JB na Skendo mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

Jmn I have something to say in this. Ni hivi Sanaa ya bongo wangekuwa serious kama mbele wangefika mbali sana. Jmn muziki Wa Tanzania utakuwa simply bcoz watu wapi talented. Na wale ambao wanadandia unaona tuu mwisho Wa siku watafifia wapotee kabisa. Ila kwenye bongo movie hawawezi kufika mbali koz hawana hizo talent na hawapo serious na kazi zao. Wana kopy sana I think hata Dereva tax imekuwa copied amecheza jb na wolper. Tho walicheza vzr I don't remember kama waliacknowledge MTU mule. Maybe wanaiga idea za Nigeria mfano movie ya guardian angel ya Ramsay so ameiga hatia sijui ya kiindi. Exactly the same tena hawa hadi wakaimba kbsa. Na mvua ikanyesha kama wahindi wanavyopenda mvua kwenye movie zao. Sasa sisi creativity inakuwa zero
 
We mtu anaenda kumchukua msichana nzuri aje auze sura kwenye movie. Jmn kwely whether anajua kuact ama laah. Link tutatoka kwa style hiyo
 
kwa JB hii si mara ya kwanza..
kuna ile movie yake inaitwa REGINA...nayo alikopi kutoka kwa '' DELIVER US FROM EVA''

JB Ni msanii mwenye heshima sana na ana kiwango kizuri tu..ila hiki ki tabia kinaharibu sana
 
Kiepe Yai , Hawa wasanii wetu wakiibiwa kazi zao wanalalamika mpaka ikulu, ila wao kuiba za wenzao unaona haina shida kisa burudani?

Hichi ndio kinaweza kushangaza zaidi wakati mtu ana dai kuwa kazi zao zina ibiwa mtaani kumbe na yeye ana kopi kazi za watu halafu tukihoji ana kasirika! Kwa mwendo huu watu wana haki ya kuiba hii kazi maana hata yeye si yake..
 
mbona wote wanaibaga kwenye movie za bollywood au nollywood jb sio wa kwanza ndo zao

Teh Teh huwa mnanishangaza na hoja zenu! Kwa hiyo JB hana uwezo wa kutunga kama hao wanao kopi? Kama ni hivyo kwanini asitangaze ana hitaji story kuliko ku kopi? Kwa hiyo JB aendelee kukopi kwa kuwa wengine walikopi?
 
kwa JB hii si mara ya kwanza..
kuna ile movie yake inaitwa REGINA...nayo alikopi kutoka kwa '' DELIVER US FROM EVA''

JB Ni msanii mwenye heshima sana na ana kiwango kizuri tu..ila hiki ki tabia kinaharibu sana

Hii tabia ya kukopi ina muharibia sana halafu akiambiwa ukweli ana panick na hili ni tatizo la kutaka kuoneka yeye ni mtunzi mzuri na muigizaji mzuri kwa wakati mmoja!

JB namkubali sana kwenye kuigiza lakini kwenye utunzi namuomba awaachie wengine..hii kazi haiwezi.
 

JB hayuko serious kabisa!
 
kwa JB hii si mara ya kwanza..
kuna ile movie yake inaitwa REGINA...nayo alikopi kutoka kwa '' DELIVER US FROM EVA''

JB Ni msanii mwenye heshima sana na ana kiwango kizuri tu..ila hiki ki tabia kinaharibu sana
Isije hicho kiwango kizuri kikawa kinatokana na wizi wa kazi za watu wengine!!
 
Kwa uzoefu wangu kwenye haya mambo, Tanzania hatuna watunzi wazuri wa script na kama wapo bado hawajajitokeza na hawajajitokeza coz' ubabaishaji mwingi! Let me tell you something Rutta... kuandika na kuigiza ni viwili tofauti lakini kwa bahati mbaya wasanii wetu wanadhani kutunga ni kazi inayoweza kufanywa na mwigizaji yeyote yule! Wewe Rutta inawezekana hujawahi kabisa kuwa mbele ya kamera na wala hujawahi kabisa kufikiria kuwa mwigizaji! Hata hivyo, leo ikiwa kunakuwa na script mzuri na anapatikana director mzuri wa kukuelekeza, unaweza kucheza filamu husika na bado ukafanya vizuri ile mbaya lakini suala la kuandika, kama huna talent ya kuandika ndo basi huna unless upitie formal training ambazo TZ hakuna hata moja! Unaweza uka-pick at a random a sample of 100 people na kati yake usipate mwandishi hata mmoja mzuri lakini at the same time unaweza kufanya zoezi lile lile na ukapata waigizaji kibao ambao utatumia muda mfupi tu kuwa-train na ndio maana hata Hollywood kwenyewe huwezi kusikia kuna audition ya waandishi wa script lakini kila siku kuna audition ya waigizaji!!!!

Suala la uandishi ni very serious lakini wana filamu wetu wanalichukulia kirahisi rahisi tu na matokeo yake wanaishia kutengeneza filamu mbovu coz' msingi wa filamu yoyote ile ni script! Na kwa wale wanaotaka kuuhadaa umma kwamba wana uwezo wa kutengeneza kazi mzuri ndio hao akina JB wanaishia ku-copy na ku-paste kazi za watu wengine badala ya kutumia pesa kutafuta waandishi wazuri! Ukisikia siri ya filamu zetu zinavyotengenezwa, unaweza usiamini....
 
