JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"


Kwa waliipitia chuo watakuwa wanaelewa kuhusu INTELLECTUAL PROPERTY RIGHTS ambapo uko utakuta mambo ya patents, copyrights na mambo ya trade mark. Ninaposema IPR namaanisha creations of minds kama music, literature and other artistic works, alichokifanya JB ni COPYRIGHT INFRINGEMENT, yaani ka produce kitu ambapo kimeshakuwa produced, sio haki kisheria, ndio maana kila siku wasanii mnapigiwa makerere mrudi shuleni ndo matokeo yake haya
 
Point hapa warumi ni kutoa ushauri kama ulioutoa hapo!!

Na siyo Kumkandia JB kwa maneno ya dharau as if ye ni wa kwanza kucopy!!!

Ushauri tu inatosha!!!

Ukitaka kumtetea mtu usitumie maneno hayo '"as if yeye ni wa kwanza kukopi"
Hivi unajua kwanini tumelivalia njuga hili tukio? Unafikiri hatujui wengine walio kopi?
JB tunamsema kwakuwa hatukutegemea vitendo kama hivi kufanywa na yeye!
 
Last edited by a moderator:

JB ameingia mkenge ni haki yake kusulubiwa maana ametia aibu..
 

Kumbe ukweli ni majungu?
Kumbe kukopi maudhui ya kazi ya mtu ni ubunifu?Hivi umesoma ulicho kiandika?
 
JB ameingia mkenge ni haki yake kusulubiwa maana ametia aibu..

Ni kosa kisheria kukopi mawazo ya mtu mwingine tena bila kumtaarifu muhusika. Na ndio maana kwenye movie nyingi uandika "ni marufuku kukopi movie hii na soundtrack iliyomo kwenye filamu hii bila idhini ya muhusika, hatua kali za kisheria zitachukuliwa"
 

Umeandika mambo mengi lakini umejikuta unashindwa kumtetea kwa hoja zenye nguvu bali hoja dhaifu sana!

Hivi kwakuwa wahindi walikopi Hollywood kwa hiyo inampa haki JB kukopi? Kwanini aliandika yeye ndio mtunzi wa story? Yani tusifie upuuzi wa JB kwa upuuzi wa wa hindi?

Kwa hiyo unajaribu kusema JB ni msanii asiye jiweza ndio maana ana kopi? Kwanini ana kopi wakati script writter ni wengi tuu nchini?

Utetezi huu ni dhaifu sana na unaendelea kumdhalilisha JB
 

Basi nilichokosea hapo ni kuweka suala la idea badala ya Maudhui!!!

Coz nilikuwa nikisema Idea, nilikuwa namaanisha kila kitu!!!

Coz kama umeangalia Movie ya partner ya Salman khan na ile ya "HITCH" utagundua kuwa CONTENTS (kile ambacho unazungumzia zaid) imechukuliwa yote!!!!

Critics waliiponda Ladies Vs Ricky Bahl, Coz ilikuwa imechukua kila kitu kutoka Kwenye John Tucker Must Die, na some Contents kutoka kwenye ile Chasing Papi...

Critics huwa hawapondi Uchukuaji wa ideas, huwa wanaponda uchukuaji wa Contects, ingekuwa hivyo basi Movie za kihindi kibao zingepondwa, kama HNY ya SK, BodyGuard ya Salman, Jaan Dushman ya kina Akshay, Etc hizi zote wamedevelop stories za Hollywood!!

kwenye suala la Sequel, nilikuwa namaanisha suala la ideas (MAUDHUI kama unavyomaanisha) limekuwa gumu sana sahiv, na ubaya watazamaj wamekuwa wakidemand zaid sequels kwenye upande wa Si-ci au comic movies kuliko new inventory, kwasababu mwisho wa siku maudhui yanakuwa yale yale tu, Mfano lastest movies za KisuperHeroes ni Captain America, Thor, Iron Man etc, ambapo ukiziangalia ni ideas zile zile tu za SpiderMan, Superman, batman na WonderWoman, hakuna kipya hapo, Thats why wakipresent idea mpya na ikibamba basi utakuwa ni mwendo wa Sequal tu, Thor ina sequal, Captain America, Iron Man etc!!!

