JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

@MosDef,
Umeongea vitu vingi sana lakini inaonekana unachanganya mambo! Kwanza, unaposema cjui XYZ alikopi idea unapaswa kufahamu kwamba hakuna hatimiliki ya idea, yaani wazo... Kwa maana nyingine, haikatazwi kutumia idea ya movie nyingine! Ninachoona ni kwamba unachanganya kati ya Idea (Wazo) na Maudhui (Contents)... hivi ni vitu viwili tofauti! Mwandishi wa JB ameeleza vizuri... alichokopi yeye sio idea/wazo bali ni maudhui/content! Kwa bahati mbaya sijaziona filamu zote mbili lakini inavyoelekea ni kwamba hizo filamu zimefanana sana... kama hivyo ndivyo, basi kilichokuwa copied sio idea kama unavyoeleza!

Unapochukua maudhui ya filamu ya mtu mwingine lazima mfanye makubaliano... haitoshi tu ku-acknowledge. Ngoja nikuulize... umeshapata kusikia kampuni ya utengenezaji filamu imenunua filamu ambayo imeshachezwa? Kama hujasikia, basi mazingira yenyewe ndo kama haya ya JB na filamu ya Kihindi, kwamba baada ya JB kuiona hiyo hiyo fulani na kuipenda basi alitakiwa kuongea na wenyewe na kufikia makubaliano... ama kwa kuuziana au kupeana bure! Lakini hata kama angepewa bure, bado mmiliki wa Ladies VS Ricky Bahl angependa kufahamu what will happen akitokea mtu mwingine akaiona filamu ya JB ambayo maudhui ni ya Ladies VS Ricky Bahl! Assume kuna Peoducer wa Hollywood ameiona filamu ya JB na akaipenda na hivyo kuamua kuinunua ili akaitengeze upya (hii inafanyika sana Hollywood)! Sasa katika mazingira kama hayo haiwezekani, kwa mfano huyo Producer wa Hollywood amlipe JB $ 500 million halafu pesa hiyo iwe ya JB wakati original work ni ya Mdosi! Ndio maana nikasema kwamba, hata ikitokea Mdosi amempa JB filamu bure na yeye kusubiria tu acknowledgement lakini lazima atahitaji kufahamu anapotokea mtu mwingine nani atapata nini! Hii haitofautiani sana na suala la uuzaji wa wachezaji! Leo hii TP Mazembe wakimuuza Mbwana Samatta, lazima kutakuwa na mgao utakaokuja Simba!

Pili umezungumzia suala la Hollywood kutengeneza filamu zao kwa kutokea kwenye novel na religious books! Tuache hilo la religious books na tujikite kwenye novels! Kwanza kabisa, sina hakika kama umewahi kuiona mikataba ya uuzianaji wa script kwa Hollywood! Kwenye mkataba, Mwandishi lazima useme ikiwa script ni original material or adapted material (from novel)! Kama material ume-adapt kutoka kwenye novel, hiyo script huwezi kuuza wala ku-option unless umethibitisha kwamba umekuwa granted right ya ku-adapt novel husika lakini sio unasema tu based on novel so and so, ndo basi tena!

Hilo la sequel labda nikuambie jambo moja! Producer/Production Company inaponunua script yako, kwenye mkataba lazima utakuta kipengele kinachosema wazi kwamba script unayouza unauza pamoja na haki ya utengenezaji wa sequel kupitia script yako! Therefore hata sequel nazo zinakuwa zimelipiwa!!! Leo hii ukitengeneza T-shirt ukazi-lable Taken kwa kumaanisha hiyo movie, basi lazima nayo uwalipe wamiliki wa filamu husika! Na hapa ndio maana linapokuja suala la mikataba, Hollywood wanataka ONLY Entertainment Lawyer coz' kuna mambo mengi kwa lawyer asiye kwenye industry hawezi kuyafahamu! Hii maana yake ni nini? Ingawaje Mkataba unamtaka Mwandishi anapouza script yake anauza na haki yakutengeneza sequel plus any other materials kama vile T-Shirt lakini Mwanasheria wa Mwandishi wa Script nae atataka kufahamu kwamba, pamoja na kwamba mteja wake anauza hadi haki ya utengenezaji wa sequel, t-shirts na mambo mengine... je, atakuwa compensated vipi? Hapa ndo unakuta mkataba unasema pamoja na kwamba anauza hizo haki, lakini akitokea mtu mwingine akataka kutengeneza series kupitia the same script basi mwandishi atapata kiasi fulani kwa idadi fulani ya episodes! Au, atapewa one payment ya kiasi fulani!

