Watanzania wengi, kwasababu ya hali ya amani na utulivu vilivyoshamiri, tumekuwa na tabia ya kujisahau na kuishi kwa mazoea tukidhani ya kwamba kila kitu kiko sawa wakati wote kumbe wakati mwingine kujisahau huko hutoa mwanya kwa wabaya wetu kutudhuru.
Nirudi kwenye mada kwa kuanza na angalizo kwamba, nitakachokisema ni mtazamo na hofu yangu tu wala haimaanishi kufanya ubaguzi. Haya, ni hivi kuna mtu anajiita Bongo zozo, ameibuka hivi karibuni na kwa style yake ya kushabikia mambo mazuri ya nchi yetu. Ni jambo jema sana kwani inaonesha namna ambavyo hata wageni wanaikubali Tanzania.
Hali hiyo imetufanya tulio wengi ikiwemo na wewe Kigwangalla kubweteka na kuona kuwa kila kitu kiko sawa tu. Niulize tu, kuna wakati ulikwisha tenga kumfanyia uchunguzi na tathimini huyo mtu kujua ni raia wa wapi ambayo siyo issue kwani inawezekana yuko cleared na mamlaka husika. Lakini la msingi, ni nini motive behind kwa kujitolea kwake, nani anamsponsor, nini malengo hitimishi (ultimate goal) nk?
Nayasema haya, kama hofu yangu tu na wasiwasi tu na inawezekana kabisa ukanitoa wasiwasi huo nami nikawa na amani.
Vinginevyo inakuwaga hivi then linatokea jambo baya watu wanaanza kulaumiana (simaanishi bongo zozo ana mpango mbaya, ni hofu na mashaka tu ambayo najaribu kuyaweka kwenye maandishi).
Nakuachia Kigwangalla na mamlaka zingine husika kunitoa wasiwasi kumuhusu mtu huyo. Mi nikimwona akili huwa hainipi kabisa. Sorry incase nakosea namna ya kupresent jambo hilo lakini hiki ndicho ninachokihofia mimi, why shouldnt i put it open ili mnaomfahamu mtu huyo mnitoe hofu!