Je, Captain Tesha, Habil na Kabil ilikuwa project ya Night walk ya Wana usalama?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Bado nipo njia panda, Namkumbuka Captain Tesha, utulivu wake, Maneno yake, na body language yake, kisha baadaye tukuo la sauti kuvuja za kina Mafwele na kikao chao.

Baadaye kabisa baada ya MO29 anazuka Mhusika Mwingine, machachari, unknown Character, anapata umaarufu mkubwa bila sura yake kuwa hewani,
Kiswahili chake cha kuokoteza kama Mswahili wa AI, huyu si mwingine, alijiita Habil na Kabil.

Anabonga, anatoa vitisho, watu wanavishwa na mshangao wakiwa hawajui wamuunge mkono au wampuuzie.

Habil na Kabil wanatoa vitisho na data bila kuzichambua kama ni kweli ama sio kweli. Watu wanakaribia kumuamini.
Habil anapigia simu maafisa aliowatambulisha kama viongozi wa polisi. Audio Ile anaiweka hewani.

Ni kama mtego wa sungura pori hivi. Imani inaongezeka na watu wanamuamini. Kwa kiwango Fulani.

Lakini Habil na Kabil anatoa taarifa jinsi D9 watakavyoifanyia kazi.
Bado watu wanamfuatilia, sasa kwa vile wanamuamini kwa kiwango cha kuridhisha, wanapunguza kufikiri na kuchunguza kile Anachokisema, hili linakuwa Kosa la kimedani.

Habil na Kabil wanahujumu D9 kwa kuelezea kinagaubaga nini wataenda kufanya, kuvamia Bandari, kuchoma minara ya simu, kuangamiza mali za wanamtandao, hapa akimhusisha Mfanyabiashara aitwaye Rostam Aziz. Huyu amemtaja mara kadhaa.
Hili pia linakuwa kosa ambalo nafikiri ni kosa la makusudi.

Wahusika hawa, je ni project ya Night Walk? Katika medani ya Kijasusi. Kuhujumu harakati na kuwa ku-act kama diverters wa vuguvugu zima?

Baada ya D9 kufeli, kutokana na hamasa na hofu ya picha itakavyokuwa iliyojengwa na Habil na Kabil na kundi lake, Jambo ambalo wao kama walikuwa wamedhamiria kikweli kweli hakukuwa na sababu ya kutoa picha kabla ya Siku yenyewe. Mambo engine yanatakiwa yafanyike Siku ya tukio na sio kuzungumzwa hadharani. Kimedani kuna mambo yanasemwa na kuonyeshwa siku ya operation.

Wale wazee wa Warmap, mastermind kwenye baadhi ya vipengele kwenye hii issue walicheza karata zao vizuri sana.

Baadaye ikaja TFF😀. Zikiwa Last card kufanya finish up ya mchezo.

Kimedani ukiona Adui yako anatumia zaidi New Characters zaidi ujue hiyo mechi unahitaji urudi kwenye meza ya kupanga vita vyako.

Swali linabaki, je Captain Tesha na Habil& Kabil ilikuwa Project ya Night Walk?

Kwenu Wataalam

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ukifatilia wanaharakati sasa hivi IG wana ugomvi wao kwa wao!
Baadhi ya taarifa walikua wanazitunga ili wachangishe michango mwisho wa siku wamedhulumiana.
Account nyingi zilikua zinatumia picha za Al.
Bongo hakuna activists, fikria mtu kama Maria Sarungi aliyeichukia serikali baada ya ugali wake kumwagwa anajitambulisha kama activist..
 
Ukifatilia wanaharakati sasa hivi IG wana ugomvi wao kwa wao!
Baadhi ya taarifa walikua wanazitunga ili wachangishe michango mwisho wa siku wamedhulumiana.
Account nyingi zilikua zinatumia picha za Al.

Kwa sehemu vijana wajanja hiyo kwao ni fursa ya kujipatia pesa huku wakitumia ukombozi kama ndoano na wananchi kama chambo
 
Wayback hatukuwahi kusikia habari za mashoga, sasa hawa mashoga ambao wapo kila kona ni kina nani? ni GEN Z

😁😁

Wako wapi huko Mkuu.

Mimi nipo mtandaoni almost muda wote lakini siwaoni.
Unaulizia habari zao mtandaoni au kujihusisha na habari zoa?
Maana mtandao unatabia ya kukuketea unachokiuliza, kitafuta
 
Wana Usalama hawafanyi project za kutania kufanya mapinduzi. Wanaweza kufanya spinining kama "mzee wa loliondo", au "popobawa", au "kumshika mtu bega nyeti zikapotea" lakini siyo project ya kumwambia na kumshawishi CDF achukue nchi!

Kuna mambo huyajui kimedani hasa yanayohusu operation na projects za Wanausalama.

Night Walk ni mbinu ya kimedani kupata taarifa, kutingisha mzinga wa nyuki ukiwa gizani kwa kuwasha moto, kisha nyuki wenye ukosefu wa uvumilivu watatoka., Kujua adui aliye ndani ya mfumo.

Ndio maana almost waliojitokeza walikuwa New Characters na wengine ni unknown person.

Hiyo ndio inaitwa Night Walk, kuwa invisible kukamilisha operation
 
Wengine hao siwezi kutia neno maana sijawafuatilia vizuri.
Kabla na baada ya October 29 nilizungumzia issue ya captain Tesha. Iko hivi:
Captain Tesha ni project ya Wakristo hasa Ufufuo na Uzima.
Yule ni polisi jamii, a.k.a sungusungu wakamshonea nembo ya jwtz na kuweka kwenye kofia ya mtumba. Mashati ya jeshi mtumbani yako mengi, na nchi za watu yanauzwa kwa wazi tu hata Raia anauziwa.
Kijana akapewa risala asome huku akirekodiwa.
Main purpose ilikuwa jeshi lipewe mshtuko lione nchi haiko salama wampoke Samia nchi.
Then baadaye utaratibu mpya ukitangazwa ndani ya chama kumteua mgombea Gwajima apenye.
surely 100% ya machafuko ya October 29 kanisa la Tanzania ndilo liliratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…