Je, baadhi ya kazi zinafanya mtu apoteze utu?

PHILE1879

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
645
Reaction score
482
Niko safarini kutoka kanda ya kati kuelekea Geita.
Nafika eneo fulani mkoani singida. Wale wenye sare nyeupe wananyoosha mkona kuashiria nisimamishe gari.

Yeye: Nipe leseni yako
Mimi: Hii hapa
Yeye: Una deni la faini
Mimi: Ndiyo
Yeye: Lipia
Mimi: Bado nina safari ndefu.Nina akiba ya kununua petroli .Nitalipa nikifika.

Yeye: Hapana . Lipa sasa hivi.
Mimi: Sina pesa.
Yeye: Usipolipa hutoki hapa.

Mimi: Nikaingia app ya GEPG.
Nikamwonyesha. App inasema pay before May 29th 2024.
Mimi: Deadline haijafika. Nitalipa kabla ya tarehe hiyo.

Yeye: Hapana. Lipa sasa hivi ama hutoki hapa.

Tukazozana sana bila suluhu kwa nusu saa hivi. Nikaona mimi ndiye napoteza. Maana bado nina safari ya kilometers 400 hivi.

Naamua kulipa na kuondoka. Nimeudhika sana.
 
Kanuni ya kwanza uwapo barabarani unapokutana na askari daima.
Kuwa muungwana hata kwa kuigiza tu,ili maisha yaende,ubaya wa polisi ni kwamba, ana nafasi ya kukusumbua,kukupotezea muda na kama haitoshi ana nafasi ya kukusababishia kesi au hasara ukalala ndani.

Pole sana mkuu,ila naamini mlianza kwa namna tofauti.
 
This is bullshit
 
Hapa unatupanga.
Faini ya kawaida huwa ni wiki ikipita inapanda mpaka kiasi fulani nimesahau ambacho utakapokamatwa unatakiwa ulipe hapo hapo, kama ni hii askari alikuwa sahihi.
Parking fee yenyewe inasema ulipe tarehe fulani na polisi huwa hawakukamati kwa parking fee, wapo wenyewe wa parking ambao wanakamata wenye madeni makubwa kama 50,000
 
Niko safarini kutoka kanda ya kati kuelekea Geita.
Nafika eneo fulani mkoani singida. Wale wenye sare nyeupe wananyoosha mkona kuashiria nisimamishe gari.

Yeye: Nipe leseni yako
Mimi: Hii hapa
Yeye: Una deni la faini
Mimi: Ndiyo
Yeye: Lipia
Mimi: Bado nina safari ndefu.Nina akiba ya kununua petroli .Nitalipa nikifika.

Yeye: Hapana . Lipa sasa hivi.
Mimi: Sina pesa.
Yeye: Usipolipa hutoki hapa.

Mimi: Nikaingia app ya GEPG.
Nikamwonyesha. App inasema pay before May 29th 2024.
Mimi: Deadline haijafika. Nitalipa kabla ya tarehe hiyo.

Yeye: Hapana. Lipa sasa hivi ama hutoki hapa.

Tukazozana sana bila suluhu kwa nusu saa hivi. Nikaona mimi ndiye napoteza. Maana bado nina safari ya kilometers 400 hivi.

Naamua kulipa na kuondoka. Nimeudhika sana.
Nimewahi kuandika humu ndani nikiomba ufanyike utafiti wa kisayansi kuona kama kufanya kazi katika mazingira ya harufu iliyopo vituo vya polisi hakuathiri uwezo wa kufikiri wa mtu. Tusije tukawa tunawalaumu hawa askari juu ya uwezo wao wa kiakili kumbe ni tatizo la maradhi kutokana na hewa wanayovuta mara kwa mara kwenye vituo vya polisi
 
Niko safarini kutoka kanda ya kati kuelekea Geita.
Nafika eneo fulani mkoani singida. Wale wenye sare nyeupe wananyoosha mkona kuashiria nisimamishe gari...
Ulikuwa sahihi tangu awali, na ulikuwa sahihi kuchukua maamuzi uliyofikia.

Japo ni dhahiri kuwa jamaa alipaswa kuwa mwelewa.

Madereva wa malori hukutana na usumbufu wa aina hii mara kwa mara.

Ni vyema kusimama kwenye sheria na ungekuwa sahihi kupinga maamuzi yake lakini ulijari mda wako.

Kazi haimfanyi mtu apoteze utu ilihali sio haramu bali kuna baadhi ya uwajibikaji hufanya baadhi ya kazi kutoheshimika licha ya kuwa wapo wenye kutenda ipasavyo.

Mfano Sare nyeupe.
 
