Je, Abedi Amani Karume alikuwa na Wake 6? Ana Watoto Wangapi?

Je, Abedi Amani Karume alikuwa na Wake 6? Ana Watoto Wangapi?

Maadahii Nimeipenda Ilasijaona Mtualiesema Kalume Alikuwa Nawatoto Wangapi.Watalamu Tuambieni
 
Sijapata jibu bado. Nimesoma mwanzo mpaka mwisho Ritz kasema wakeze karume walikuwa watatu na watoto wake ni wangapi wa huyo muasisi wa muungano.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Nimeikuta hii humu jf kwenye mjadala fulani hebu jisomee mwenyewe!.

Kwa mujibu wa mtoa hoja hii, Mkuu Zomba wa JF,

Wake wa Abedi Amani Karume ni hawa wafuatao

  1. Bibi Pili binti Ahmed Ambari
  2. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara.
  3. Mke wa tatu ni Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944
  4. Bibi Nasra, -Amebahatika naye mtoto mmoja wa kike
  5. Bibi Helemu-amebahatika nae mtoto mmoja wa kike
  6. Bibi Fadya-amebahatika naye mtoto mmoja wa kike


    Pasco.

Angalau leo kuna mtu kalithibitisha hili kama alivyoeleza hapa
Kuhusu wake zake kwa ninaowakumbuka mimi ni kama wafuatao:
1. Fatma Karume mama yao Amani na Ali
2. Moza Nassor (marehemu) kutoka Ole Pemba (muarabu na hakubahatika kupata mtoto)
3. Nasreen (muhindi ithnasheri) wa Unguja mama yake Ahsa Karume
4. Fadya (muarabu) wa Unguja mama yake Asha Karume
5. Helemu (muarabu) wa Wete Pemba mama yake Ahadi Karume.

Inasemekana huyu first lady alikuwa tayari amepewa talaka ila hakuna uthibitisho.
Mkuu Binti Mkongwe, asante kwa hii taarifa yako, ila naomba uilinganishe na hii taarifa ya Mkuu Tigo Pesa
Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini.

Bibi Fatma Gulamhussein Ismail alizaliwa Bumbwini mwaka 1929 akiwa ni mtoto wa Bwana Gulamhussein Ismail na Bibi Mwanasha Mbwana Ramadhani. Wazazi wa Bibi Fatma Karume ni wazaliwa wa Bumbwini. Bi Fatma Karume alipata elimu ya msingi katika skuli ya Bumbwini na kuolewa mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo hayo. Mara tu baada ya kufunga ndoa, Bibi Fatma Karume na Bwana Abeid Amani Karume walihamia mtaa wa Kisimamajongoo nyumba Nambari 18/22 mjini Unguja kwa Sheikh Karume. Nyumba nyengine mbili za Bwana Karume zilikuwa Gongoni na Michenzani.

Bi.Fatuma Karume alijifungua mtoto wa kwanza wa kike aliyeitwa Asha katika mwaka 1946, lakini mtoto huyo alifariki siku ya pili yake. Mtoto wa pili wa hayati Karume ni Amani Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 1 Novemba, 1948. Mtoto wake wa tatu ni Ali Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 24 Mei, 1950.

Mama yake mzazi Abeid Amani Karume, Bibi Amina binti Kadudu alifariki dunia 1963 na kuzikwa katika makaburi ya Michenzani. Wake wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.

Hivyo nikijumlisha lie original list na hii ya kwako kwa kutumia elimination method, nitapata jibu hili
  1. Mke wa kwanza Bibi Pili binti Ahmed Ambari, (hakuna details za ethnicity wala watoto)
  2. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. (Hakuna details za ethnicity wala watoto)
  3. Mke wa tatu ni Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944-Amani na Ali Karume
  4. Moza Nassor (marehemu) Mwarabu-kutoka Ole Pemba (muarabu na hakubahatika kupata mtoto)
  5. Bibi Nasra, Mmatumbi- alishiriki shindano la Bibi Bomba Clouds. Amejitambulisha kama mke mkubwa Ana mtoto
  6. Nasreen -Mhindi-Amebahatika naye mtoto mmoja wa kike-Ahsa Karume
  7. Bibi Helemu-Mwarabu-amebahatika nae mtoto mmoja wa kike-Ahadi Karume.
  8. Bibi Fadya-Mwarabu-amebahatika naye mtoto mmoja wa kike Asha Karume.
Kitu ambacho nimenote, Karume mwenyewe aliitwa Abedi, Baba yake aliitwa Amani, Mama yake Karume aliitwa Amina, mmoja wa wakeze aliitwa Ashura, mmoja wa wakweze ni Ahmed Ambari, watoto wake Asha (rip), Amani, Ali, Ahsa, Ahadi, Asha, what a coincidence?!.

Wanahistoria wa Zanzibar, hizi details haziko consistence, yupi sahihi, Binti Mkongwe au lile andishi, au wote wako sahihi hivyo wake ni 8?!.

Pasco.
 
Angalau leo kuna mtu kalithibitisha hili kama alivyoeleza hapa

Mkuu Binti Mkongwe, asante kwa hii taarifa yako, ila naomba uilinganishe na hii taarifa ya Mkuu Tigo Pesa


Hivyo nikijumlisha lie original list na hii ya kwako kwa kutumia elimination method, nitapata jibu hili



  1. [*=left]Mke wa kwanza Bibi Pili binti Ahmed Ambari, (hakuna details za ethnicity wala watoto)
    [*=left]Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. (Hakuna details za ethnicity wala watoto)
    [*=left]Mke wa tatu ni Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944-Amani na Ali Karume
    [*=left]Moza Nassor (marehemu) Mwarabu-kutoka Ole Pemba (muarabu na hakubahatika kupata mtoto)
    [*=left]Bibi Nasra, Mmatumbi- alishiriki shindano la Bibi Bomba Clouds. Amejitambulisha kama mke mkubwa Ana mtoto
    [*=left]Nasreen -Mhindi-Amebahatika naye mtoto mmoja wa kike-Ahsa Karume
    [*=left]Bibi Helemu-Mwarabu-amebahatika nae mtoto mmoja wa kike-Ahadi Karume.
    [*=left]Bibi Fadya-Mwarabu-amebahatika naye mtoto mmoja wa kike Asha Karume.
Kitu ambacho nimenote, Karume mwenyewe aliitwa Abedi, Baba yake aliitwa Amani, Mama yake Karume aliitwa Amina, mmoja wa wakeze aliitwa Ashura, mmoja wa wakweze ni Ahmed Ambari, watoto wake Asha (rip), Amani, Ali, Ahsa, Ahadi, Asha, what a coincidence?!.

Wanahistoria wa Zanzibar, hizi details haziko consistence, yupi sahihi, Binti Mkongwe au lile andishi, au wote wako sahihi hivyo wake ni 8?!.

Pasco.​

Mimi nilisema ninaowakumbuka na ni hao wa baada ya mapinduzi. Hao wa kabla niliwahi kusikia tu lakini sikuwa nafahamu.
 
Yule binti yake ambaye ni wakili anaitwa nani?
 
Kule mambo yamemshinda kaja kutafuta msaada huku. Lakini watu wengi wa JF wameshamjua alivyo mnafik, hata hao ambao anategemea watampa msaada kwa huu uongo wake, wanamponda tu.

Eti mtu yuko kwenye fani ya habari anaenda kubadili post yangu kwa kuwa nimemshinda kwa hoja.
Duh! Hatari
 
Back
Top Bottom