Je, biashara ya Uwakala inalipa? Nina milioni 2, inatosha kuanzia?

inalipa mwaya tena ni mtaji mkubwa tu kama kodi na line unazo tayari unatosha kuanzia kikubwa umakini na consistency
 
Inalipa ila kabla ya kuifanya tambua kuwa kuna Chuma ulete.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Inalipa ndiyo..... lakini kabla ya kujiingiza kwenye biashara hii ni vema ukajua kinaga ubaga faida zake na hasara
 
Inalipa,lkn kwa kias hicho,inabid uwe eneo lenye movement kubwa sana ya watu, pia usiwe na benk yoyote kwa sabab itakulazim walau kuwa na 10m plus
l
Ubaya wa akiwa kwenye movement kubwa hiyo pesa ni ndogo.

Labda sehemu za kawaida, ila sio sehemu kama makumbusho stand, mbezi kimara, kariakoo, zenye mishe mishe nyingi.

At least awe na 5M.

Sababu sehemu yenye movement kuna mtu anakuja kutoa 1m mwingine laki8 huna kazi tena,
Na milion2 anaanza na line ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…