Je, Bunge likivunjwa Mawaziri wataendelea na kazi hadi Oktoba?

Hizo ni hisia zako tu. Utawala wa kidikteta haufuati katiba wala sheria.kwa hiyo unataka kulazimisha hapa Tanzania kuna udikteta?

Narudia tena, ww huwezi kuona maana ni mfaidika wa huu ukandamizaji. Hata weupe walifuata katiba yao.
 
Imefikia mahala nimetambua sasa kwanini hata musa alipata wakati mgumu Sana katika safari ya kuwapeleka wale Wana kaanani kuna watu wana vichwa vigumu na hawana shukrani wao kila kitu lawama. Hivi mnadhani ni nani atawaongoza awapendeze? Kila anayekuja lawama tu.
 
Narudia tena, ww huwezi kuona maana ni mfaidika wa huu ukandamizaji. Hata weupe walifuata katiba yao.
Haikuwa katiba kama hii ya JMT ambayo inazuia ubaguzi na udikteta.
Na nufaika na huu utawala? Sio kweli ni kusema ukweli tu.
 
Chini ya awamu hii, katiba ni sawa na gazeti la udaku. Hilo liko wazi. Ww ni mnufaika wa huu uovu, sina shaka na nisemalo.
 
Tarehe 16/06 Mhe. Rais anavunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama hakutakuwa na mabadiliko. Kisheria baada ya kuvunja Bunge hatutakuwa na mawaziri Kwa kuwa kikatiba Waziri lazima awe mbunge. Katika kipindi hicho Wizara zitaendelea kusimamiwa na makatibu wakuu mpk hapo uchaguzi mkuu utakapomalizika na uteuzi mpya kufanywa na Rais aliyechaguliwa.

Tunawakumbusha mawaziri wetu kutunza rasilimali za umma na waache kuendelea kuzunguka nazo mitaaani na maiimboni mwao kutafutia Kura. Najua nchi hii hatuna utamaduni wa kutii Sheria, sitashangaa kuona mawaziri waliomaliza muda wao wakiendelea na ziara kama kawaida na kutoa maagizo Kwa watendaji au hata kuwasimamisha kazi.

Hatutaacha kuwakumbusha maana ipo siku atakuja asiyejulikana, msije mkasema mlikuwa hamjui. Spika wetu yeye kajitoa ufahamu anaendelea kuchapa kazi na wabunge waliofukuzwa ktk vyama vyao na inawezekana wakalipwa kodi zetu wakatwange maisha mitaani.
 
Swali kwa wenye ufahamu.

Hivi hao wabunge, waliojiuzuru na kuvuliwa uanachama badala yake wakiendelea kusalia bungeni kwa msaada wa spika

, Siku mazingira yakiruhusu hawezi kufunguliwa mashtaka ya kuvunja katiba?
 
Spika hawezi kulifanya Hilo analolifanya kufanya kazi na wabunge walio fukuzwa au kuachia ngazi bila maagizo .
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini
 
Swali kwa wenye ufahamu.

Hivi hao wabunge, waliojiuzuru na kuvuliwa uanachama badala yake wakiendelea kusalia bungeni kwa msaada wa spika

, Siku mazingira yakiruhusu hawezi kufunguliwa mashtaka ya kuvunja katiba?
Spika anaweza akafunguliwa mashitaka kwa jambo hilo na lipo wazi kabisa ndiyo maana wameweka kinga ya kutoshitakiwa Spika na Naibu wake kwa kuwa amevunja sheria sana katika uongozi wake.
 
Tarehe 16/06 Mhe. Rais anavunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama hakutakuwa na mabadiliko. Kisheria baada ya kuvunja Bunge hatutakuwa na mawaziri Kwa kuwa kikatiba Waziri lazima awe mbunge. Katika kipindi hicho Wizara zitaendelea kusimamiwa na makatibu wakuu mpk hapo uchaguzi mkuu utakapomalizika na uteuzi mpya kufanywa na Rais aliyechaguliwa.
Tunawakumbusha mawaziri wetu kutunza rasilimali za umma na waache kuendelea kuzunguka nazo mitaaani na maiimboni mwao kutafutia Kura. Najua nchi hii hatuna utamaduni wa kutii Sheria, sitashangaa kuona mawaziri waliomaliza muda wao wakiendelea na ziara kama kawaida na kutoa maagizo Kwa watendaji au hata kuwasimamisha kazi.
Hatutaacha kuwakumbusha maana ipo siku atakuja asiyejulikana, msije mkasema mlikuwa hamjui. Spika wetu yeye kajitoa ufahamu anaendelea kuchapa kazi na wabunge waliofukuzwa ktk vyama vyao na inawezekana wakalipwa kodi zetu wakatwange maisha mitaani.

Inabidi tuombe Mungu tena tuombe kweli kweli kwa kuwa mamuzi mengi kwa sasa yanaenda kwa "Executive Order" kama ambavyo uamuzi ya wa kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani ulivyofanyika.

Atatokea mtu mwenye mamlaka yake ya duniani atatoa amri Mawaziri waendelee kuchapa kazi kwa kuwa katiba siyo Msahafu!!!!
 
Yaani katiba ipo hari kwenye app, unashindwa kudownload ili usome, badala yake unakuja kumwaga upumbavu hapa jukwaani. Mleta mada, hebu nenda kasome katiba kwanza ndiyo urejelee bandiko lako, ujishuhudie mwenyewe ulivyo kiazi.
 
Mara nyingi nasema Jambo hili. JF ni nyumba ya fikra pevu. Unatakiwa kujenga hoja za kisomi na siyo kutoa matusi. Kutukana ni fikra ya mwisho ya mpumbavu. Jitahidi kufikiri ndugu

Back
Top Bottom