Mkuu, mengine siyajui but hili la binadamu wa kwanza kuishi mbinguni wewe unalitoa wapi!? Adamu aliumbwa hapa hapa duniani, sio mbinguni, ni pale mashariki ya kati na hiyo bustani ilikua pale pale mashariki ya kati and most probably ni nchini Iraq ya leo, soma vizuri Biblia, utakuta hiyo bustani ya Eden inaoneksana Mto Frati ni miongoni mwa mito ilioizunguka hiyo bustani, mto huo upo hadi leo, angalia kidogo atlas/ramani ya mashariki ya kati pale, mto huo upo Iraq ya leo. Sema baada ya makosa ya Adamu na Hawa ndipo walifukuzwa kwenye hiyo bustani na kuishi nje ya bustani cause waliambiwa, "kwa jasho mtakula (Adam, may be wanaume wote) na mtazaa watoto wenu kwa uchungu (Hawa and may be wanawake wote)