Mwisho umemalizia kwamba hata Hollywood ideas zimeisha na wamebakia kwenye re-make... you're right lakini naomba nikukumbushe tena tusichanganya idea na contents... hivi ni vitu viwili tofauti! Aidha kwamba movie fulani ya Hollywood ni copy and paste ya movie nyingine ya UK nayo sio hoja kwavile hakuna anayekataa kwamba hakuna copy and paste provided wahusika walikubaliana!

Kwa waliipitia chuo watakuwa wanaelewa kuhusu INTELLECTUAL PROPERTY RIGHTS ambapo uko utakuta mambo ya patents, copyrights na mambo ya trade mark. Ninaposema IPR namaanisha creations of minds kama music, literature and other artistic works, alichokifanya JB ni COPYRIGHT INFRINGEMENT, yaani ka produce kitu ambapo kimeshakuwa produced, sio haki kisheria, ndio maana kila siku wasanii mnapigiwa makerere mrudi shuleni ndo matokeo yake haya
 
Point hapa warumi ni kutoa ushauri kama ulioutoa hapo!!

Na siyo Kumkandia JB kwa maneno ya dharau as if ye ni wa kwanza kucopy!!!

Ushauri tu inatosha!!!

Ukitaka kumtetea mtu usitumie maneno hayo '"as if yeye ni wa kwanza kukopi"
Hivi unajua kwanini tumelivalia njuga hili tukio? Unafikiri hatujui wengine walio kopi?
JB tunamsema kwakuwa hatukutegemea vitendo kama hivi kufanywa na yeye!
 
Last edited by a moderator:
Kwa waliipitia chuo watakuwa wanaelewa kuhusu INTELLECTUAL PROPERTY RIGHTS ambapo uko utakuta mambo ya patents, copyrights na mambo ya trade mark. Ninaposema IPR namaanisha creations of minds kama music, literature and other artistic works, alichokifanya JB ni COPYRIGHT INFRINGEMENT, yaani ka produce kitu ambapo kimeshakuwa produced, sio haki kisheria, ndio maana kila siku wasanii mnapigiwa makerere mrudi shuleni ndo matokeo yake haya

JB ameingia mkenge ni haki yake kusulubiwa maana ametia aibu..
 
Wabongo Mnapenda Sana Majungu.Mnatutemea Mimate Tu Humu.TambiTumbo Ni Mbunifu.Na Ndoman Kaitendea Haki Ile Muvi.Na Kama Inshu Ni Kucopy Mshaambiwa Hajaanza Yeye Na Wala Sio Yeye Atakua Wa Mwisho.Na Kama Kosa Lake Ni Kutokumuacknowledge Mtunzi Wa Origianal Muvi.Wakulalamika Ni Muhindi Sio Nyie Wabongo.Labda Niwaulize Swali Nyie Wahindi?.Nyie Kinachowafanya Mtutemee Mimate Humu Ni Gerous Zenu 2.Huyo Zamaradi Mwenyewe Alijifanya Kuja Na Aidea Yake.Matokeo Yk Katulea Mimavi Mitupu.Sasa Ipi Bora?.Sisi Tunataka Burudani.Mambo Ya Kucopy Na Kupaste Mnajua Nyie Wahindi.Mambo Ya Kuchamba Kwingi Hayo Mnayajua Nyie.Big Up TambiTumbo Umeidhihirishia Jamii Kua " Old Is Gold".Utamuacknowledge Mtunzi Kwenye Part3 Ili Masnitch Walidhike.Na Tunaisubiri Kwa Hamu Part3 Na 4 Pia.Kumbukeni Kua Hapa Ni " Bongo " Na Hii Ndo " Bongo Muvi ".

Kumbe ukweli ni majungu?
Kumbe kukopi maudhui ya kazi ya mtu ni ubunifu?Hivi umesoma ulicho kiandika?
 
JB ameingia mkenge ni haki yake kusulubiwa maana ametia aibu..

Ni kosa kisheria kukopi mawazo ya mtu mwingine tena bila kumtaarifu muhusika. Na ndio maana kwenye movie nyingi uandika "ni marufuku kukopi movie hii na soundtrack iliyomo kwenye filamu hii bila idhini ya muhusika, hatua kali za kisheria zitachukuliwa"
 
Moyo wa Mtanzania umejaa "uselfish" na siyo kwamba hawez kureason vitu kwa Utashi mpana, NO, ni chuki tu na kutopenda kuona Mtanzania mwenzao anawazid kwa kitu flani ndo kunafanya wasijishughulishe kufatilia vitu kwa kina zaidi..(black folks wanaHate kuona Black mwenzao Anafanikiwa)..

