Je, AI itatusaidia au itachukua nafasi zetu?

Je, AI itatusaidia au itachukua nafasi zetu?

Chosen Rich

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2019
Posts
1,565
Reaction score
1,118
Humu mpo magenius, Watu mliojawa maarifa na hekima, Wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kupambanua mambo mbali mbalimbali

Note: Majibu na hoja yazingatie mantiki
 
Nafasi gani itawachukulia AI Tanzania? boda boda au?
80% ya watanzagiza hawana ajira rasmi wanafanya kazi kama kulima kwa ajili tu ya chakula, kuuza mboga mboga, kuendesha boda boda, dala dala, fremu za maduka, uimamu, kuuza baa, etc sasa ni kazi gani ai itakazochukuwa labda ktk kwa watanzagiza?
 
Kwa kiasi cha kutosha ni faida chanya ,ila kwa sasa.
Huko mbele kidogo tujishike aisee, kila leo inaboreshwa na kujiboresha.

Ila nafasi zitakazo chukuliwa haswa huku kwetu miaka 50 mbele huko, na ni za ofisin huko.
 
AI itabeba nafasi nyingi sana huko mbele ya safari madaktari, sijui madereva etc wengi watakosa ajira, kuna haja ya kujiwekeza uwe na pesa ya kutosha itakusaidia kwenda na dunia inavyotaka.
Leo wewe dereva kwa gari ya mtu mwenyewe akinunua gari inayojiendesha yenyewe wewe huna ajira.

Daktari wa operation, ikifanikiwa teknolojia ya kifaa kinachofanya operation bila usimamizi wa mwanadamu kifuatacho ni huna ajira. Mgonjwa anaenda kwenye camera anazungumza dalili zake, sampo inachukuliwa hapo hapo, majibu hapo hapo na tiba inaanza.. hapa daktari, mtu wa maabara wote hawana ajira.

Unaipa AI wazo inakuchorea ramani nzuri na kamilifu.. wachora ramani hapa wakatafute mchezo wa kufanya. Ai ina design logo vizuri hapa kifuatacho ni nini?
Unaipa wazo, yenyewe inandika mistari na biti inakutengenezea, Producer hapa atafute cha kufanya.

Hapo hujakutana na kesi, kisha unaiambia AI hali ilivyo yenyewe inakupa maelekezo, inakupa muongozo pita humu, pita humu wanasheria wajiandae kutafutavkazi nyingine.
Wahasibu nao wajiandae.

Na sekta nyingine kibao.​
 
Dunia inavyoenda akili ya binadamu itahitajika ifunguke zaidi!, Dunia inayokuja haitaki lelemama sio dunia yakujikomaza mikono bali ukomavu wa akili utahitajika!, by the way AI itahitaji ilindwe alasivyo muda si muda itaanza kukutana na kila aina ya attacks!.

Hii inanipa picha ni aidha katika kulinda utu wa mtu AI itatungiwa sheria ili baadhi ya vitu fulani fulani isiweze kufanya!, ikishindikana hivyo basi tunaenda kwenye standard yani kila binadamu atakuwa na maisha ambayo yataratibiwa kuwa na standard fulani na hii itatulazimu tuishi chini ya sheria kadhaa ili kuweza ku maintain hiyo standard!.
 
Back
Top Bottom