Nilichokuwa namaanisha hapa ni kwamba, copying katika Viwanda tofauti vya movies duniani ipo, Bollywood wanacopy sana movies za Hollywood, SANA, najua ni ilegal lakin sijawah kusikia ikileta tatizo kabisa, NA critics wa Bollywood wasingekuwa wanalalamika sana kama Kweli crew za movie husika zingekuwa zinashirikishwa katika hili!!!!

Me ninachoshauri, ni kuwaambia Wasanii wakibongo wadeal na ideas na Siyo Contents kama unavyosema, na pia ningewaambia Bollywood the Same thing!!!
 
Last edited by a moderator:

sijaja kwa ajili ya kumtete JB hapa!!

Nilichotaka kukiweka, Copying katika Movies, ni tatizo la dunia nzima katika viwanda vya Movies duniani!!

So ulichotakiwa kukileta hapa, ni kwann suala la KuCopy maudhui ya Movies zilizochezwa awali limekuwa kubwa???? kiini chake ni nini???
 
Ukitaka kumtetea mtu usitumie maneno hayo '"as if yeye ni wa kwanza kukopi"
Hivi unajua kwanini tumelivalia njuga hili tukio? Unafikiri hatujui wengine walio kopi?
JB tunamsema kwakuwa hatukutegemea vitendo kama hivi kufanywa na yeye!

Typical Tanzanian!!

So kama ungeanza kupiga makelele kuhusu suala la kucopy movies za nje kwa hao wengine unaowajua, unafikiri huyo usiyemtegemea (JB) kufanya hicho kitu Angethubutu kufanya???

So Ray, Mtambalike and Co. wakicopy ni sawa tu?? but since JB ambaye ndo anatakiwa kuwa m-bunifu (Kuliko wote) akiCopy ni tatizo???

Hawa wengine wanaoperate kwenye mfumo gani wa Movies hapa bongo???

Wapo tofauti na huyo JB???
 

Tanzania tunayo hiyo Sheria, na USA kuna kipind ilikuwa signed na kupitishwa kama Criminal offense..

Kwa mtazamo huo, Tungekuwa tunafata Strictly law inavyosema, Tusingekuwa na hizi CD's za kina Albaba, AK-47 etc, na pia tusingekuwa na Kina LUFUFU au JUMA KHAN!!

So why Can't you just Blame the laws???

Kama ulikuwa unalijua hili suala la IP, kwann tangu awali usingetumia Influence yako KUBWA uliyonayo kwenye hili jukwaa kupinga hizi ishu??? coz am sure ungeanza tangu zaman kuziEnforce hizo sheria humu, akina JB wasingethubutu kucopy tangu hizo enzi za kina "regina"..
warumi, movie industry duniani kote itakosa msisimko kama Hiyo sheria ikiwa implemented strictly!!!

Kiwanda kingine kuAcknowledge movie ya kiwanda kingine after copying it ni NGUMU, thats why unaona hata Big heads wa kwenye movies industry kama Bollywood wanaCopy contents za Hollywood!!!
 
Last edited by a moderator:

Nilivyosoma hii comment ikabidi niangalie nani ka comment aseh, kuanzia Leo kaa ukijua warumi anakukubali sana yani, bonge la comment bro salute sana
 
Last edited by a moderator:

Well said mkuu, ila lengo la huu uzi ni kumkumbusha JB kutojibweteka , maana hii kashfa ya kukopi movie sio Mara ya kwanza na haipendezi kuendekeza kuiga movie mpaka watu wanagundua, inashusha sana hadhi ya msanii..

Nadhani hii scandal pia ilishawahi kumtafuna Eric shigongo kuwa uwa anatafsiri novel za nje na kuziweka kwenye magazeti yake , ila mpaka kesho hakuna aliyewahi kuthibitisha uvumi huo, hivyo kwake inabaki kuwa tetesi tu ila kwa JB big no asiendekezwe kiasi hiko bwana
 
Last edited by a moderator:

Sawa Mkuu umehitimisha vyema!!
Ila nguvu ya matusi iliyotumika awali ni wazi kuwa watu wengi tunaojibebesha mamlaka ya kukosoa haya mambo wengi wetu hatufuatilii kwa undani sana mambo haya.