"Kwanza kabisa ningeanza kwa salam kwenu nyote na naamini muwazima wa afya.

Nimeamua kuandika ujumbe huu baada ya kuona na kupigiwa simu chache kuhusu "SKENDO" wa filamu Mzee wa Swagga kuwa imekopiwa.

Nijibu jibu fupi bila kusita kuwa kweli Story imekopiwa na original Story inaitwa Ladies Vs Ricky Bahl na mimi ndiye niliyemshauri JB kuichukua Story hiyo yenye maudhui ya kuvutia. Nataka nieleze sababu ya kufanya hivyo ila kabla sijaeleza sababu ningependa kuwaambia wale wote wanaotumia skendo hii kuyarefusha mambo haya kuwa kwenye ulimwengu wa filamu ni jambo la kawaida duniani watu kuchukua maudhui ya story na kuyatengeneza katika mazingira yao endapo maudhui hayo yataelimisha au kukosoa au kufurahisha kuhusu jambo..watakaoendelea kulalamika baada ya ujumbe huu ni dhahiri wanania zao nyingine na si kujenga.

Kwanza kabisa mimi ndiye mwandishi mkuu wa filamu za JB kuanzia enzi za DJ Ben, Dereva Taxi, Nakwenda kwa Mwanangu, Shikamoo Mzee, Bado Natafuta mpaka hii Mzee wa Swagga na hizo nyingine zote zikiwa ni original scripts kutoka kwenye ubongo wangu.

Filamu anazofanya JB ni Romantic Comedies na Inspirational Comedies kwa hiyo yeye huwa anapenda maudhui ya kuentertain zaidi yani filamu zenye kuchangamsha na kuburudisha tofauti na waigizaji wengine kama Single Mtambalike anayependelea filamu za ugentleman zaidi (haya ni kutokana na kukaa nao na kuzungumza nao na kuwafahamu kwa kina).

Sasa kuhusu Mzee wa Swagga:


JB alitengeneza filamu mfululizo zenye maudhui tofauti na alizozoeleka, kama Hukumu ya Ndoa, Mikono Salama ambazo sikuziandika mimi na nakiri kuwa hazikufanya vizuri sana sokoni.

Sababu ya filamu hizi kuandikwa na watu wengine ni sababu nilikuwa nashughulika na Script ya filamu yangu mwenyewe niliyoproduce mwaka jana October inayoitwa SAFARI YA GWALU (bado haijatoka mpaka mwezi wa 3 mwishoni), aliyoigiza Gabo kama kijana anayerudi shule ya msingi baada ya kupigika na maisha.

Filamu hii imenichukua mwaka mzima kuanzia kuiandika mpaka kuja kuproduce, kuandika ilianza January-march 2014 hivyo sikupata nafasi kumuandikia JB tangu tulipotoa BADO NATAFUTA na CHARLE MVUVI (bado haijatoka).

Baada ya filamu hizi mbili (Hukumu ya Ndoa na Mikono Salama);JB alinieleza angetamani nimuandalie Filamu na Mzee Majuto wakati huo wakiwa safarini kwenda Uturuki ili wakashoot Uturuki iwe filamu kali. Wakati nikiandaa filamu hiyo mshtuko mkubwa ukaja kwa misiba ya mfululizo ya wana Tasnia wenzetu iliyopelekea Safari ya JB na Mzee Majuto ya Uturuki kufa na hivyo kufanya hata script niliyoandaa kukosa msisimko tena.

Baada ya matatizo JB alitaka filamu inayofanana na Senior Bachelor, DJ Ben na Nakwenda kwa Mwanangu, akiigiza kama mburudishaji zaidi na kwa kuwa sikuwa na Idea mpya kwenye kichwa na muda ulikuwa unaenda sana na anahitajika kupeleka filamu yake kwa msambazaji ikabidi nitafute story itakayofanana na JB mburudishaji tunayemfahamu muda mrefu;

kwa ninavyomuelewa vizuri JB labda kuliko waandishi wengi wanavyomuelewa hiyo haikuwa ngumu kutafuta wazo la kumfaa na ndipo tukaipata Ladies Vs Rick Bahl, JB aliipenda ila sote tulikuwa na wasiwasi kwani JB ni muoga sana wa kuandikwa vibaya, nikamwambia jambo ambalo nataka niwaeleze nanyi leo. Jambo ambalo lilimfanya JB kukubali niandike script mpya kupitia kisa kile na kuiproduce...

Ukweli ni kuwa duniani kote (masoko ya filamu yote namaanisha) watu wanapoona maudhui ya story ya nchi au taifa jingine kuwavutia wanaweza kuchukua maudhui hayo na kuyatumia kutengeneza filamu za maudhui yale kwenye mazingira yao. Kuna Filamu nyingi hapa Tanzania na Nigeria na Bollywood Hata Hollywood zimefanyika hivyo na si dhambi.

