Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Nimeikuta hii humu jf kwenye mjadala fulani hebu jisomee mwenyewe!.
Kwa mujibu wa mtoa hoja hii, Mkuu Zomba wa JF,
Wake wa Abedi Amani Karume ni hawa wafuatao
Kama ni kweli, jee muasisi wetu huyu ana jumla ya watoto wangapi?. Vipi hali za hao watoto na vipi hali za hao wake?.
Lengo la kuyauliza haya kwasababu ndoa ni jambo la kheri, hivyo hakuna ubaya wowote kuijua status ya familia nzima ya Shujaa huyu, kiongozi wa yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na Muasisi wa Muungano wetu Adhimu, ili tunaposherehekea Diamond Jubilei (50-years) ya Mapinduzi na Muungano, pia tuwaenzi watu waliohusika na maisha ya Shujaa na muasisi wetu huyu!.
NB. Kuna kitu kinaitwa "the right to privacy" ambapo kila mtu anayo haki ya faragha ya mambo yake binafsi, na mtu yoyote haruhusiwi kuingilia uhuru huo wa hifadhi ya mambo yake ya faragha na kuyaleta public. Haki hii ya faragha, inakuwa imeondolewa kwa watu ambao ni "public figures" ambao wamekuwa wakilipwa misahara kwa fedha za walipa kodi!, yaani wanalipwa kwa fedha za "taxpayers money", hivyo walipa kodi hao, "The Public has the right to know the publi and private conduct" of their leaders! kwa sababu hayo ni matumizi ya kodi zao!.
Pasco.
Nimeikuta hii humu jf kwenye mjadala fulani hebu jisomee mwenyewe!.
Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini.
Isitoshe, si Fatma tu na Ashura ambao ni wakizazi cha "mabwana", pia kuna wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.
Unawajua khabari zao hawa mabibi Nasra, Helemu na Fadya?
Pasco Zanzibar huijui. Waachie Wazanzibari wenyewe
"Sisi mambo twayajua" - Khadija Kopa.
nna uhakika somo umelipata.
Kwa mujibu wa mtoa hoja hii, Mkuu Zomba wa JF,
Wake wa Abedi Amani Karume ni hawa wafuatao
- Bibi Pili binti Ahmed Ambari
- Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara.
- Mke wa tatu ni Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944
- Bibi Nasra, -Amebahatika naye mtoto mmoja wa kike
- Bibi Helemu-amebahatika nae mtoto mmoja wa kike
- Bibi Fadya-amebahatika naye mtoto mmoja wa kike
Nawauliza wale wajuzi wa siasa za Zanzibar, jee haya ni ya kweli ua anasingiziwa?!.Angalau leo kuna mtu kalithibitisha hili kama alivyoeleza hapa
Mkuu Binti Mkongwe, asante kwa hii taarifa yako, ila naomba uilinganishe na hii taarifa ya Mkuu Tigo Pesa
Hivyo nikijumlisha lie original list na hii ya kwako kwa kutumia elimination method, nitapata jibu hili
Kitu ambacho nimenote, Karume mwenyewe aliitwa Abedi, Baba yake aliitwa Amani, Mama yake Karume aliitwa Amina, mmoja wa wakeze aliitwa Ashura, mmoja wa wakweze ni Ahmed Ambari, watoto wake Asha (rip), Amani, Ali, Ahsa, Ahadi, Asha, what a coincidence?!.
- Mke wa kwanza Bibi Pili binti Ahmed Ambari, (hakuna details za ethnicity wala watoto)
- Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. (Hakuna details za ethnicity wala watoto)
- Mke wa tatu ni Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944-Amani na Ali Karume
- Moza Nassor (marehemu) Mwarabu-kutoka Ole Pemba (muarabu na hakubahatika kupata mtoto)
- Bibi Nasra, Mmatumbi- alishiriki shindano la Bibi Bomba Clouds. Amejitambulisha kama mke mkubwa Ana mtoto
- Nasreen -Mhindi-Amebahatika naye mtoto mmoja wa kike-Ahsa Karume
- Bibi Helemu-Mwarabu-amebahatika nae mtoto mmoja wa kike-Ahadi Karume.
- Bibi Fadya-Mwarabu-amebahatika naye mtoto mmoja wa kike Asha Karume.
Wanahistoria wa Zanzibar, hizi details haziko consistence, yupi sahihi, Binti Mkongwe au lile andishi, au wote wako sahihi hivyo wake ni 8?!.