Kijana kijana
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 2,546
- 2,621
Ahaahhaaa huu wimbo rafiki yangu kiranga ushauimba sana.Ingekuwa vizuri sana kama ungethibitisha Mungu yupo kabla ya kuniombea kwa huyo Mungu.
Thibitisha yupo.
لا يحتاج كثير من القوة في إثبات وجود الله سبحانه وتعالى
"haihitaji nguvu nyiiiiiingi kuthibitisha uwepo wake Allah"
Mimi kwa mujibu wa kitabu changu cha imani nathibitisha na nakiamini kinaweza kuniridhisha uwepo wa Mola.
Sasamfano tu
بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله الذي خلق السماوات والأرض وجعل الظلمات والنور ثم الذين كفروا بربهم يعدلون
[ AL - AN-A'AM - 1 ]
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi.
Hapo ni uthibitisho wa Uwepo huyomwenye sifa njema.
Kwa mujibu wa imani na kitabu changu Nathibiutisha yupo Mola kwa maandiko mfano wa hayo juu.
Kama ambavyo nathibitisha uwepo wa isack newton kwa kupitia maandishi basi ndivyo nathibitisha uwepo wa Mola kupitia maandishi ninayoyaamini.
Sasa hiyo ndo njia ambayo nimeitumia kuthibitisha uwepo wa Mola bwana kiranga au unaweza kunichagulia njia ya uthibitisho labda ukasema "nataka uthibitishe uwepo wa Mola kupitia njia fulani na fulani na sio maandiko ya kitabu chako cha imani"
Kama utasema hivyo litakuwa suala lingine ila nadhani ulitaka uthibitisho tu kuhusu uwepo wake nimekupatiaa kwa ufupi.
Asante