Je, 2006 inajirudia Mashariki ya Kati?

Kosugi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
16,166
Reaction score
25,197
Israel imeandaa jeshi na imepeleka jeshi,vifaru na mifumo ya roketi mipakani na Lebanon.
Na jeshi tayari limeshasogea kilometa nyingi zaidi ya Shebah farms.
Ni kilometa chache tu zimebaki kwa IDF kuweza kuingia rasmi ndani ya mipaka ya Lebanon kusini.
Licha ya jeshi lililopelekwa bado kuna askari wa akiba wameitwa kujiunga ukanda huo wa Lebanon kusini.
Ikumbukwe 2006 yalijiri kama yanayojiri sasa.
Hadi kufikia sasa Hizbollah haijasema lolote wala kutoa tamko lolote,ukimya umetanda sana kuliko kawaida kwa Hizbollah.

Je,2006 inaenda kujirudia!!??
 
Israel inasema 2006 kuna makosa alifanya yaani alitumia nguvu ndogo na kasi kubwa kushambulia maeneo machache hezbollah alishambulia na kuvamia baadhi ya maeneo tu sasahivi atafanya uvamizi kama ule 1982 kwa hiyo msitegemee hezbolah wataweza kuipiga israel tena kama 2006 mpaka sasa israel anaendelea kuchoma silaha za hezbollah na kuuawa viongozi wao kwa kasi kubwa
 
Ya sasa ni tofauti, Israel imedhamiria kuliko siku nyingine yoyote, kilichofanyika Oktoba saba kimefanya Israel wamekuwa wanyama maana ni dhahiri hao Waislamu wameonyesha nia yao ni kuua kila Myahudi, kwa sasa hivyo Israel lazima ipige bila huruma.
 
Hezbollah labda kama sio hawa , ukiua mtu leo atateuliwa mwingine 😀 😀 😀 ...Hao jamaa hapana sio rahisi kuwavuruga kiuzalendo ....Hilo shambulio la pagers ndio lingewarudisha nyuma ila ,timing kumchinja kobe hapo .
 
Alichokifanya Gaza anataka akifanye Lebanon, hii ni kuipa Hezbollah pressure.

Kiuhalisia sidhani kama Israel ipo tayari kwa vita kamili na Hezbollah, watazunguka hapo mipakani wataindoka. Matarajio yao makubwa ni vita isimame.
Akipeleka jeshi lote ni hatari , kitu ambacho anafanya ni kuhakikisha hakuna passage ya Hezbollah kupokea silaha la sivyo ni hatari kwake.
 
Sidhani kama una uhakika na hichi ulicho kiandika.
 
Nikikumbuka mwaka 2006 Israel iliishambulia hizbullah zaidi ya wiki nzima tena kwanguvu kubwa mara 10 ya mashambulizi ya sasa bila majibu yeyote kutoka kwa hizbullah ninakuwa na akiba ya maneno.
Kiufupi ukimia wa hizbullah sio wa kawaida.
Hata hivi vifo vya makamanda wake usikute ni vya kufeki.
 
Akipeleka jeshi lote ni hatari , kitu ambacho anafanya ni kuhakikisha hakuna passage ya Hezbollah kupokea silaha la sivyo ni hatari kwake.
Hezbollah wana tunnels ambazo zipo complex na nyingi kuliko Hamas, Hamas wame survive Gaza kwenye tunnels.

Kuhusu silaha, Hezbollah wana shehena kubwa ya silaha.

Israel anaweka pressure kwa Hezbollah na kufarakanisha Hezbollah na serikali ya Lebanon, najua hadi hivi sasa kuna mvutano kati ya Hezbollah na serikali ya Lebanon.

Ndio maana umesikia viongozi wengi wameanza kupaza sauti hawataki kuona Lebanon ikiwa Gaza nyingine.

Israel inaelewa hilo ndio maana na yeye hapoi, kwenye ugomvi ukiwa unaamua watu utaona wana hasira sana kupambana hawataki kuamuliwa lakini ukiwaacha hao kila mmoja njia yake...

Serikali ya Lebanon haitokubali Hezbollah ianzishe vita kamili...

Netanyahu nae alisikika akiwaambia raia wa Lebanon "tuna vita na Hezbollah sio ninyi" hio ni kauli ya uchonganishi..

Maswali baina ya wanaharakati, viongozi wa Lebanon na wananchi itakuwa vita ikianza watakaoumia ni watoto wetu, wazazi, wanawake na wasio na hatia wakati huo Iran wanaishi kwa amani..
Wakati huo Hezbollah wapo kwenye tunnels, je hii vita inatufaa?

Kitu kitakacho surprise Israel ni kama Hezbollah watangaze vita kamili, nina uhakika Israel hajajipanga kwa hilo...

Nionavyo hapa hakuna vita...
Israel haitaki hii vita, ndio maana Hezbollah kawachokoza Israel muda mrefu wamekaa kimya...
 
Nendeni mkamzike Hassan Nasraillah tayar confirmed eliminated.

Hakuna vita mbaya ambayo Hizbullah wamepigana na Israel kama hii.
 
Nendeni mkamzike Hassan Nasraillah tayar confirmed eliminated.

Hakuna vita mbaya ambayo Hizbullah wamepigana na Israel kama hii.
 
 
Mtu asiyejua historia ya Israel anaweza kubeza.

Israeli in Deep History ya vita kuliko taifa lolote lile Duniani.

Mbinu za vita wamejifunza kizazi hadi kizazi Tangu wakati wanaingia Kanani.

Wayebusi kwa siku moja tu waliuliwa kwa mapanga( vita vya uso kwa uso)
Wapiganaji 28,000.

Bibilia inataja Jeshi la Israali likipambana na Wafilist, waamori, waamoni, wa Edom na wa Parizi wote kwa pamoja na linashinda.

Wakati huo Jeshi la Israeli likiwa na Wapiganaji zaidi ya Laki tatu. Hii ni miaka takribani 1500 Kabla Yesu Hajazaliwa. Leo hii Tanzania watu 61M hatuna idadi inayokaribian hata nusu ya hiyo idadi.

Mwaka 2010 nilifanikiwa kurika Israeli. Utaratibu wao kila Raia ni Mwanajeshi. Wako Smart kwa kila kitu.

Imagine kwa Tension iliyopo ya vita wanapataje Access ya kumuua Kamanda mkubwa?

Wao ktk vita Target zao ni Viongozi.

Wakati wanapigana na Wa Amaleki walimpiga Agagi( kamanda), wakati wa wafilisti walimpiga Goliati.

Kumbuka Jinsi Mwanausalam Ehudi alivyovamia Ikulu ya Mfalme wa Moabu yaani Eglon
Soma; wamuzi 3:12
 
Taifa la hovyo linajisifu kupigana a wanamgambo! Mbaya zaidi wanauawa wanawake na watoto, wanamgambo wameshindikana...
Wenzio akina nasra wapo peponi saiv wanaogelea kwenye mito yapombe we unabwabwaja
 
Wanaua kiongozi ila wa HAMAS tayari amekufa na mpya kashachukua madaraka mwendo ni ule, huyu aliyekuwa Nasrallah kumbuka alichukua kijiti baada ya wa mtangulizi wake kuuliwa ...Huyu ndio alimpiga ile 2006.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…