Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa na kv naona hapa chini umechanganya tena, ngoja nifafanunue! Sina shaka umeshaingalia Series ya 24! Sikumbuki ni Season gani, lakini kuna season moja, Chief of Staff (wa US), kupitia watu wake anafanya mchezo na kuwapatia magaidi mitungi ya nerve gas! Awali, Mwandishi ali-suspend lengo la Chief of Staff kutoa mitungi ya nerve gas kwa magaidi lakini baadae tukajuzwa kwamba, kumbe lengo la Chief Of Staff na watu wake ilikuwa ni kuwafanya Magaidi waondoke na ile mitungi ya gas (waliamini wangeenda nayo kwao) lakini Magaidi watakapofika Eastern Europe, Chief of Staff na watu wake wairipue ile mitunge remotely ili mataifa ya Eastern Europe yadhani ni shambulizi lililofanywa na Magaidi! Hiyo tayari ni idea... wewe unaweza kuchukua hiyo idea na kuandika script upya... na hilo kwenye filamu halikatazwi! Na katika uandishi wa script, moja ya source za idea ambazo zinakubalika ni hiyo... kwamba unachukua kipande kidogo sana cha filamu/series kisha unakiandikia upya bila contents kufanana! Na kama umeangalia hiyo season ninayoisema, hilo suala la magaidi kuondoka na nerve gas hadi Eastern Europe wala halikuendelezwa kwenye series kwahiyo hata wewe ukisema uandikie suala hilo itakuwa ni kitu kipya kabisa kv mwandishi wa series ali-divert matumizi ya hizo nerve gas na kutumika ndani ya US!
Ngoja nirudie kwa mara nyingine hapo kwenye RED! Hakuna anayekataa au anayepinga suala la ku-copy and paste... HAKUNA! Ninachosema ni kwamba, kama umevutiwa na filamu fulani na unataka kuichukua kama ilivyo kwa kiasi kikubwa basi ni LAZIMA ufanye makubaliano na wamiliki wa filamu/script husika! Usipofanya nao makubaliano lakini ukaitoa ili watu waamini kwamba hiyo ni original work, basi inakuwa ni wizi wa intellectual property! Haya mambo mie sijayasoma darasani bali nimewahi kufanya attempt ya kuuza script Hollywood kwahiyo nayafahamu from my experience! Ingawaje sijafanikiwa kuuza, but I hope one day nitauza tu! Kwahiyo, kabla sijafanya jaribio hilo, kabla sijafanya hilo jaribio, nilii-study international film industry inside out ikiwa ni pamoja na kuongea na wadau wenyewe... kwahiyo naongea kitu ambacho nafahamu ABC zake!
Hivyo basi, kwanza, hata kama fulani na fulani wa nchi fulani alikopi movie hii na ile kutoka nchi ABC, bado hicho hakiwezi kuwa kigezo cha mtu mwingine, katka mjadala huu JB, kukopi filamu ya mtu bila makubaliano! Lakini kubwa kuliko yote, una uhakika gani kwamba huyo ambae alikopi filamu fulani hakufanya makubaliano ya aina yoyote na mmiliki wa filamu husika?
Kama nilivyosema hapo awali... issue sio kufanana issue nikufanya makubaliano! Kwa mfano, ni kweli ukiangalia Iron Man, wanapita mule mule mwa Spiderman na ideas ni zile zile za Captain America and so on!
Hata hivyo, hapa nikukumbushe au kukujuza jambo moja kama ulikuwa hufahamu! Filamu na series nyingi Hollywood, pamoja na kutokana na novels, zingine zinatokana na comic books kama The Walking Dead! Iron Man nayo inatokana na comic book kutoka Marvel Comics! Na hata hizo Spider Man na Captain America nazo zinatokana na Marvel Comics! Sina uhakika na hiyo Thorn! Sasa basi, ukiangalia mlolongo huo, utaona kwamba Spiderman, Iron Man, Captain America, zote ni baba mmoja mama mmoja kwahiyo hakuna wizi uliofanyika! Hata X-Man na Iron Fist nazo zinatoka huko huko kwenye Marvel Comics! Kwahiyo hizo issue za hizo filamu huwezi kuzilinganisha na suala la JB kv zote hizo source yake ni sehemu moja... Marvel Comics! Na Marvel wana materials nyingi sana coz' hii kampuni ni ya muda mrefu, kwahiyo hata wewe kama una pesa, unaweza kuingia mkataba na Marvel Publications kwa Marvel Comics uipendayo na ukatengeneza movie/series!
Hapa ndipo lilipo tatizo! Yaani kwavile Bollywood nao wanakopi basi na sisi tuwe tunakopi tu unless tusikie Bollywood nao wamepata matatizo! Then what, matatizo yakianzia kwetu? Wakati unafikiria hayo, malizia na habari zifuatazo:
Kisha:Halafu na hii hapa:Kwahiyo ndo mnayoyataka hayo?
Hapa nakubaliana na wewe lakini kama idea ipo very unique wajitahidi kuomba ruhusa kwa wahusika!