Hapa unatupanga.
Faini ya kawaida huwa ni wiki ikipita inapanda mpaka kiasi fulani nimesahau ambacho utakapokamatwa unatakiwa ulipe hapo hapo, kama ni hii askari alikuwa sahihi...
Umesoma alichoandika? Hujui ilikuwa faini ya nini, na amesema kwenye mtandao kuna pay by date ambayo haijafika, halafu unasema ametupanga. Wewe ni Polisi nini? Na kama unalosema ni kweli,kwa nini Polisi wasimwambie tu kuwa japo kuna pay by date hii faini ni ya paop kwa hapo?
 
Kanuni ya kwanza uwapo barabarani unapokutana na askari daima.
Kuwa muungwana hata kwa kuigiza tu,ili maisha yaende,ubaya wa polisi ni kwamba, ana nafasi ya kukusumbua,kukupotezea muda na kama haitoshi ana nafasi ya kukusababishia kesi au hasara ukalala ndani.

Pole sana mkuu,ila naamini mlianza kwa namna tofauti.
Nikuwa muungwana. Nikamueleza vizuri tu kwamba nina safari ndefu. Nitalipa nikifika nyumbani. Aligoma kabisa.
 
Hapa unatupanga.
Faini ya kawaida huwa ni wiki ikipita inapanda mpaka kiasi fulani nimesahau ambacho utakapokamatwa unatakiwa ulipe hapo hapo, kama ni hii askari alikuwa sahihi...

Anasema "Fine Due Date" ni 29th May 2024... that means kukamilisha 7 days za kisheria... within such period of time Traffic hatakiwi kumsumbua mlipaji wala kumharakisha. Leo ni tarehe 25th. Mdaiwa bado ana siku 3 mbele za kufanya malipo husika.

Penalty (ongezeko) itaanza kuhesabu after 29th, na hapa sasa Traffic aweza kukusumbua.

-Kaveli-
 
Umesoma alichoandika? Hujui ilikuwa faini ya nini, na amesema kwenye mtandao kuna pay by date ambayo haijafika, halafu unasema ametupanga. Wewe ni Polisi nini? Na kama unalosema ni kweli,kwa nini Polisi wasimwambie tu kuwa japo kuna pay by date hii faini ni ya paop kwa hapo?
Huoni nimetoa maelezo kwa aina zote za faini na nini kunatakiwa? Ile ya parking huwa inakupa muda mrefu na polisi hahusiki,hatakiwi kukusumbua.

Ila ile faini ya polisi unapewa muda maalum usipolipa inaongezeka hadi kikomo chake then wakikunasa hutoki hadi ulipe. Kuna mkanganyiko hapo. Polisi sio wanyama ni watu,mkiacha ujuaji hawatawasumbua.
 
Anasema "Fine Due Date" ni 29th May 2024... that means kukamilisha 7 days za kisheria... within such period of time Traffic hatakiwi kumsumbua mlipaji wala kumharakisha. Leo ni tarehe 25th. Mdaiwa bado ana siku 3 mbele za kufanya malipo husika.

Penalty (ongezeko) itaanza kuhesabu after 29th, na hapa sasa Traffic aweza kukusumbua.

-Kaveli-
Sasa kwanini kakubali kulipa? Aje aseme hapa ni faini gani.
 
Kanuni ya kwanza uwapo barabarani unapokutana na askari daima.
Kuwa muungwana hata kwa kuigiza tu,ili maisha yaende,ubaya wa polisi ni kwamba, ana nafasi ya kukusumbua,kukupotezea muda na kama haitoshi ana nafasi ya kukusababishia kesi au hasara ukalala ndani.

Pole sana mkuu,ila naamini mlianza kwa namna tofauti.
Uwe mnyenyekevu kwa wao kukosa uadilifu? Uungwana ni muhimu ila si kwasababu mtu atakusingizia kesi, hii sio sawa.
 
Huoni nimetoa maelezo kwa aina zote za faini na nini kunatakiwa? Ile ya parking huwa inakupa muda mrefu na polisi hahusiki,hatakiwi kukusumbua. Ila ile faini ya polisi unapewa muda maalum usipolipa inaongezeka hadi kikomo chake then wakikunasa hutoki hadi ulipe. Kuna mkanganyiko hapo. Polisi sio wanyama ni watu,mkiacha ujuaji hawatawasumbua.
Sikubaliani na kauli Polisi sio wanyama, wengi wao ni wanyama!
 
Traffic polosi wana roho mbaya sana wakikukuta na kosa. Halafu pia wanapenda kuomba pesa kama wakiona huna kosa , huwa nawashangaa sana.

Siwezi mpa polisi pesa hata iweje, ni bora aniandikie fine.
 
Back
Top Bottom