Watanzania wengi hawapendi kujua ukweli. Nadhani hulka hii inatokana na wananchi kufungiwa nchini mwao na hivyo kukosa nafasi ya kuona jinsi nchi zingine zilivyoendelea.
Kuna siku Lema alisema bodaboda sio ajira, watu walikuja juu na kusema kuwa kawakosea watu na ni kama anadharau ajira za watu. Wadiriki kusema kuwa bodaboda ni Kama ajira zingine. Cha kushangaza leo hii viongozi hao hao waliomsema Lema, wamewafungia bodaboda wasifanye kazi ili wapishe mkutano, je watatoa fidia kwa bodaboda?