Je, Balozi Ombeni Sefue ndiye mshauri Mkuu wa Rais Samia?

Je, Balozi Ombeni Sefue ndiye mshauri Mkuu wa Rais Samia?

Balozi sefue yupo smart kidogo na huyo judge mstaafu nae yupo fiti natumaini majeshi yatakuwa na mwondoko mpya baada ya ripoti zao.

Hayo majeshi yatayopata muondoko mpya kwa ushauri wa wastaafu, ujue hapo hakuna majeshi, bali makundi yenye silaha ya kulinda tabaka la walio kwenye madaraka.
 
Hili ni swali zuri sana. Kulijibu sharti uwe makini. Katika hali ya kawaida kama Bosi siyo mlevi wa kuabudiwa, ni mdadisi na si mvivu wa kusoma na kutembelea maeneo yake na kukagua kazi hakuna atakayedhubutu kuchukua rushwa. Lakini akiwa ni mtu mzubao anayependa kusifiwa, kupokea zawadi za hapa na pale, kuandaliwa sherehe na mapambio, anaweza asipokee rushwa lakini akaruhusu walioko chini yake wakapokea rushwa kwa niaba yake tena kwa wingi mnoo. Wa aina hii huweka sahihi document bila hata kuzipitia na bila kujua kilichopo ndani ya document anayoweka sahihi kwa sababu tu imeletwa kwake na mfanyakazi fulani anayempenda au anayemwamini. Hapo ukiongezeka ufuska basi tena.

..Na bosi akiwa katili, laghai, na mbaguzi, wasaidizi wake watafanya anavyopenda bosi. Hali hiyo tuliishuhudia ktk awamu ya 5.
 
Kazi wanazopewa wazee wetu wastaafu sio ajira as such ni kazi za muda mfupi, na zinahitaji watu wazoefu, hakuna ubaya wowote kwenye kuwapa hizo kazi, hawachukui ajira ya mtu, tutumie uzoefu wao kwa maslahi ya Taifa
Huo uzoefu wao umeshindwa kufanya kazi walipokuwa kazini, wameshachoka ndio wakaririshe watu philosophy za zamani!
 
Busara imetumika kwenye viongozi wa hiyo kamati. Mmoja ni jaji mkuu mstaafu na mwingine ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu. Hizo ndio kazi zao. Who else would someone wish zaidi ya hao? Kama hao hawana busara za kumshauri kiongozi mkuu wa nchi, basi hali yetu ni tete.

..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
 
..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
Maswali murua sana hayo!
 
Pamoja na kwamba nipo nyutro vitu vingi, lakini Balozi Sefue ni mojawapo ya senior citizen wetu ambao wana akili na busara na kufanya maamuzi kwa kiasi. He does not possess extreme behaviour. Lakini pia anajua nini ambacho dunia inataka.
Sefue ni sampuli ya Balozi Mahiga.
Nakubaliana na wewe
 
..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
Bado hazijawekwa wazi. Kama una maoni yako juu ya composition na hadidu za rejea, basi toa kupitia channels au hata mitandao kama huu hapa.
Lakini pia usidhani kwamba ndani ya serikali hakuna watu wenye mawazo sawa na wapinzani. Ni kwa sababu tu ya busara ya kutokuwa mropokaji ndani ya serikali.
Mimi naamini kutakuwa na wajumbe wasiotumia hisia zaidi(driven by emotions). Na hawa mara nyingi ni watumishi wa umma wastaafu.
Kuna wakuu wastaafu wa hivyo vyombo.
 
Kwa sasa tunatakiwa tujadili na kutia maoni juu ya hadidu za rejea za kamati.
Mama Samia ametutendea haki. Ametupa nafasi ya kutoa maoni juu ya miundo ya Majeshi yetu. What a chance! Hii ni penatly kabisa. Hatutakiwi kukosa. Tupige mpira golini.
Mimi naona swala la Sifa za kujiunga na majeshi lisisahaulike na Recruitment Mechanism zote za vyombo vyetu. Mitaala katika vyuo vyao. Mifumo yao ya ajira, mifumo ya kupanda vyeo, Uhuru wao dhidi ya Watawala na Chama tawala. How independent are they in our security organs?
 
Ngoja tujazie nyama ili kamati ya Raisi ipate vichwa stahiki. Napendekeza Prof Haji Semboja huyu ni mchumi lakini amekuwa mshauri kwa miaka mingi kuhusu maboresho ya Polisi kwa hiyo ana uzoefu wa kutosha

Yupo Ndugu wakili msomi Peter Madeleka huyu ni wakili na amekuwa kwenye harakati za kuhimiza maboresho ya jeshi letu la polisi na yeye alikuwa polisi.

Yupo Ndg Albert Shelukindo huyu ni Security consultant na amewahi kuhudumu kwenye jeshi la polisi la uingereza japo kwa sasa yupo sekta binafsi kama Security Executives, Watu kutoka TLS hata Hosea ana madini mengi kuhusu utendaji wa polisi, TAWLA, Hata IGP mstaafu Saidi Mwema atafaa kuwa ndani ya kamati.

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
 
Kazi wanazopewa wazee wetu wastaafu sio ajira as such ni kazi za muda mfupi, na zinahitaji watu wazoefu, hakuna ubaya wowote kwenye kuwapa hizo kazi, hawachukui ajira ya mtu, tutumie uzoefu wao kwa maslahi ya Taifa
Watu wana wivu
Wako radhi sijui apewe yule KMK wa Magu

When it comes to experience inabidi kuheshimu baadhi ya watu
 
Ngoja tujazie nyama ili kamati ya Raisi ipate vichwa stahiki. Napendekeza Prof Haji Semboja huyu ni mchumi lakini amekuwa mshauri kwa miaka mingi kuhusu maboresho ya Polisi kwa hiyo ana uzoefu wa kutosha

Yupo Ndugu wakili msomi Peter Madeleka huyu ni wakili na amekuwa kwenye harakati za kuhimiza maboresho ya jeshi letu la polisi na yeye alikuwa polisi.

Yupo Ndg Albert Shelukindo huyu ni Security consultant na amewahi kuhudumu kwenye jeshi la polisi la uingereza japo kwa sasa yupo sekta binafsi kama Security Executives, Watu kutoka TLS hata Hosea ana madini mengi kuhusu utendaji wa polisi, TAWLA, Hata IGP mstaafu Saidi Mwema atafaa kuwa ndani ya kamati.

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
Mkuu ni kwanini umechelea kumtaja au kumpendekeza Kibatala?
 
Watu wana wivu
Wako radhi sijui apewe yule KMK wa Magu

When it comes to experience inabidi kuheshimu baadhi ya watu
... Dr. Bashiru Ally? The shortest serving Chief Secretary in history.
 
Attachments

  • 33c43059-8bad-4efe-b85c-aa45b6d50bfe.jpeg
    33c43059-8bad-4efe-b85c-aa45b6d50bfe.jpeg
    129.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom