sanaa ya muziki, mmojawapo ni Lady Jaydee anastahili heshima Sana...

Lakini hata hivyo tusianze kabisa kuwapa wasanii wakongwe sifa za uongo kuwa ni wakali Sana kuzidi wasanii wa sasa. Wakati Sanaa imekuwa sana na sasa hakuna tena ubabaishaji kama wa zamani ...kama kipaji kipo kinaonekana na kama sauti ipo inaonekana.

Nampa Lady Jaydee heshima kuliko Zuchu au Maua Sama lakini kulazimisha kuwa lady Jaydee ni mkali kisanaa kuliko Zuchu na Maua Sama sio kweli.

Wasanii wakongwe wanastahili heshima lakini tusiwape sifa za Uongo.

Lady Jaydee hata Ray C kwenye ubora wake alikuwa hamfikii kabisa, tuwape heshima lakini sio sifa za Uongo..
Kabla sijakuhukumu nitajie huo ubabahishaji wa zamani ambao sasa haupo
 
Siku nyingine punguza kuropoka pumba mkuu
 
Kumbe producer Studio unatusifu, ukifika JF unatuponda hivyo. Kwel ww n snitch
😂😂 Na wewe huwa unaomba auto-tune? Ila naamini vocal yako ni iko good haihitaji hizo robots.

Njoo tu studio, wala sitakusnitch.
 
Binafsi nimefanya muziki wa Hip Hop. Nimerekodi kwa Amba AB Records na Lamar lakini ilikuwa nikiwasikiliza Wasanii wa zamani naona kabisa siwezi kupenya.
😂 Hip Hop inataka swagger, ukimiss tu hapo inakumwaga. Hapo ungechagua aina ya Hip hop maana ziko tofauti. Kuna ngumu, nyepesi, mnato, n.k.
 
Mtoe Zuchu wasafi and that girl will be done!
Autotunes, Ngoma aandikiwe, promo apigwe na Bado anapigwa viatu jukwaani..
Hebu Zuchu afanye kolabo na rappers wawili watatu kwanza afu afikie nusu ya Jide wa kwenye Nimeamini featuref by Prof. Jeezy au atoe Ngoma kama Understanding by Jide na TID ndipo tuanze kufikiria kumlinganisha na Commando Jay D.
Jay D ashindwe nini?
Utake hisia gani usiipate kwake?
Beat gani umpe aishindwe?
Lugha gani umpe aishindwe kuiimba kwa ufasaha na utamu?

Jide anaweza fanya Ngoma na KR Mulla Jibaba CD 700 na Ngoma ikawa hit.

Can Zuchu or Maua dare do any of that? Labda Maua kidogo.
Wakati wa Jaydee wengi walikuwa wanaRap, na ndio maana collabo na hao wanamuziki zilikuwa nyingi tofauti na sasa.
Kwahiyo hizo featuring sio kigezo cha ubora zaidi ya Zuchu, nadhani kama watu wangekuwa wanachana sana kama zamani sidhani kama wangekwepa kumweka Zuchu.

Pia zamani kushirikiana ilikuwa kwa upendo tu, sasa hivi ni biashara. Jaydee alikuwa bora wakati wake na amejenga legacy for years, ila kumlimganisha na Zuchu ambae anatawala era hii ni kumdanganya.
 
Tukubali Zuchu na Jaydee wamefanya mziki kwenye era tofauti, na kila mtu ana style yake yake ya kuandika na kuimba wako tofauti.

Sasa hivi ni ngumu kwa Jaydee kutengeneza shabiki mpya kutokana na aina ya muziki na uimbaji unaofanywa sasa.

Kama ilivyo kwa wacheza mpira Ronaldo si bora kama ilivyokuwa mwanzo, ila heshima yake aliyojenga ipo pale, kimlinganisha na Vinnie sasa hivi ni kumdanganya.

Jaydee hawezi shindana na kina Zuchu, Nandy wakati na akashinda.
 
Mtoe Zuchu wasafi and that girl will be done!
Autotunes, Ngoma aandikiwe, promo apigiwe
Ukali wa msanii unatokana na potential yake na si lebo, kama lebo ingekua na msaada zaidi wasafi kusingekua kuna failure lavalava, queen darlin.
 
Ukali wa msanii unatokana na potential yake na si lebo, kama lebo ingekua na msaada zaidi wasafi kusingekua kuna failure lavalava, queen darlin.

Hatuwezi kupuuzia mchango wa labels kwenye muziki.. labda kama si mtu wa muziki.

Huyo Lavalava anajulikana nchi nzima kwa sababu yupo wasafi.
Meanwhile, kuna wasanii ni wakali sana na hakuna anayewajua kwa kuwa wako label za kijinga.

Remember Rich Mavoko?
Bro, alikuwa relevant akiwa wasafi. Alipotoka tu na habari yake ikaishia hapo.

Sasa hebu imagine Tyga angekuwa wau bila Young Money!
Kendrick angekuwa wapi bila Aftermath au TDE?

So kipaji ni kitu kimoja, ila kufanikiwa na kuwa relevant as a musician ni suala la label au Juhudi nyingi sana za kibinafsi.
 
We jamaa unazeeka.
Tangu uanze kushabikia CCM akili ya afya yako imetwist...
😂😂😂

Embu tafuta albam ya Jide inaitwa Binti. Uisikilize yote. Kama utalinganisha na hao watoto hapo..
 
Kwenye wimbo wa Zuchu mwambieni mwabieni mali yake yaliwa kuna mstari unasema "wape salamu za Betty Mkwasa" ,nilivyosikia tu hapo nikasema 100% huyu Chuchu anaandikiwa nyimbo zake.
 
Back
Top Bottom