Je, CCM ilisajiliwa UPYA ulipoasisiwa mfumo wa Vyama vingi Julai 1992?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!

Swali hili nimekuwa nikujiuliza kitambo sasa kuwa, Ulipoasisiwa mfumo wa Vyama vingi July 1, mwaka 1992, CCM iliyokuwa chama pekee katika mfumo wa chama kimoja, ilipata usajili UPYA na kujitenga na kujishikamanisha na system?

Maana ukikiangalia chama hiki Kwa nje ni kama chama Cha siasa, lakini Kwa ndani, nionavyo ni zaidi ya hapo.

Wajuzi wa mambo watujuze ikiwa CCM ilipata usajili mpya Ili kuwa sawa na vyama vingine vya siasa, au walifanya Yale mambo ya KINYONGA kujibadili RANGI ilhali ni kinyonga yule yule?

Waonaji katika Ulimwengu Ule, Kila wakikitafuta, kinasoma kitu kingine, tuambieni mlifanyaje fanyaje? Pascal Mayalla

Karibuni🙏
 
Nani alikuwa msajili wa vyama vya siasa 1992?
 
Masjala ya msajili wa vyama vya siasa ina documentation zote ikiwemo orodha ya usajili.
 
CCM haikusajiliwa Upya

Iliendelea kuwepo ikiwa namba 1

Katiba ya CCM ni ya 1977 sawia na ile ya JMT

Karibu sana
Unachosema ni kuwa, msajili wa Vyama vya siasa, Hana document za CCM?

Kwahiyo ni Chama HEWA, invisible 🙃
 
Nambari wanieeeeeee nambari wani ni CCM
RIP CAPT.KOMBA
Hata me naanza kuliona Hilo!!

MAPINDUZI daima!!!

Halafu Kuna watu wanataka kuitoa CCM Kwa Sanduku la kura!!!
 
Kinajiendesha kinyume na taratibu.
Hakijasajiliwa popote chama hiki.
Tumejiumanisha na nchi.

Yaani kupe ana afafhali
 
Mfumo wa vyama vipya ilipoanzishwa mwaka 1992, na kuundwa kwa ofisi ya msajilli wa vyama vya siasa. Vyama vyote viliwasilisha nyaraka za usajili kwa msajili wa vyama vya siasa, na kupokea maelekezo ya kupata usajili na kukabidhiwa kanuni, vigezo, masharti na taratibu za kufuata ili hatimae kupata usajili wa kudumu.

Vyama vyote, ikiwa ni pamoya na CCM vilifuata utaratibu na kupata usajili wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…