Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Je, asili ya Washirazi ni Persia?

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Posts
5,486
Reaction score
3,473
Zanzibar kuna wenyeji wengi hasa Kaskazini Unguja, Tanga, Pangani, Mombasa nk. hujinasibu kuwa wao ni Washirazi. Kuna wakati kule Mombasa walikuwa wanaitwa wageni na wengi ilibidi wajichanganye hivyo wengine wakajiita Wadigo ili mradi waweze kuishi kwa amani.

Kwa ZanzibaKwumuhimu wao unajionyesha hata kwenye siasa kwani ninasikia walikuwa na chama kiitwacho Shirazi Party ambacho baadaye kiliungana na Afro na kuitiwa Afro Shirazi Party na mwishowe kuwa sehemu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hawa ni watu walitokea wapi? na asili yao hasa ni ipi? Ningependa wana historia wachangie kwenye hili ili lieleweke vizuri.

Katika kudadisi kwangu kwanza Washirazi hawapendi kujinasibu na Waarabu na ndiyo maana ilikuwa rahisi kwao kushirikiana na African Association kuliko Hizbu.

Nilichokipata Mimi [na ambacho ningependa wajuzi zaidi wachangie] ni kwamba asili ya Washirazi ni Persia ya zamani na inasemekana kuwa katika kile kipindi cha utata wa Ukhalifa baada ya kufariki Mtume Muhammad (SAW), ambapo baadhi waumini waligawanyika wakati wengine walitaka Sayyed na Ally apewe nafasi hiyo na wengine wakataka waraka wa mtume ufuatwe.

Hali hiii ilileta farka na ilienea hadi persia ambapo Sayyed na Ally alikubalika sana [Je, hiki ndicho chanzo cha Shiraz? [wajuzi tusaidieni].

Kule Persia kwa wale wachache ambao walitaka utashi wa mtume utumike katika uchaguzi wa ukalifa wakawa persecuted na kulazimika baadhi kukimbia. Wengine walikuja huku Pwani ya Afrika ya Mashariki. Hawa jamaa hawakuwa traders bali walikuwa craftsmen wakitengeneza milango, viti majahazi na walipokuja huku hiyo ilikuwa kazi yao kubwa na hivyo kuthaminiwa sana na falme za Pwani ambapo walihusika sana na shughuli hiyo [Milango ya Zanzibar, Madirisha] ingawa wengine wakaingia katika uvuvi na biashara.

Ingefaa sana kama wajuvi wa historia wangeongeza nyama kwenye historia ya kundi hili historia ya jamii hii ya Kizanzibari likae sawa na vile vizazi vya sasa na vijavyo vifahamu asili yao.

NAWASILISHA
 
Persia = Shirazi kwa kiswahili
Acha kuhororoja hapa
 
Kwa uchache ufahamu wangu upon hivyo kwamba washirazi asili yao Persia mbayo in maeneo ya Irani ya leo.
 
Afghanistan, Pakistan, na Iran
Iran ilikuwa inaitwa persia. Na persia ya zamani ilikuwa inatawala eneo kubwa kuliko ilivyo hivi sasa.

Inaelekea hawa washirazi, hasa asili yao ni Shiraz ambayo ni makao makuu ya jimbo la Fars.

Mji huu ndiyo ulikuwa mji mkuu wa persia hadi mwaka kuanzia 2000BC [mabaki ya historia ya kale]hadi mwaka 1800.

Mji huu ulikuwa ni mji wa washairi,uandishi,utaalam mkubwa wa bustani[kurembesha] mazulia[sasa huitwa persian carpets],wajenzi wa kila fani, biashara n.k.

Nadhani ndiyo maana kila mahala walipoamua kuishi[nje ya persia] walikuwa wanaheshimiwa na kuthaminiwa. Ukiangalia yale majengo ya kale kule kilwa na mafia yanashabihiana sana na aina ya wajenzi walivyokuwa wanajenga persia miaka hiyo. Waarabu ambao sasa wanasifiwa kwa majengo ya ukanda huu ninadhani sifa hii wanaipata kwa sababu tu majengo haya yalijengwa wakati wa himaya yao.
 