Kama Tanzania tazama filamu Ya BEST MAN ya Hemedi na Yussuf Mlela, ni copy ya BEST MAN ya Morris Chestnut na Taye Diggs...

Nollywood filamu Ya GUARDIAN ANGEL ya Ramsey Noah ni copy ya Filamu HATYA ya Bollywood ya Govindah...
Pia filamu za ROMEO AND JULIET developed kutoka kwa William Shakespears plays zimekopiwa Bollywood kwenye filamu iliyoleta Mabadiliko makubwa Bollywood ya QAYAMAT SE QAYAMAT TAK kama nasema uongo mtu aziangalie na kuja kunikosoa na nitaleta dazeni ya filamu zilizokopiwa kutoka nchi na nchi.

Ila nataka kuuliza swali, mbona nyingine zilizokopiwa hapa Tanzania toka nje hazikuzungumziwa kama Mzee wa Swagga?

Nadhani jibu ni moja tu: sababu JB ameitendea haki filamu hiyo. Ila tusiende huko !

Jambo jingine (nadhani ndio la msingi zaidi), mnapokaa kulaumu mjue kazi ya kuwapa watazamaji kitu wanachotaka kila siku na kuwafanya wakupende si suala dogo, tunaumiza vichwa mchana na usiku.

JB si kwamba namfagilia sababu namuandikia ila huwa anaumia sana kutafuta story mpya na ukweli hata mimi nateseka sana kutengeneza vitu vipya na ukitazama mtu huyu mmoja atengeneze filamu 6 au 7 kwa mwaka na zote mzipende na kufurahia inahitaji kujitoa kwa hali ya juu.

Nikiwa kama mwandishi kihalali nahitaji kuandika script 2 tu kwa mwaka ili nitoe vitu vikali, unapoelemewa na mzigo ni rahisi kuharibu kazi na kwa kuwa tunajitahidi (mimi na JB) kuwapa mnachopenda basi huwa tunatafuta kila njia kutowakwaza mashabiki, naomba mtuhurumie nasi kwani mazingira ya kazi ni magumu mno.

Kwa haya niliyoandika ningependa kuwaambia tusiwe watu wa kulaumu na kuhukumu, mimi kuproduce filamu yangu mwaka jana kumepunguza kujitoa kwangu kuandaa filamu kali za JB, mimi ndiye wa kulaumiwa na si JB.

Na kwa niaba ya mashabiki wa JB nawaomba radhi kama kwa namna moja au nyingine mmejisikia vibaya ila kwa niliyoeleza mtaungana nami kuwa si dhambi kufanya hivyo inapobidi na tushirikiane kupeleka gurudumu hili mbele.

Nikiwa kama mwandishi bora wa script (Kama nilivyotambuliwa na ZIFF, JULY 2014 kupitia Filamu ya "SHIKAMOO MZEE") natambua jukumu langu kama mwandishi simkingii kifua JB bali nasimamia kile ninachokifanya kama Professional.

Naomba tuache kuongea na tushirikiane kuboresha filamu zetu."


Daniel Manege
 
mwizi ni mwizi tusiku hizi za mwizi ni 10 sio 40 tena kwa nini hauku aknowledge kama umeiba idea ya watu ulidhani watu hawaangalii za bollywood, bongo movie wengi ni failures division 5 hamko creative,hamjifunzi vitu vipya, hamuumizi vichwa mnashinda baa mtapata wapi muda wa kubrain storm kajipange tena uje na utetezi mwingine hii ni rubish
 

Upo sahihi Boss,

Hii stori ilikuwepo hapa kwenye "JB na Scandal mpya ya kuiba mawazo ya Movie ya ''Ladies Vs Ricky Bahl"

Mi nimefanya kuleta upande wa pili wa stori toka kwa muandishi wa husika,
ndio maana hiyo stori imekaa kama nanukuu tu.

Hivyo kwa kuweka kumbukumbu sahihi Mimi si Daniel Manege ila ni mjumbe wa JF kama ilivyo wewe.

Punguza munkari Boss!
 
so anataka kutuaminisha kwamba kwenye tasnia ya muvi kukopi na kupest kunaruhusiwa bila ku-acknowledge the source???
 
Khaaaaa! Jamaa kajielezea kwa unyenyekevu na bado anapewa za uso.....hii JF ndio maana celebrities wanaiogopa sana.

Hata mimi baada ya kuona Maelezo ya jamaa nikaona ni vyema kuwashirikisha waungwana wa upande huu.

Kuna vitu kimsingi vinatokea kwenye tasnia ya filamu hata mifano aliyotoa.

Ni bahati mbaya kuwa wabongo wengi tumekuwa watu wa mihemko tu.
 
na wewe ndio unafanya the same mistake ungesema mapema kuwa wewe sio muhusika bali umekopi kama huyo alivyokopi ahahahahaha pole sana
 
jaman i jamani jamani jamani, nyamazeni tu asije akatokea mmbeya wa kimataifa akawasiliana na hao wahindi jamani , mtafilisiwa hadi hayo mapumbu watayachukua
sasa mbona kwenye movie credit ya story JB ndo kajipa ? shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…