"Planet X iliaminika ipo kwasababu ya uvutano na planet pluto baadaye ikajakuwa proved wrong baada ya Hubble Telescope kugundua kwamba hiyo planet X haipo".-- nimekunukuu.
---Tunajua kuna nguvu za uvutano kati ya Jua na sayari na nguvu hiyo ndiyo inayozifanya sayari ziendelee kulizunguka jua, je ni nani aliyeanzisha huo mzunguko?? (recall the mechanism to keep an artificial satellite in the orbit).
--Ni nani aliyeanzisha nuclear reaction (fussion reaction) ya Hydrogen kuwa Helium ili kuzalisha joto, mwanga kwenye jua??, isitoshe ni nani aliweka hiyo gas ya Hydrogen huko??, (recall thermonuclear bomb).
--- Ni nani aliyepanga illi wewe uzaliwe na hao wazazi wako na uwe na jinsia uliyonayo?? (Refer watu wanaojibadilisha jinsia zao kwa operation).
Ni hadi pale utakaponipa majibu ya maswali hayo kwa ushahidi jinsi Hubble telescope ilivyotoa majibu ya kutokuwepo kwa Planet X, nami nitaamini hakuna the Supreme conscious disciplined intelligent being anayesimamia shughuli zote hizo na zingine nyingi,, The almighty God.
Maswali yako yote ni nani? Ni nani??
Yani umeshaasume kuwa lazima awepo 'Fulani'.
Ungeanza kwanza kuthibitisha hiyo assumption yako kuwa lazima awepo Fulani ili hivyo vitu vitokee...na haviwezi kutokea vyenyewe bila Fulani.
Cha ajabu nikikuuliza Huyo 'fulani' katokea wapi, utaishia kusema Hana chanzo.
Sasa kama unaamini Mungu Hana chanzo, unashindwaje kuamini hydrogen,gravity havina chanzo??
Ingawaje majibu ya maswali yako yote kwenye sayansi yapo.
Maelezo ni marefu na yanaboa, ila kifupi hivyo vyote vilitokea from nothing...
Hata sasahivi kwenye empty space unayoina unayodhani Haina kitu, Kuna vitu vinaumbika na kupotea(quantum fluctuations)...Sema hivyo vitu ni vidogo sana na Vinakaa Kwa muda mchache sana (10^–23seconds) kiasi kwamba huwezi kuviona...ila Kwa mashine vinaonekana...na vimeshathibitishwa.
Kuna particles zinatokea from nothing na kupotea kwasababu Huwa zinatokea in pair, Yani particle na anti-particle yake, Hivi vikitokea vinaungana na kurudi kuwa nothing.
Yani ni sawa ulete 1 na -1 uviunganishe, lazima utapata 0
hata sasa, Kuna particles zinatokea from nothing na kurudi back into nothing.
Sasa kama hivi vitu vinaweza kutokea from nothing, ulimwengu unashindwaje?
Ulimwengu wenyewe ulitokea from nothing, Hizi Protons,Electrons,Neutrons ambazo ndio zinatengeneza kila kitu zilikuwa formed kupitia Hizi Quantum fluctuations...Kilichotokea TU kipindi cha big bang ni kwamba Hizi particle hazikubalance (maana zikibalance zinapotea, particle vs anti-particle)
Kwahyo particle zilipokuwa nyingi tukaanza kupata gluons zilizotengeneza electrons na protons zilizoleta Hydrogen na element zote.
Gravity ni matokeo ya uwepo wa hizi particles,maana zina property ya kubend space...Na gravity ni space iliyobend...Ukielewa hili utaelewa kuhusu hizo Satellite,Jua, Hydrogen na maswali yako yote.
Kwa kifupi nomeandika Kwa kifupi saaana...Maana SoMo ni pana.
Kasome Kuhusu Quantum fluctuations na na quantum field theory....Ukishakuwa na Basics kidogo tunaweza kuendelea kuelimishana.
Hapa chini ni picha ya empty space ila inaonesha hizo particles zonavyokuwa formed from nothing na kupotea back into nothing