Je bei ya usafirishaji mizigo toka China Kwa CBM ni kiasi gani Kwa wastan

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Naomba kujua wastani wa bei ya usafiri Kwa njia ya Meli toka China kuja Tanzania Kwa CBM.

Nimepanga kuagiza bidhaa Fulani Fulani Kwa ajili ya kuuza huku KWa jumla, supply akanipa CBM ya mzigo kuwa ni 7.29 na bei ya manunuzi na usafiri Hadi Kwa agent wangu ni TSHS. 5,800,000/=, nikamuuliza huyo agent kabla mzigo hujaenda kuwa Kwa CBM hizo bei ya usafirishaji inaweza kuwa Shilingi ngapi.

Jibu nililopewa ndio nimechoka, ni 450$ Kwa CBM, Yaani ni zaidi ya 8Milion TSHS.

Nataka kujua kama wastani wa usafiri Kwa mzigo kama huo inaweza kuwa hiyo.
 
Nimepanga kuagiza bidhaa Fulani Fulani Kwa ajili ya kuuza huku KWa jumla, supply akanipa CBM ya mzigo kuwa ni 7.29
  • Hapo kwenye fulani Fulani ndio hasa penye kutupatia gharama halisi.
  • Ila kwa kuwa umeficha, acha tuishie hapo, iko hivi range ya usafirishaji ni kati ya USD 340 hadi USD 700 kwa CBM 1: kwa kutegemea mambo mawili.
1. Shipping agent.
2. Ni bidhaa ipi kati ya hizo bidhaa Fulani Fulani

Image itakusaidai kuweza kupa idea jinsi bei zilivyo kwa bidhaa fulani fulani.


- Ili kujua kwa TZS utalipa kiasi gani; Uliza shipping agent wako je USD 1 = Anafanya kwa TZS ngapi? ( Kila agent ana rate yake, hawafuatishi rate ya benki au BOT)
 
Nakaziaa 📌📌
 
Hapa inategemeana na unacho agiza lakin cubic meter moja unapata faida tena sana tu.

Mfano kama ni simu za viswaswadu kuvijaza mpaka kufikia cbm 1 ujue ni vingi na nahisi ni duka zima
Nataka na accessories zake kama chaji, earbuds, wireless earphone na betri za viswaswadu, Sasa kama Sina supplier wa uhakika napo wanasaidia, mkuu faida ipo kweli kwa biashara hiyo
 
Nataka na accessories zake kama chaji, earbuds, wireless earphone na betri za viswaswadu, Sasa kama Sina supplier wa uhakika napo wanasaidia, mkuu faida ipo kweli kwa biashara hiyo
Kuhusu faida pia inategemeana na eneo ulipo je ina mzunguko mzuri wa biashara husika(bidhaa husika)

Yeah makampuni mengi ya usafirishaji yana saidia pia kukutafutia supplier wa uhakika,

Wewe unawapa pesa kampuni wao ndio wanafanya kila kitu kuanzia kumtafuta supplier kufanya savey, kununua bidhaa mpaka kukusafirishia bidhaa kufika Tanzania na mpaka kufika mkononi mwako.

Kikubwa upate tu kampuni yenye review nzuri katika kusafirisha na kufanya yote hayo.

Na zingatia tu kampuni nyingi hua zinaanzia cbm 1 hua ni 450 doller
 
ASante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…