Hiyo Movie ya Ladies Vs Ricky Bahl (ya Anushka Sharma na Ranveer) ilileta controvesy kubwa wakat inatoka kwa Critics na wapenz wa movie bollywood, coz walicopy idea nzima kwenye Movie ya Hollywood ya mwaka 2006 ya "JONH TUCKER MUST DIE"..Anushka Sharma alizunguka kila sehem kupinga hizo shutuma, lakin haikuficha ukweli kuwa Yash Raj waliCopy hiyo movie..

Je walitoa Acknowledgement kwa Crew ya Jonh Tucker Must die???..

Na je pia walitoa Acknowledgement kwa crew ya "Chasing papi" (2003) huko nako si waliiba ideas??

Salman khan na Govinda kuhusu copy kila kitu kwenye Movie ya HiTCH ya Will Smith katika Movie yao ya "Partner"??? walitoa Acknowledgement kwa Will Smith?

Hollywood Sahiv wamebase katika Mkondo wa movie za Aina nne!!!

1. Si-ci fiction Movies (sicience fictions)
2. Adventures & historical Movies
3. Novel based movies
4. Super heroes (insparation from Comic books)

movies nying za Adventures and Historical movies nying sana huwa zinatoka kwenye novel, au religious history (Nothing new)

katika Science fiction ndo kabisa, sequal zipo nying sana, Hollywood wamefeli kudevelop new stories kwa upande huu, sequal ni nyingi, Ellysium, Specific rim etc zote zilishindwa kufikia matarajio ya wengi!!!

Mfano mdogo kuna Taken ( Action) ya Liam Neeson, kila mwaka ni Sequal tu, hatujuia next sequal itakuwaje!!

Sahiv kuna 50 shades of Grey (love story) ile ni NOVEL..

Movie industry imepungukiwa ideas, Viwanda vikubwa vya movies dunian (Hollywood na Bollywood) vimebase sana katika "Re-Make" na siyo Actual ideas!!!!

So suala la kucopy ideas ni kitu cha kawaida saaana Aisee!!

Death at a funeral(chris rock) ya US ni copy and paste ya ile ya UK.

So kabla hamjampigia makelele JB kampigieni makelele, Anushka Sharma na kampuni ya Yash Raj kwa kucopy movies za hollywood kwenye hiyo hiyo movie!!!!

View attachment 230879

Umeandika mambo mengi lakini umejikuta unashindwa kumtetea kwa hoja zenye nguvu bali hoja dhaifu sana!

Hivi kwakuwa wahindi walikopi Hollywood kwa hiyo inampa haki JB kukopi? Kwanini aliandika yeye ndio mtunzi wa story? Yani tusifie upuuzi wa JB kwa upuuzi wa wa hindi?

Kwa hiyo unajaribu kusema JB ni msanii asiye jiweza ndio maana ana kopi? Kwanini ana kopi wakati script writter ni wengi tuu nchini?

Utetezi huu ni dhaifu sana na unaendelea kumdhalilisha JB
 
Mkuu MosDef
Umeongea vitu vingi sana lakini inabidi ufahamu kwamba hakuna hatimiliki ya idea/wazo... Kwa maana nyingine, haikatazwi kutumia idea ya movie nyingine! Hapa naona unachanganya kati ya Idea (Wazo) na Maudhui (Contents)... hivi ni vitu viwili tofauti! Mwandishi wa JB ameeleza vizuri... alichokopi yeye sio idea/wazo bali ni maudhui/content!

Unapochukua maudhui ya filamu ya mtu mwingine lazima mfanye makubaliano... na kwa kawaida, hapo lazima biashara ifanyike! Lakini kwa JB hata kama angepewa bure, bado mmiliki wa Ladies VS Ricky Bahl angependa kufahamu what will happen akitokea mtu mwingine akaiona filamu ya JB ambayo maudhui ni ya Ladies VS Ricky Bahl! Assume kuna Peoducer wa Hollywood ameiona filamu ya JB na akaipenda na hivyo kuamua kuinunua ili akaitengeze upya (hii inafanyika sana Hollywood)! Sasa katika mazingira kama hayo haiwezekani, kwa mfano huyo Producer wa Hollywood amlipe JB $ laki 3 halafu pesa hiyo iwe ya JB wakati original work ni ya Mdosi... hapo mmiliki wa Ladies VV Ricky lazima apewe chake! Hii haitofautiani sana na suala la uuzaji wa wachezaji! Leo hii TP Mazembe wakimuuza Mbwana Samatta, lazima kutakuwa na mgao utakaokuja Simba!

