Je, biashara ya mochwari binafsi inaruhusiwa?

Je, biashara ya mochwari binafsi inaruhusiwa?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Wakuu ukigoogle utaona huko mambele hii ni biashara ya kawaida kabisa.

Kwa hapa kwetu sheria zikoje?. Je, sheria zinaruhusu mtu binafsi kuwa na mochwari binafsi?

Naomba mwenye abc za uhalali wa biashara hii, mchanganuo wa mahitaji n.k atuwekee hapa.
 
Wakuu ukigoogle utaona huko mambele hii ni biashara ya kawaida kabisa.

Kwa hapa kwetu sheria zikoje?. Je, sheria zinaruhusu mtu binafsi kuwa na mochwari binafsi?

Naomba mwenye abc za uhalali wa biashara hii, mchanganuo wa mahitaji n.k atuwekee hapa.
Hata kenya kuna baadhi ya funeral houses zinakuwa na mortuary. Nadhan hapa tz ni possible pia
 
Kwa kuwa watu wanakufa bila hata ya kupimwa wamekufa kwa sababu gani? Basi hata hii itakuwa rahisi tu kupokea maiti na kuhifadhi na hata unaweza kuwa Funeral Director yaani ukaandaa mazishi yote mpaka kupeleka makaburini
Anza mkuu ila kwa gharama pia
Unahitaji kwanza Generator kubwa la uhakika la kufanya 24/7
 
Inawezekana kweli ni uoga wangu, huwa nikipita maeneo wanakouza majeneza huwa naangalia pembeni kabisa nisiyaone, makaburi pia hivyo hivyo.
Mimi nilikuwa naogopa sana,baba yangu mzazi alifia mikononi mwangu!Hapo Sasa siogpopi hata naweza kulala chumba Kimoja na maiti!
 
Huu unaitwa ubunifu
miaka ya nyuma hapa nchini let say kuanzia miaka ya 1979 kurudi nyuma ilikuwa ni ajabu sana kusikia kuna watu wanafanya biashara ya majeneza kwa maana kwamba wanayatengeneza huku wakijua hakuna mtu kafariki kama ilivyo sasa wanatengeneza na kwa uzoefu wao wameshafanya statistics kujua watu wengi wanakufa ni wa size gani hasa pamoja na watoto.Na siku ukienda kununua wanasindikiza na neno karibu tena yaani ufiwe tena.

Kwa sasa watengeneza majeneza wengi wako karibu na hospitali kubwa kubwa kama Muhimbili,KCMC,Bombo,Bugando n.k haionekani ni uchimvi au tena ni jambo la kawaida.
Funeral home kama ilivyo nchi za Ulaya,Marekani sina uhakika kwa kweli kwamba zipo chini yaani wewe mtu wako akifa unakwenda tu kutoa taarifa watakusaidia kumuosha kumuandaa na mazishi unapewa hata gari la kwnda kumzika wakiwepo na ndugu zako wachache.Ila ninachojua kwa nchi yetu kwa sasa kuna kuvaa sare za msiba na kuna kabila nasikia hata ukitaka waliaji utakodisha.

Yote haya ni maendeleo na mabadiliko ya kijamii ni vigumu kuyazuiya
Kuna kutunza maiti mortuary vinakwenda na funeral home sina uhakika hili lipo nchi yetu lakini ni bonge la dili ila serikali ikiruhusu mhusika lazima kuna vigezo atapewa mfano awe mtaalamu wa pathology au cheti.

Ninakotoka kuchimba makaburi siku hizi kuna watu maalum wakipewa hela wanachimba ndugu wa marehemu wanakabidhiwa shimo kulingana na imani za kidini za watu tofauti.
Kwenye harusi nako siku hizi watu hawahangaiki na kupika kama vijijini wanakodisha buffe wewe unasema tu idadi ya watu kila kitu utafanyiwa huna haja ya kununua mchele,au mafuta unaepuka wizi wa vyakula na watu kuchambana au wanaharibu shughuli yako makusudi majirani.

Kuna kitu inanaitwa Cremation yaani kwa watu waliokosa pa kuzika ardhi ila kwa hapa kwetu kuna watu wa imani flani wanachoma miili huenda nalo litakuja.
 
Back
Top Bottom