Je, binadamu wapo katika hatari ya kutoweka kwenye uso wa Dunia?

Asteroid ilivyodondoka;

1. ilitetemesha ardhi, vumbi likajaa kwenye atmosphere, mimea mingi ikakosa mwanga

2. iliharibu tectonic movements, kukawa na matetemeko ya ardhi, milipuko ya volcano na tsunamis

kuna viumbe vilibaki pamoja na mizizi, mbegu za mimea, hili tukio lilikuwa la mpito tu

sema hii ni nadharia tu, zipo nyingi ila hii ndo inakubalika zaidi
 
dah, huwa nashangaa sana watu wanaobishana na sayansi tena bila hoja kabisa,.....kama wachache wanaoropoka hapo juu🚮🚮

turudi kwenye mada,.... binadamu kutoweka kabisa kwenye uso wa dunia ni jambo ambalo linaweza kutokea muda wowote ule kwa sababu tajwa hapo juu,.... LAKINI haitakuwa rahisi, kwasababu ya uwezo mkubwa sana wa AKILI ya mwanadamu katika kupambana na majanga mbali mbali,....
 
Hawakufa viumbe wote. Kuna viumbe kibao kama mende, mamba na papa bado wanadunda
 
Binadamu hakuzuka tu ghafla kwenye uso wa Dunia. Viumbe hai wengi walipatakina baada ya mabadiliko mbalimbali ya Kibaiolojia, uwepo wa binadamu Duniani ni mada pana sana ambayo inapingana kati ya Sayansi na Dini.
Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani baada ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Inakuwaje Dinosaurs wapotee tu wao wenyewe?

Je ina maana kwamba kabla ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Kulikuwa hakuna viumbe wengine?

Je dinosaurs pekee ndio viumbe vilivyo toweka duniani vyenyewe tu?

Je dinosaurs pekee ndio viumbe pekee kuishi duniani kabla ya viumbe wengine wote?

Je dinosaurs ndio viumbe pekee kuishi duniani kabla ya species zote za mimea?

Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani baada ya hayo mawe makubwa kuanguka duniani, Dinosaurs walishindwaje na wao kuendelea kuwepo duniani?

Iweje dinosaurs tu, wapotee halafu viumbe wengine waendelee kuwepo?

Sasa kama madhara ya hayo mawe makubwa yaliyoanguka duniani yalikuwa makubwa kiasi hiki, Viumbe wengine waliwezaje kutokea duniani?

Kama viumbe wengine waliweza kutokea duniani licha ya hayo mawe makubwa na athari zake, Dinosaurs na wao walishindwaje kuendelea kuwepo?
Mawe yaliyoanguka yalikuwa na kipenyo cha kilometa 10, hivyo isingewezekana mawe hayo kuchukua eneo lote la Dunia. Ila athari zake zilikuwa ni kubwa zaidi.
Mbona hizo athari za hayo mawe hazikuzuia viumbe wengine kuendelea kuwepo duniani?

Kama viumbe wengine viliweza kuwepo duniani licha ya hizo athari za mawe, Dinosaurs walishindwaje na wao kuendelea kuwepo?
 
Hufikirii mbali. unadhani Gimba lenye uzito mkubwa nusu ya uzito wa dunia likigonga duniani watu hawawezi kufa?. Inawezekana jiwe lisikufikie na hata dunia isipasuke ila linaweza kubadilisha mfumo wote wa kusapoti maisha
Jiwe la nusu uzito wa dunia siyo jiwe, hiyo ni sayari kabisa.
 
Je viumbe wengine na binadamu walikujaje kuwepo tena duniani?
Dinosaurs ndiyo walikuwa top of the food chain. Chukulia mfano kwenye mbuga watoweke wanyama spishi zote kasoro Simba na Nyumbu. Namba yao iwe Simba 1,000 na Nyumbu 1,000,000. Pia, spishi zote za mimea zitoweke kasoro spishi 10. Je, ni spishi ipi ya mnyama itaweza ku-adapt kirahisi zaidi kulingana na mabadiliko yaliyotokea?