Pili umezungumzia suala la Hollywood kutengeneza filamu zao kupitia novels! Kwanza kabisa, sina hakika kama umewahi kuiona mikataba ya uuzianaji wa script kwa Hollywood! Kwenye mkataba, Mwandishi lazima useme ikiwa script ni original material or adapted material (from novel)! Kama material ume-adapt kutoka kwenye novel, hiyo script huwezi kuuza wala ku-option unless umethibitisha kwamba umekuwa granted right ya ku-adapt novel husika!

Hilo la sequel labda nikuambie jambo moja! Producer/Production Company inaponunua script yako, kwenye mkataba lazima utakuta kipengele kinachosema wazi kwamba script unayouza unauza pamoja na haki ya utengenezaji wa sequel! Therefore hata sequel nazo zinakuwa zimelipiwa!!! Leo hii ukitengeneza T-shirt ukazi-lable Taken kwa kumaanisha hiyo movie, basi lazima nayo uwalipe wamiliki wa filamu husika! Na hapa ndio maana linapokuja suala la mikataba, Hollywood wanataka ONLY Entertainment Attorneys coz' kuna mambo mengi kwa lawyer asiye kwenye industry hawezi kuyafahamu! Hii maana yake ni nini? Ingawaje Mkataba unamtaka Mwandishi anapouza script yake anauza na haki yakutengeneza sequel plus any other materials kama vile T-Shirt lakini Attorney wa Mwandishi nae atataka kufahamu, pamoja na kwamba mteja wake anauza hadi haki ya utengenezaji wa sequel, t-shirts na mambo mengine... je, atakuwa compensated vipi? Hapa ndo unakuta mkataba unasema pamoja na kwamba anauza hizo haki, lakini akitokea mtu mwingine akataka kutengeneza (say) series kupitia the same script basi mwandishi atalipwa kiasi fulani kwa idadi fulani ya episodes! Au, atapewa one payment ya kiasi fulani!

Mwisho umemalizia kwamba hata Hollywood ideas zimeisha na wamebakia kwenye re-make... you're right lakini naomba nikukumbushe tena tusichanganya idea na contents... hivi ni vitu viwili tofauti! Aidha kwamba movie fulani ya Hollywood ni copy and paste ya movie nyingine ya UK nayo sio hoja kwavile hakuna anayekataa kwamba hakuna copy and paste provided wahusika walikubaliana!

Basi nilichokosea hapo ni kuweka suala la idea badala ya Maudhui!!!

Coz nilikuwa nikisema Idea, nilikuwa namaanisha kila kitu!!!

Coz kama umeangalia Movie ya partner ya Salman khan na ile ya "HITCH" utagundua kuwa CONTENTS (kile ambacho unazungumzia zaid) imechukuliwa yote!!!!

Critics waliiponda Ladies Vs Ricky Bahl, Coz ilikuwa imechukua kila kitu kutoka Kwenye John Tucker Must Die, na some Contents kutoka kwenye ile Chasing Papi...

Critics huwa hawapondi Uchukuaji wa ideas, huwa wanaponda uchukuaji wa Contects, ingekuwa hivyo basi Movie za kihindi kibao zingepondwa, kama HNY ya SK, BodyGuard ya Salman, Jaan Dushman ya kina Akshay, Etc hizi zote wamedevelop stories za Hollywood!!

kwenye suala la Sequel, nilikuwa namaanisha suala la ideas (MAUDHUI kama unavyomaanisha) limekuwa gumu sana sahiv, na ubaya watazamaj wamekuwa wakidemand zaid sequels kwenye upande wa Si-ci au comic movies kuliko new inventory, kwasababu mwisho wa siku maudhui yanakuwa yale yale tu, Mfano lastest movies za KisuperHeroes ni Captain America, Thor, Iron Man etc, ambapo ukiziangalia ni ideas zile zile tu za SpiderMan, Superman, batman na WonderWoman, hakuna kipya hapo, Thats why wakipresent idea mpya na ikibamba basi utakuwa ni mwendo wa Sequal tu, Thor ina sequal, Captain America, Iron Man etc!!!

