Je, baba alitutesa au alitufundisha maisha?

Je, baba alitutesa au alitufundisha maisha?

Baba yangu alikuwa kanali wa jeshi la wananchi (jwtz)huko kusini mwa Tanzania mkoa unaozalisha mahindi kwa wingi hapa nchini mzee wetu alikuwa mkali Sana

Nakumbuka mwaka 2008 wakati Mimi nko darasa la sita ,kaka yangu mkubwa first born yupo form one na mdogo angu marehemu kwa Sasa (r.i.p) tulipewa kazi ya kubeba tofali 100 Mimi na Kaka, mdogo wetu abebe tofali 50 na sehemu zilipokuwa tofali ni mbali Sana hakuna gari unabeba kichwani unavuka Kama mitaa 3 mikubwa nakumbuka siku Ile tulibeba tofali mpaka unalia njia nzima unapumzika ukikutana mtu mnaye fahamiana anakupiga tafu kidogo,nakumbuka bimkubwa alikuwa ana toa machozi kutuhurumia na sauti kwa mzee hana ilibidi tupambane tu

Tukio lingine home tulikuwa na eneo kubwa mzee alipanda miti ya matunda na migomba kila mtu alipewa miti yake ole wake mti wako unyauke utachezea fimbo na adhabu zakutosha
Ukirud shuleni baada ya kula unachukua ndoo zako unaenda mtoni kuchota maji tulikuwa tunaisha karibu na mto na usiku ata arudi saa 6 anachukua tochi anapita kugagua kila mti Kama umepata maji ya kutosha ole wako usimwagilie utaenda mtoni usiku kuchota maji umwagilie

Nakumbuka nilikuwa mchezaji mzuri Sana wa mpira nishachaguliwa Sana umintashuta na umisenta kwenda kuwakilisha shule kwenye soka Ila tatizo mzee alikuwa hataki kusikia habari za mpira alichotaka yeye ni kusoma tu na saa 12 jioni uwe ndani kipaji kikapotea...

Tukio lingine nyumbani tulikuwa tunafuga kuku Kuna siku moja kuku mmoja jogoo kumbe hakulala ndani na sisi hatukukagua na tulikuwana na jogoo mmoja tu kwa wakati huo usiku kumbe mzee ajalala anasikilizia saa 9 jogoo awike kimya saa 11 alfrajiri Tena kimya jogoo ajawika akatoka kwenda chumba Cha kuku kuangalia kumbe yule jogoo hayupo nakumbuka tuliamsha wote nyumba nzima tukatafute kuku Hadi tumpate ilikuwa kasheshe kila pori tunatafuta hatuna ata tochi tulifanikiwa kumpata asubuhi kesi ikaisha

Ni matukio mengi Sana yalitokea home mzee alikuwa mafia afu acheki ovyo majirani walikuwa wanamuogopa Sana
Nw kastaafu yupo nyumbani tu Japo ukali umepungua wajukuu na ndugu wanaoishi pale wananienjoy tu
Mzee wenu alikuwa na nia njema juu yenu ila hakuwa na elimu sahihi ya kuwafundisha.
Yy alikuwa ana apply military techniques kwa watoto tena ni under 18..

huo ni ukatili aliwafanyia.
 
Alifanya vyema maana aliwaandaa kwa ajili ya kupambana na hii dunia ya kiwaki.
Angezubaa mngekua mchele mchele, vijana rojo rojo mnaopenda kuita ita dadi .
ENDELEZA moto huo huo kwa wanao.
Mwanaume ukipenda kudekezwa huchelewi kufinywa kajicho.
Hongera nyingi ziende kwa huyo soja.
Mkuu fact but kwa wanang na hii dunia ya Sasa nisije nikapata kesi ya child abuse Ila respect nyingi kwa mshua master
 
Aliwafundisha maisha ilo la tofali mmh ni noma
Alitufundisha maisha Ila kwa tofali ilikuwa kisanga unabeba tofari huku machozi yanatoka afu njaa inauma kinoma nakumbuka nilikuwa nabeba afu narudi nyuma kumsaidia dogo tofali zake na Kaka mkubwa akawa ananisaidia Mimi
 
Naskia Marehem Maghufuli alishawahi mueleza mkewe kwamba Kuna mtu ataleta mchanga tipa moja, mwambie amwage sehemu flan, watu wa mchanga walipokuja mama Janet hakusimamia ule mchanga umwagwe sehemu ambapo Maghufuli alisema umwagwe, Maghufuli kurudi akamwambia mke wake kwamba, kwa sababu ulizembea mchanga ukamwagwa ndipo sipo, usombe upeleke nlipokuwa nimesema, mama wa watu akaanza kuusombelea na karai anabeba kichwani .
Nakumbuka mama yetu ametusaidia Sana kubeba mchanga kwenye nyumba yetu mpya kipindi hicho mpaka tunamaliza gari nzima
 
Hongera sana kwa huyo afande baba mzazi, kama bado yupo hai ninakushauri uchukue zawadi umpelekee kutoa shukrani japo kibinadamu utakuwa ukiumia roho kiaina kwamba alikunyanyasa [emoji1][emoji1][emoji1]. Mimi nimekuja kuelewa ukubwani maana ya hiki ulichoandika maana kilinitokea katika maisha, na ninawashukuru sana wazazi wangu wapendwa kwa yale waliyonifundisha maana yana faida kubwa [emoji120].
Respect sanaa nyingi kwa mshua🙌
 
Kweli alizidisha ukali na ukatili pia. Na nyie muwe waangalifu msiwe kama mzee wenu kwani mtoto wa nyoka nyoka pia.

Baba ni baba tu, sasa amezeeka amekuwa mpole mtunzeni. Malezi ya ukali na ukatili hayamfanyi mtu kuwa bora, wazazi wengi hawajui hili.
Mkuu respect nyingi kwa mshua
 
𝑫𝒖𝒉, 𝒗𝒊𝒋𝒂𝒏𝒂 𝒕𝒆𝒑𝒆𝒕𝒆𝒑𝒆 𝒃𝒂𝒏𝒂....𝒔𝒊𝒆 𝒕𝒖𝒍𝒊𝒌𝒖𝒂 𝒎𝒑𝒌 𝒕𝒖𝒏𝒂 𝒎𝒄𝒉𝒂𝒌𝒂𝒎𝒄𝒉𝒂𝒌𝒂 𝒘𝒂 𝒇𝒂𝒎𝒊𝒍𝒊𝒂, 𝒏𝒅𝒐 𝒌𝒊𝒔𝒉𝒂 𝒖𝒘𝒂𝒉𝒊 𝒔𝒉𝒖𝒍𝒆, 𝒔𝒂𝒂 12 𝒌𝒂𝒎𝒊𝒍𝒊 𝒛𝒊𝒏𝒂𝒉𝒆𝒔𝒂𝒃𝒊𝒘𝒂 𝒏𝒂𝒎𝒃𝒂....
Familia za kijeshi hizo
 
Lazima upate tafsiri mpya ya KITU inaitwa mateso kichwani mwako hii kauli tulikuwa tukiambiwa akiwepo mjengon.
Kama uliweza kuhandle stress basi alikufunza namna ya kureact na kurespond pale unapokutana nazo.
Fact mkuu
 
Back
Top Bottom