fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,073
USIPOTOSHE HUNA HAKI HIYO. Utakumbuka kuna mwaka hata rais JK hakualikwa kuhudhuria mei mosi na alitii.
RC ni Raia kama ilivyo kwa wengine wote, huna ruksa kwenda sehemu yoyote ambapo kwa kufanya hivyo unahatarisha amani na kuingilia uhuru wa watu kukusanyika. SO hayuko juu ya hilo.
Sherehe hujipachiki, UNAALIKWA. BILA MWALIKO huendi na kwenda kwako tafasiri yake ni kuvunja amani kwa kuleta fujo
Nawasilisha
RC ni Raia kama ilivyo kwa wengine wote, huna ruksa kwenda sehemu yoyote ambapo kwa kufanya hivyo unahatarisha amani na kuingilia uhuru wa watu kukusanyika. SO hayuko juu ya hilo.
Sherehe hujipachiki, UNAALIKWA. BILA MWALIKO huendi na kwenda kwako tafasiri yake ni kuvunja amani kwa kuleta fujo
Nawasilisha
Jana tarehe 08/03/2020 wanawake wote duniani waliadhimisha kumbukizi kwa ajili Yao ikiwa na lengo la kupaza sauti kupatiwa USAWA na kupinga ukandamizaji wa kijinsia!!
Katika maadhimisho hayo wanawake kwa vikundi ama kwa jumuiya zao walijumuika pamoja kujiwekea mikakati mbalimbali kijamii na kisiasa.
Lakini kituko zaidi kilitokea wakati Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Christian Makonda alipoamua kwenda ili kuwasapoti wanawake wa Chama Cha demokrasia na maendeleo ( Chadema) .
Kilichotokea kulingana na clip zinazogaa katika mitandao ya kijamii Ni kuzuiliwa kuingia huku ikisemekana Mwenyekiti wa Bawacha Taifa Halima James Mdee kuamuru Jambo Hilo.
Well, kwa jicho la kawaida inaonekana Ni sawa kwa kitendo hicho cha kufedhesha alichofanyiwa RC Makonda, Lakini Ni Cha kijinga kufanywa na Baraza Hilo la wanawake Tena ambao wengi wao wanajua protocol za kiuongozi ya kwamba RC anaweza kuhudhuria hafla yeyote ya kitaifa inayofanyika mkoani kwake isipokuwa shughuli binafsi.
Baraza la wanawake Chadema linaongozwa kwa sheria za Nchi na Lina usajili, sio Ngo's Ni taasisi halali inayotambulika na Serikali ikiwa chini ya udhamini wa CHADEMA.
Rai yangu kwao Kuna wakati wa kushirikiana na Serikali ili kufikisha maoni Yao kwa urahisi bila kushupaza shingo, Uzuri waalikwa wao walikuwa Ni moja ya watu waelewa na wanaharakati Kama Fatuma Karume wangeweza kufikisha kero za wanawake kwa RC na yeye akafikisha mahali husika.
Halima Mdee namuona Kama kiongozi mshamba Sana na hii Ni Mara ya pili kufanya vitu vya ajabu Ana chuki, fitina..
Kwa kufanya vile moja kwa moja alimjengea picha RC Makonda kwamba ni moja ya watu wanaokandamiza haki za wanawake.
Kitendo cha hovyo kufanywa na watu waungwana ilitakiwa wamruhusu ili kumsikiliza Halima Mdee asijifanye Bibi Titi Mohamed Hana Kariba hiyo na Wala hatokaa amfikie...
Katika post yangu ya juzi nilivyomuaga Halima James Mdee katika nafasi ya ubunge watu walinishambulia na hoja zao mfu haya semeni na hili ni Sahihi?