Nilichokuwa namaanisha hapa ni kwamba, copying katika Viwanda tofauti vya movies duniani ipo, Bollywood wanacopy sana movies za Hollywood, SANA, najua ni ilegal lakin sijawah kusikia ikileta tatizo kabisa, NA critics wa Bollywood wasingekuwa wanalalamika sana kama Kweli crew za movie husika zingekuwa zinashirikishwa katika hili!!!!

Me ninachoshauri, ni kuwaambia Wasanii wakibongo wadeal na ideas na Siyo Contents kama unavyosema, na pia ningewaambia Bollywood the Same thing!!!
 
Last edited by a moderator:
Umeandika mambo mengi lakini umejikuta unashindwa kumtetea kwa hoja zenye nguvu bali hoja dhaifu sana!

Hivi kwakuwa wahindi walikopi Hollywood kwa hiyo inampa haki JB kukopi? Kwanini aliandika yeye ndio mtunzi wa story? Yani tusifie upuuzi wa JB kwa upuuzi wa wa hindi?

Kwa hiyo unajaribu kusema JB ni msanii asiye jiweza ndio maana ana kopi? Kwanini ana kopi wakati script writter ni wengi tuu nchini?

Utetezi huu ni dhaifu sana na unaendelea kumdhalilisha JB

sijaja kwa ajili ya kumtete JB hapa!!

Nilichotaka kukiweka, Copying katika Movies, ni tatizo la dunia nzima katika viwanda vya Movies duniani!!

So ulichotakiwa kukileta hapa, ni kwann suala la KuCopy maudhui ya Movies zilizochezwa awali limekuwa kubwa???? kiini chake ni nini???
 
Ukitaka kumtetea mtu usitumie maneno hayo '"as if yeye ni wa kwanza kukopi"
Hivi unajua kwanini tumelivalia njuga hili tukio? Unafikiri hatujui wengine walio kopi?
JB tunamsema kwakuwa hatukutegemea vitendo kama hivi kufanywa na yeye!

Typical Tanzanian!!

So kama ungeanza kupiga makelele kuhusu suala la kucopy movies za nje kwa hao wengine unaowajua, unafikiri huyo usiyemtegemea (JB) kufanya hicho kitu Angethubutu kufanya???

So Ray, Mtambalike and Co. wakicopy ni sawa tu?? but since JB ambaye ndo anatakiwa kuwa m-bunifu (Kuliko wote) akiCopy ni tatizo???

Hawa wengine wanaoperate kwenye mfumo gani wa Movies hapa bongo???

Wapo tofauti na huyo JB???
 
Kwa waliipitia chuo watakuwa wanaelewa kuhusu INTELLECTUAL PROPERTY RIGHTS ambapo uko utakuta mambo ya patents, copyrights na mambo ya trade mark. Ninaposema IPR namaanisha creations of minds kama music, literature and other artistic works, alichokifanya JB ni COPYRIGHT INFRINGEMENT, yaani ka produce kitu ambapo kimeshakuwa produced, sio haki kisheria, ndio maana kila siku wasanii mnapigiwa makerere mrudi shuleni ndo matokeo yake haya

Tanzania tunayo hiyo Sheria, na USA kuna kipind ilikuwa signed na kupitishwa kama Criminal offense..

Kwa mtazamo huo, Tungekuwa tunafata Strictly law inavyosema, Tusingekuwa na hizi CD's za kina Albaba, AK-47 etc, na pia tusingekuwa na Kina LUFUFU au JUMA KHAN!!

So why Can't you just Blame the laws???

Kama ulikuwa unalijua hili suala la IP, kwann tangu awali usingetumia Influence yako KUBWA uliyonayo kwenye hili jukwaa kupinga hizi ishu??? coz am sure ungeanza tangu zaman kuziEnforce hizo sheria humu, akina JB wasingethubutu kucopy tangu hizo enzi za kina "regina"..
warumi, movie industry duniani kote itakosa msisimko kama Hiyo sheria ikiwa implemented strictly!!!

Kiwanda kingine kuAcknowledge movie ya kiwanda kingine after copying it ni NGUMU, thats why unaona hata Big heads wa kwenye movies industry kama Bollywood wanaCopy contents za Hollywood!!!
 
Last edited by a moderator:
Umeandika mambo mengi lakini umejikuta unashindwa kumtetea kwa hoja zenye nguvu bali hoja dhaifu sana!

