Je, Balozi Ombeni Sefue ndiye mshauri Mkuu wa Rais Samia?

Balozi sefue yupo smart kidogo na huyo judge mstaafu nae yupo fiti natumaini majeshi yatakuwa na mwondoko mpya baada ya ripoti zao.

Hayo majeshi yatayopata muondoko mpya kwa ushauri wa wastaafu, ujue hapo hakuna majeshi, bali makundi yenye silaha ya kulinda tabaka la walio kwenye madaraka.
 
..Na bosi akiwa katili, laghai, na mbaguzi, wasaidizi wake watafanya anavyopenda bosi. Hali hiyo tuliishuhudia ktk awamu ya 5.
 
Kazi wanazopewa wazee wetu wastaafu sio ajira as such ni kazi za muda mfupi, na zinahitaji watu wazoefu, hakuna ubaya wowote kwenye kuwapa hizo kazi, hawachukui ajira ya mtu, tutumie uzoefu wao kwa maslahi ya Taifa
Huo uzoefu wao umeshindwa kufanya kazi walipokuwa kazini, wameshachoka ndio wakaririshe watu philosophy za zamani!
 
..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
 
..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
Maswali murua sana hayo!
 
Nakubaliana na wewe
 
..Wajumbe wengine wa Tume / Kamati hiyo ni kina nani?

..Na hadidu za rejea za Tume / Kamati ni zipi?

..Je, kuna mtu yeyote toka UPINZANI yuko ktk tume hiyo, maana wao ndio wamechagiza iwepo.
Bado hazijawekwa wazi. Kama una maoni yako juu ya composition na hadidu za rejea, basi toa kupitia channels au hata mitandao kama huu hapa.
Lakini pia usidhani kwamba ndani ya serikali hakuna watu wenye mawazo sawa na wapinzani. Ni kwa sababu tu ya busara ya kutokuwa mropokaji ndani ya serikali.
Mimi naamini kutakuwa na wajumbe wasiotumia hisia zaidi(driven by emotions). Na hawa mara nyingi ni watumishi wa umma wastaafu.
Kuna wakuu wastaafu wa hivyo vyombo.
 
Kwa sasa tunatakiwa tujadili na kutia maoni juu ya hadidu za rejea za kamati.
Mama Samia ametutendea haki. Ametupa nafasi ya kutoa maoni juu ya miundo ya Majeshi yetu. What a chance! Hii ni penatly kabisa. Hatutakiwi kukosa. Tupige mpira golini.
Mimi naona swala la Sifa za kujiunga na majeshi lisisahaulike na Recruitment Mechanism zote za vyombo vyetu. Mitaala katika vyuo vyao. Mifumo yao ya ajira, mifumo ya kupanda vyeo, Uhuru wao dhidi ya Watawala na Chama tawala. How independent are they in our security organs?
 
Ngoja tujazie nyama ili kamati ya Raisi ipate vichwa stahiki. Napendekeza Prof Haji Semboja huyu ni mchumi lakini amekuwa mshauri kwa miaka mingi kuhusu maboresho ya Polisi kwa hiyo ana uzoefu wa kutosha

Yupo Ndugu wakili msomi Peter Madeleka huyu ni wakili na amekuwa kwenye harakati za kuhimiza maboresho ya jeshi letu la polisi na yeye alikuwa polisi.

Yupo Ndg Albert Shelukindo huyu ni Security consultant na amewahi kuhudumu kwenye jeshi la polisi la uingereza japo kwa sasa yupo sekta binafsi kama Security Executives, Watu kutoka TLS hata Hosea ana madini mengi kuhusu utendaji wa polisi, TAWLA, Hata IGP mstaafu Saidi Mwema atafaa kuwa ndani ya kamati.

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
 
Kazi wanazopewa wazee wetu wastaafu sio ajira as such ni kazi za muda mfupi, na zinahitaji watu wazoefu, hakuna ubaya wowote kwenye kuwapa hizo kazi, hawachukui ajira ya mtu, tutumie uzoefu wao kwa maslahi ya Taifa
Watu wana wivu
Wako radhi sijui apewe yule KMK wa Magu

When it comes to experience inabidi kuheshimu baadhi ya watu
 
Mkuu ni kwanini umechelea kumtaja au kumpendekeza Kibatala?
 
Watu wana wivu
Wako radhi sijui apewe yule KMK wa Magu

When it comes to experience inabidi kuheshimu baadhi ya watu
... Dr. Bashiru Ally? The shortest serving Chief Secretary in history.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…