KUHOROROJA!!!!! tafadhalini tujitahidi kutumia kiswahili sanifu kwenye uchangiaji wetu humu maana kuna maneno mengine yanayotumika humu jamvini yanatia ukakasi
Kuhororoja kuropoka.

Shirazi ni Maeneo ya mAshariki ya kati kwa sasa Iran.

Mtu akisema yeye mshirazi kwa maana hiyo, lakini wakaazi wa maeneo ya visiwa ni Waafro shirazi = muunganiko Washirazi na Waafrika waliokuwa wakiishi maeneo hayo. Kwa maana ni Mulato
 
Je, wale wasukuma waliochanganyika na wahadimu kule unguja utawaitaje?
 
Jee wale wasukuma waliochanganyika na wahadimu kule unguja utawaitaje?
Ni wazanzibari lakini sio Waafro shirazi, kizuri ni kuwa tayari umeshawatambua kama wasukuma.
Zanzibar kuna:
Wasukuma
Wandengereko
Wayao
Wazaramo
Wagunya
Wamanyema
Wanyamwezi
Wahadimu
Mamakonde
Ambao hao asili yao bado imebaki kama ilivyo kwa vile hawajanganyika (kuzaliana na washirazi) na kuna wengine kama hao ambao asili yao imechanganyikana na washirazi pamoja na wahadimu. Waliochanganyikana na washirazi baadhi kizazi kimekuwa cha kishirazi, baadhi waliochanganyikana na wahadimu kizazi kimekuwa cha wahadimu na wengine wameendelea kubaki na makabila yao kizazi kwa vizazi hadi sasa.
 
Ni wazanzibari lakini sio Waafro shirazi
Uzanzibari ni utaifa kama ulivyo wewe kutambulika kama mtanzania. Lakini utaifa hauhuwishi asili ya mtu.

Ndiyo maana hata leo wale wasukuma waliohamia pemba na unguja miaka hiyo kabla ya mapinduzi na baada ya kuchanganyika kwenye kuoana bado wajukuu zao wanajiita wasukuma, wamakonde nk.
 
Kutokana na hakukuwa na mchanganyiko baina yao na washirazi.
 
Ni wazanzibari lakini sio Waafro shirazi, kizuri ni kuwa tayari umeshawatambua kama wasukuma.
Zanzibar kuna:
Wasukuma
Wandengereko
Wayao
Wazaramo
Wagunya
Wamanyema
Wanyamwezi
Wahadimu
Mamakonde
Ambao hao asili yao bado imebaki kama ilivyo kwa vile hawajanganyika (kuzaliana na washirazi) na kuna wengine kama hao ambao asili yao imechanganyikana na washirazi pamoja na wahadimu. Waliochanganyikana na washirazi baadhi kizazi kimekuwa cha kishirazi, baadhi waliochanganyikana na wahadimu kizazi kimekuwa cha wahadimu na wengine wameendelea kubaki na makabila yao kizazi kwa vizazi hadi sasa.
Hebu nenda kaskazini ya unguza sehemu za bumbwini bado utawakuta. Sheikh Thabit Kombo alikuwa ni mshiraza[Mwanawe sasa ni waziri hebu muulizeni kabila lake-atawaambia kuwa yeye ana asili ya Kisharazi[kwa baba yake] Vile vile unavyosema wagunya hio siyo kabila bali ni sehemu [Lamu] na huko kuna makabila vile vile.

Hebu tembelea mwambao wa pwani wote hasa kuanzia pangani hadi somalia utakutana na washirazi. Kama huamini basi hebu fanya utafiti[hicho ndiyo chanzo cha mimi kuandika thread hii] Nisingependa kuyazungumzia haya kiwepesi kama unafanya wewe.

Niliandika humu nikitambuwa aina wa watu wanaoingia jamvini na nikatarajia maelezo ambayo ni yakinifu. TAFADHALI USIUHARIBU UZI HUU KAMA HUNA CHA KUCHANGIA NI BORA USOME HALAFU TUWAWACHIE WATAALAM[WAPO WENGI HUMU] WATUSAIDIE NA NAOMBA TUSIINGIZE SIASA KWENYE HILI.
 
Kutokana na hakukuwa na mchanganyiko baina yao na washirazi
Ila pia wapo wanyamwezi waliochanganyika kuoana na kuzaa na washirazi ambapo kizazi chao wanajiita waafro shirazi.
Hapa ngoja nikueleweshe kidogo.

Mzanzibar akija bara imeshazoeleka kuonekana kama hana kabila, lakini ukweli ni kuwa wengi wa wazanzibari ni wahadimu na wengine ni waafro shirazi kwa maana ni mulato (Afrika na shirazi) na wengine makabila yao yamestik kuwa vile vile kwakuwa hawakuwa na muingiliano wa mahusiano ya moja kwa moja na washirazi.

Moja ya makabila hayo ni yale ambayo walikuwa wakichukuliwa bara na kupelekwa visiwani kama watumwa enzi za biashara hiyo (Kamsome Tip-Tippu) na wengine ni wale ambao walitoroka bara kuepuka kuchukuliwa watumwa na kukimbilia visiwani kwa wakati huo.

Washirazi waizaa sana na wahadimu kuliko haya makabila yaliopelekwa visiwani enzi za utumwa na ndio maana wengi wa waafro shirazi sio kutoka katika haya makabila mengine.
 
Shekhe, Mzee Thabit Kombo binafsi ni babu yangu.

Then wagunya ni kabila kama makabila mengine.

Wapo waliochanganyika na washirazi na wapo waliostik hadi leo hii hawakuzaliana na washirazi.
 
Kwa hivi sasa ukimkuta mtu ambae anajiita mshirazi tu basi elewa kuwa huyo baba au babu yake kwa upande wa baba alikuwa ni mshirazi safi na sio vingine.
 
Ila pia wapo wanyamwezi waliochanganyika kuoana na kuzaa na washirazi ambapo kizazi chao wanajiita waafro shirazi.
Hapa ngoja nikueleweshe kidogo.

Mzanzibar akija bara imeshazoeleka kuonekana kama hana kabila, lakini ukweli ni kuwa wengi wa wazanzibari ni wahadimu na wengine ni waafro shirazi kwa maana ni mulato (Afrika na shirazi) na wengine makabila yao yamestik kuwa vile vile kwakuwa hawakuwa na muingiliano wa mahusiano ya moja kwa moja na washirazi.

Moja ya makabila hayo ni yale ambayo walikuwa wakichukuliwa bara na kupelekwa visiwani kama watumwa enzi za biashara hiyo (Kamsome Tip-Tippu) na wengine ni wale ambao walitoroka bara kuepuka kuchukuliwa watumwa na kukimbilia visiwani kwa wakati huo.

Washirazi waizaa sana na wahadimu kuliko haya makabila yaliopelekwa visiwani enzi za utumwa na ndio maana wengi wa waafro shirazi sio kutoka katika haya makabila mengine.
Kwa taarifa yao Asili ya Neno Afro Shirazi ni muunganiko wa vyama 2 vya siasa huko visiwani navyo ni AFRICAN PARTY NA SHIRAZ PARTY. Viongozi wa vyama hivyo waliona ni busara kuunganisha nguvu pamoja na wananchi kwa kuungana pamoja na chama cha AFRO SHIRAZ PARTY kiliundwa chama hiki ndiyo kilichosimamia mapinduzi ya znz na baadaye kuungana na TANU ambapo sasa ni Chama Cha Mapinduzi.
 
Washirazi walipotoka zao maeneeo ya kwao (hasahsa Iran, hadhramut Yemen) walipitia na kuacha vizazi vyao maeneo ya pwani ya Afrika mashariki kuanzia Kenya, bagamoyo na visiwa vya Zanzibar mpaka maeneo ya Lindi na kisiwa cha Mafia.
 
Kwa taarifa yao Asili ya Neno Afro Shirazi ni muunganiko wa vyama 2 vya siasa huko visiwani navyo ni AFRICAN PARTY NA SHIRAZ PARTY. Viongozi wa vyama hivyo waliona ni busara kuunganisha nguvu pamoja na wananchi kwa kuungana pamoja na chama cha AFRO SHIRAZ PARTY kiliundwa chama hiki ndiyo kilichosimamia mapinduzi ya znz na baadaye kuungana na TANU ambapo sasa ni Chama Cha Mapinduzi
Mbali na hivyo kizazi kilichochanganya baina ya muafrika na washirazi ndio afro shirazi pia (mulato)
 
Back
Top Bottom