Hivi kwakuwa wahindi walikopi Hollywood kwa hiyo inampa haki JB kukopi? Kwanini aliandika yeye ndio mtunzi wa story? Yani tusifie upuuzi wa JB kwa upuuzi wa wa hindi?

Kwa hiyo unajaribu kusema JB ni msanii asiye jiweza ndio maana ana kopi? Kwanini ana kopi wakati script writter ni wengi tuu nchini?

Utetezi huu ni dhaifu sana na unaendelea kumdhalilisha JB

Nilivyosoma hii comment ikabidi niangalie nani ka comment aseh, kuanzia Leo kaa ukijua warumi anakukubali sana yani, bonge la comment bro salute sana
 
Last edited by a moderator:
Tanzania tunayo hiyo Sheria, na USA kuna kipind ilikuwa signed na kupitishwa kama Criminal offense..

Kwa mtazamo huo, Tungekuwa tunafata Strictly law inavyosema, Tusingekuwa na hizi CD's za kina Albaba, AK-47 etc, na pia tusingekuwa na Kina LUFUFU au JUMA KHAN!!

So why Can't you just Blame the laws???

Kama ulikuwa unalijua hili suala la IP, kwann tangu awali usingetumia Influence yako KUBWA uliyonayo kwenye hili jukwaa kupinga hizi ishu??? coz am sure ungeanza tangu zaman kuziEnforce hizo sheria humu, akina JB wasingethubutu kucopy tangu hizo enzi za kina "regina"..
warumi, movie industry duniani kote itakosa msisimko kama Hiyo sheria ikiwa implemented strictly!!!

Kiwanda kingine kuAcknowledge movie ya kiwanda kingine after copying it ni NGUMU, thats why unaona hata Big heads wa kwenye movies industry kama Bollywood wanaCopy contents za Hollywood!!!

Well said mkuu, ila lengo la huu uzi ni kumkumbusha JB kutojibweteka , maana hii kashfa ya kukopi movie sio Mara ya kwanza na haipendezi kuendekeza kuiga movie mpaka watu wanagundua, inashusha sana hadhi ya msanii..

Nadhani hii scandal pia ilishawahi kumtafuna Eric shigongo kuwa uwa anatafsiri novel za nje na kuziweka kwenye magazeti yake , ila mpaka kesho hakuna aliyewahi kuthibitisha uvumi huo, hivyo kwake inabaki kuwa tetesi tu ila kwa JB big no asiendekezwe kiasi hiko bwana
 
Sawa Mkuu umehitimisha vyema!!
Ila nguvu ya matusi iliyotumika awali ni wazi kuwa watu wengi tunaojibebesha mamlaka ya kukosoa haya mambo wengi wetu hatufuatilii kwa undani sana mambo haya.

Mos Def amejitahidi kusawazisha mjadala kwenye maeneo mengi. Hapo awali kwa watu tusioweza kupayuka na kutukana tulishindwa kuwasilisha zaidi.
Nadhani ni vyema tujenge utamaduni wa hii mijadala katika namna ya kujenga zaidi.
Hapo awali kwa kupitia jukwaa la burudani kule tulikuwa na Bishop Hiluka kama nomekosea jina anisamehe, Hiluka ni mwandishi sana wa masuala ya tasnia ya filamu na pia ameshiriki miradi kadhaa.
Kwa bahati mbaya wakati wa mijadala kule hakukuwa na hamasa sana kama inavyoonekana mda wa matusi na kejeli.

Itapendeza hili likitupa mwanzo mpya wa kuitumia JF kutengeneza fukuto la walaji wa kazi za sanaa ambalo tutakuwa na ufahamu mpana wa sanaa na hivyo kuyaelewa mazingira ya utendaji kazi wa wasanii wetu na kiwanda chetu kwa ujumla, hatimaye maoni tutakayokuwa tukitoa hata wadau watajua duh kweli JF ni soo.

Pamoja katika Tasnia!!
 
AGREED warumi
 
Last edited by a moderator:
Dah! Hii nchi tunachukulia mambo kirahisi rahisa sana labda kv tunaona tupo kisiwani kumbe tunasahau kwamba mtu kama JB anapofanya kitu kama hicho, si tu kwamba mwenyewe anajishusha bali movie yake hata ikibamba namna gani hatakuwa na ubavu wa kuifikisha kwenye platform ya kimataifa!