Ndiyo kilichotokea Dinosaurs walishindwa kuendana na mabadiliko yaliyotokea na viumbe waliokuwa dominated kwenye food chain wakapata nafasi ya kuzaliana kwa wingi na baada ya muda Dinosaurs wakapotea kabisa. Pia Mamalia wengi walikuwa wadogo na wakijificha kwa Dinosaurs, wanyama wengine waliweza kuhimili mazingira magumu, pia baadhi ya spishi zilipata madhara madogo kama baharini.
 
Seriously? Hivi hukusoma hata basic Geography form 1 au umeisha la 5?
Elewa hoja vizuri.

Kama kuna mawe yali anguka duniani yakaleta athari. Inakuwaje sasa viumbe wengine viliweza kuendelea kuwepo duniani licha ya hizo athari?

Kwa nini Dinosaurs walishindwa kuendelea kuwepo?
 
Umeandika "Binadamu walianza kuonekana miaka milioni 6-7 baada ya Dinosaurs kutoweka kabisa baada ya mawe makubwa kutoka angani kuanguka Duniani."

Hii habari umeipata wapi?
 
Kwa nini viumbe wengine viliweza kubaki duniani hadi leo, ila tu dinosaurs pekee ndio wakatoweka?

Dinosaurs walishindwaje kuendelea kuwepo duniani kama viumbe wengine?

Au wakati hizo Asteroids zina anguka, Dunia ilikuwa na dinosaurs tu?
 
binadamu kila siku wanatoweka wanakufa hivyo ondoa wazo la kufikilia kutoweka kwa wanadamu kwamba ni nadharia hapana wanadamu tunatoweka kila siku mamilioni ya wanadamu hutoweka
 
Kwa nini viumbe wengine viliweza kubaki duniani hadi leo, ila tu dinosaurs pekee ndio wakatoweka?

Dinosaurs walishindwaje kuendelea kuwepo duniani kama viumbe wengine?

Au wakati hizo Asteroids zina anguka dunia ilikuwa na dinosaurs tu?
dinosaurs walikuwa na maumbile makubwa kwahiyo mahitaji yao ya kiikolojia yalikuwa makubwa pia(haswa chakula)

hivyo walipata tabu sana
 
Ah hizi semi za miaka milioni mia sita iliyopita sijuwi kiumbe gani alifanya hivi na hivi sijuwi walihama kwenda huku zinaumiza kichwa kwa kweli.
 
Hizo Asteroids zilileta milipuko.

Sasa ni viumbe gani wenye uwezo wa kuhimili milipuko?

Kama Dinosaurs walishindwa kuhimili milipuko ya hizo Asteroids, Viumbe wengine waliwezaje?

Kama viumbe wengine waliweza kuhimili milipuko ya hizo Asteroids wakaendelea kuwepo, Dinosaurs walishindwaje na wao kuhimili hiyo milipuko?
 
liliua na wengine na wengine walisalimika.
Leta orodha ya species zilizo kuwepo kabla ya kuanguka kwa Asteroids.

Pia leta orodha ya viumbe vilivyo salimika na athari za Asteroids.

Pia leta orodha ya viumbe vilivyo toweka baada ya athari za Asteroids.

Asteroids zilileta milipuko, Je ni viumbe gani wana uwezo wa kuhimili milipuko?

Kama Dinosaurs tu walishindwa kuhimili milipuko ya hizo Asteroids, Je viumbe wengine ni non -flammable?
 
Niletee kwanza orodha ya species zote zilizowahi kuwepo duniani na kipindi zilichoishi ili niweze kukuchambulia.
 
Umeandika "Binadamu walianza kuonekana miaka milioni 6-7 baada ya Dinosaurs kutoweka kabisa baada ya mawe makubwa kutoka angani kuanguka Duniani."

Hii habari umeipata wapi?
Hapo nilikosea maana hicho kilikuwa kipindi cha Paleocene Epoch, maana ndiyo mfumo wa ikolojia ulikuwa unaanza kuimarika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…