Mos Def amejitahidi kusawazisha mjadala kwenye maeneo mengi. Hapo awali kwa watu tusioweza kupayuka na kutukana tulishindwa kuwasilisha zaidi.
Nadhani ni vyema tujenge utamaduni wa hii mijadala katika namna ya kujenga zaidi.
Hapo awali kwa kupitia jukwaa la burudani kule tulikuwa na Bishop Hiluka kama nomekosea jina anisamehe, Hiluka ni mwandishi sana wa masuala ya tasnia ya filamu na pia ameshiriki miradi kadhaa.
Kwa bahati mbaya wakati wa mijadala kule hakukuwa na hamasa sana kama inavyoonekana mda wa matusi na kejeli.

Itapendeza hili likitupa mwanzo mpya wa kuitumia JF kutengeneza fukuto la walaji wa kazi za sanaa ambalo tutakuwa na ufahamu mpana wa sanaa na hivyo kuyaelewa mazingira ya utendaji kazi wa wasanii wetu na kiwanda chetu kwa ujumla, hatimaye maoni tutakayokuwa tukitoa hata wadau watajua duh kweli JF ni soo.

Pamoja katika Tasnia!!
 

AGREED warumi
 
Last edited by a moderator:

Huna lolote wewe hata darasani unajulikana kwa kutoa photocopy maana umepitiliza kwenye copy and paste. Bongo kucopy na kupaste ni kitu cha kawaida so punguza kuhukumu mwemzako mfyuuuu.
 

Tena huyo warumi sijui ke au me apunguze lugha zake za kipuuzi mkosoe mtu kistaarabu atakuelewa mwanzo wa thread ameonge maneno machafu sana. Pamoja na yote aliyokosea jb lakini tukumbuke ni mwanadamu pia sasa mwanume unamwita litumbo sijui nini sio fresh. Warumi na hii sio mara moja kujifanya yeye ni Mungu wa jukwaa hili hizo tabia acha bwana umekaa kimajungu majungu tu kama muuza kahawa. UNABOA SANA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI YA JF.
 
Huna lolote wewe hata darasani unajulikana kwa kutoa photocopy maana umepitiliza kwenye copy and paste. Bongo kucopy na kupaste ni kitu cha kawaida so punguza kuhukumu mwemzako mfyuuuu.

Hapa umeandika nini? umemtetea?Kama ni kweli ni jambo la kawaida kwanini JB alindika yeye ndio mtunzi wa story?Kwanini hadi sasa ana kaza shingo pamoja na ukweli unajulikana?
 

Well said..hapa lengo ni kuhakikisha tunawambia ukweli ili wasirudie makosa.
 
Well said..hapa lengo ni kuhakikisha tunawambia ukweli ili wasirudie makosa.

Rutta na warumi nyie sio wakosoaji bali lengo ni kumdharirisha mtu lugha zenu sio nzuri kabisa. Nandomana naona kama kukopi na kupest jb sio wa kwanza labda mna mengine. Maana jouneGwalu alifafanua hii issue kwa kumqoute manege lakini mlikuja na abusive language kitu ambacho sio fresh.
 

Huu ni uwanja na mada inayo muhusu JB.. kama hao wengine wakikopi tukathibitisha nao tuta wasema lakini hatuwezi kumtetea JB kwa kigezo ana fanya kama wengine..unatakiwa kujua JB ni msanii mwenye nguvu katika soko la sanaa ndio maana mjadala wake umeteka sana hisia za wengi..kwakuwa ni mmoja ya wasanii wanao tazamwa sana..

Ningekuwa yeye ninge jivunia sana kwa kuthibitisha natazamwa sana maana si rahisi kutega mijadala kama huna ushawishi kwenye soko..kabisa..nani kuhakikishia Filamu hii kauza sana na inayo fata atauza sana maana kila mmoja atataka kujua kafanya nini

Mimi namfatilia sana JB sio kwamba nachangia tuu bali ni mmoja wa wateja wake na ni msanii wa kiume bongo ninaye amini ana uwezo mkubwa sana lakini kwenye hili siwezi kumfumbia macho kabisa..ameharibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…