Mkuu Ruttashobolwa, nimeona kuna mahala umazungumzsia suala la ku-acknowledge... itoshe tu kusema kwamba katika issue kama hii ya JB, ikiwa ipo kama inavyosemwa, basi hapo hakuna suala la ku-acknowledge! Una acknowldge kitu ambacho umekopi kwa kiasi kikubwa kiasi hicho? Yaani linapokuja suala la hati miliki, moja kwa moja huo ni wizi! Unaposikia suala la ku-acknowledge kwenye movie, wenyewe wanaita kutoa credit ni pale, assume chige nimeandika script nimekuuzia Rutta... umenilipa pesa yangu yote kwa 100%! Pamoja na yote hayo bado ukishatengeneza movie unalazimika kutoa credit kwangu! Au baada ya wewe kuuzia script na ukatoa filamu, kisha mtu mwingine akanunua script kutoka kwako (kv ulishaimiliki) na akatengeneza series, pamoja na yote hayo bado mtengeneza series anatakiwa kutoa credit kwa chige! Lakini kwa issue ya JB ikiwa inavyosemwa ndivyo ilivyo hapo hakuna cha ku-acknowledge/ kutoa credit wala nini bali moja kwa moja inaingia kwenye suala la wizi! Tena yeye amekopi movie lakini hata kama ingekuwa amepata script tu ya hiyo movie na movie yenyewe ilikuwa haijatengenezwa, kwa staili hiyo pia inaingia kwenye kundi la wizi na wala hakuna cha kutoa credit wa ku-acknowledge hapo!!

Kitu ambacho kinakubalika kwenye movie/series ni kimoja! Kwanza, unaweza kuchukua portion ndogo sana ya movie/series/script... hapa nazungumzia scene isiyofikia hata dakika moja kisha ukai-develop into a new script! Hilo linakubalika na wala hautahitajika ku-acknowledge lakini unachukua madakika kadhaa... wakikudaka, fahamu umekwisha labda ujivune kwamba li nchi lenyewe hili halina taratibu!

Kwa wenzetu wapo very script na ndio maana mahali kama US, hata mwandishi anashauriwa kuwa na entertainment lawyer! Mwenyewe nili-join context fulani hivi nikajifanya kutafuta entertainment lawyer... wewe! Hiyo bei ambayo nilitajiwa ya kumlipa kwa saa nikalazimika kupeleka mambo kibongo bongo na badala yake nikaamua tu kuisajili kwenye registry ya Writers of America (sio copyright) coz' it serves the purpose to some extent! Na hapo kumbuka hakuwa lawyer kwa ajili ya A-List writers bali ni lawyers wa kawaida tu! Sasa mtu hawezi kumlipa lawyer kwa $$$ kadhaa halafu aje mwingine achukue tu kazi yake kirahis rahisi!

Huna lolote wewe hata darasani unajulikana kwa kutoa photocopy maana umepitiliza kwenye copy and paste. Bongo kucopy na kupaste ni kitu cha kawaida so punguza kuhukumu mwemzako mfyuuuu.
 
Sawa Mkuu umehitimisha vyema!!
Ila nguvu ya matusi iliyotumika awali ni wazi kuwa watu wengi tunaojibebesha mamlaka ya kukosoa haya mambo wengi wetu hatufuatilii kwa undani sana mambo haya.

Mos Def amejitahidi kusawazisha mjadala kwenye maeneo mengi. Hapo awali kwa watu tusioweza kupayuka na kutukana tulishindwa kuwasilisha zaidi.
Nadhani ni vyema tujenge utamaduni wa hii mijadala katika namna ya kujenga zaidi.
Hapo awali kwa kupitia jukwaa la burudani kule tulikuwa na Bishop Hiluka kama nomekosea jina anisamehe, Hiluka ni mwandishi sana wa masuala ya tasnia ya filamu na pia ameshiriki miradi kadhaa.
Kwa bahati mbaya wakati wa mijadala kule hakukuwa na hamasa sana kama inavyoonekana mda wa matusi na kejeli.

Itapendeza hili likitupa mwanzo mpya wa kuitumia JF kutengeneza fukuto la walaji wa kazi za sanaa ambalo tutakuwa na ufahamu mpana wa sanaa na hivyo kuyaelewa mazingira ya utendaji kazi wa wasanii wetu na kiwanda chetu kwa ujumla, hatimaye maoni tutakayokuwa tukitoa hata wadau watajua duh kweli JF ni soo.

Pamoja katika Tasnia!!

Tena huyo warumi sijui ke au me apunguze lugha zake za kipuuzi mkosoe mtu kistaarabu atakuelewa mwanzo wa thread ameonge maneno machafu sana. Pamoja na yote aliyokosea jb lakini tukumbuke ni mwanadamu pia sasa mwanume unamwita litumbo sijui nini sio fresh. Warumi na hii sio mara moja kujifanya yeye ni Mungu wa jukwaa hili hizo tabia acha bwana umekaa kimajungu majungu tu kama muuza kahawa. UNABOA SANA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI YA JF.
 
Huna lolote wewe hata darasani unajulikana kwa kutoa photocopy maana umepitiliza kwenye copy and paste. Bongo kucopy na kupaste ni kitu cha kawaida so punguza kuhukumu mwemzako mfyuuuu.

Hapa umeandika nini? umemtetea?Kama ni kweli ni jambo la kawaida kwanini JB alindika yeye ndio mtunzi wa story?Kwanini hadi sasa ana kaza shingo pamoja na ukweli unajulikana?
 
Sawa Mkuu umehitimisha vyema!!
Ila nguvu ya matusi iliyotumika awali ni wazi kuwa watu wengi tunaojibebesha mamlaka ya kukosoa haya mambo wengi wetu hatufuatilii kwa undani sana mambo haya.

Mos Def amejitahidi kusawazisha mjadala kwenye maeneo mengi. Hapo awali kwa watu tusioweza kupayuka na kutukana tulishindwa kuwasilisha zaidi.
Nadhani ni vyema tujenge utamaduni wa hii mijadala katika namna ya kujenga zaidi.
Hapo awali kwa kupitia jukwaa la burudani kule tulikuwa na Bishop Hiluka kama nomekosea jina anisamehe, Hiluka ni mwandishi sana wa masuala ya tasnia ya filamu na pia ameshiriki miradi kadhaa.
Kwa bahati mbaya wakati wa mijadala kule hakukuwa na hamasa sana kama inavyoonekana mda wa matusi na kejeli.

Itapendeza hili likitupa mwanzo mpya wa kuitumia JF kutengeneza fukuto la walaji wa kazi za sanaa ambalo tutakuwa na ufahamu mpana wa sanaa na hivyo kuyaelewa mazingira ya utendaji kazi wa wasanii wetu na kiwanda chetu kwa ujumla, hatimaye maoni tutakayokuwa tukitoa hata wadau watajua duh kweli JF ni soo.

Pamoja katika Tasnia!!

Well said..hapa lengo ni kuhakikisha tunawambia ukweli ili wasirudie makosa.
 
Well said..hapa lengo ni kuhakikisha tunawambia ukweli ili wasirudie makosa.

Rutta na warumi nyie sio wakosoaji bali lengo ni kumdharirisha mtu lugha zenu sio nzuri kabisa. Nandomana naona kama kukopi na kupest jb sio wa kwanza labda mna mengine. Maana jouneGwalu alifafanua hii issue kwa kumqoute manege lakini mlikuja na abusive language kitu ambacho sio fresh.
 
Typical Tanzanian!!

So kama ungeanza kupiga makelele kuhusu suala la kucopy movies za nje kwa hao wengine unaowajua, unafikiri huyo usiyemtegemea (JB) kufanya hicho kitu Angethubutu kufanya???

So Ray, Mtambalike and Co. wakicopy ni sawa tu?? but since JB ambaye ndo anatakiwa kuwa m-bunifu (Kuliko wote) akiCopy ni tatizo???

Hawa wengine wanaoperate kwenye mfumo gani wa Movies hapa bongo???

Wapo tofauti na huyo JB???

Huu ni uwanja na mada inayo muhusu JB.. kama hao wengine wakikopi tukathibitisha nao tuta wasema lakini hatuwezi kumtetea JB kwa kigezo ana fanya kama wengine..unatakiwa kujua JB ni msanii mwenye nguvu katika soko la sanaa ndio maana mjadala wake umeteka sana hisia za wengi..kwakuwa ni mmoja ya wasanii wanao tazamwa sana..

Ningekuwa yeye ninge jivunia sana kwa kuthibitisha natazamwa sana maana si rahisi kutega mijadala kama huna ushawishi kwenye soko..kabisa..nani kuhakikishia Filamu hii kauza sana na inayo fata atauza sana maana kila mmoja atataka kujua kafanya nini

Mimi namfatilia sana JB sio kwamba nachangia tuu bali ni mmoja wa wateja wake na ni msanii wa kiume bongo ninaye amini ana uwezo mkubwa sana lakini kwenye hili siwezi kumfumbia macho kabisa..ameharibu.
 
Back
Top Bottom