Uchaguzi 2020 Je, CCM itaruhusu wanachama wake wachukue fomu za kugombea Urais kama Katiba yao inavyoelekeza?

Uchaguzi 2020 Je, CCM itaruhusu wanachama wake wachukue fomu za kugombea Urais kama Katiba yao inavyoelekeza?

Mkuu kama wewe bado unaendelea na ulozi kwanini usitusaidie kuiroga corona ikaisha ili tuendelee kupata watalii wengi?
Wakifanya hivyo naacha ulozi nafunga kilinge najiunga na CCM kugombea nafasi nyeti.

Jr[emoji769]
 
Ni kawaida sana kwa muovu kuogopa sheria
Ngumu sana, muulze membe. Kuonyesha nia tu unafukuzwa uwanachama. Wanakwambia Ni desturi. Desturi mpaka inavunja katiba. Ni aibu sana CCM kuogopa demokrasia.
 
Chama Cha Maigizo
Ni hatari kwa mkuu wa idara ya propaganda ya chama kikuu cha upinzani kujikita katika thread za kuipaisha CCM
Ndio mana tunaamini CCM itatawala miaka 100, wapinzani wetu wapo bize kutukodolea macho badala ya kujenga saccos yao.
 
Hivi kwanini Rais anasifiwa sana? Kila kitu rais kila kitu rais kuna agenda gani nyuma ya pazia?
Kuganga njaa
Mathayo 4:8-9 ;Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka na kunisujudia.
 
Eti chama kikongwe kushindwa kufuata demokrasia ,mtu achaguliwe kwenye vikao,ukongwe wa
chama wa umri sio maamuzi hovyo kabisa yaani Jiwe na makosa yake ya waziwazi arudi?
Ndiyo hiyo nafasi ni tamu hawezi kuachia hivi hivi
 
wakifata katiba ya chama chao kuna mtu ataandika historia ya kuwa one-term president

Mimi naweza kudiriki kusema kuwa namuelewa Jakaya, naweza hata kutafsiri body lamguage yake kwani nimesoma nae kwa muda mrefu. Ukitafakari hotuba yake aliyoitoa pale Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la IKULU Chamwino alisisitiza sana uamuzi wa kufanya Dodoma kuwa makao makuu kuwa ulifanywa KIDEMOKRASIA na sio na baba wa Taifa peke yake!!! He was trying to insist that maamuzi ndani ya chama chao hayana buda kufanywa kwa kufuata demokarasia. Sasa wale waliomuelewa walimuelewa kuwa alikuwa anasisitiza kuwa chama hakina budi kuonekana kuwa kinafuata demokrasia katika maamuzi yake!! Sasa tungoje tuone huko mbele itakuwaje. Huko mbele si shwari tena!!!
 
Thubutu! Hata wakielewa tu kwamba unafikiria kuchukua fomu watakushukia kama mwewe anavyoshukia kifaranga cha kuku!
Wakifanya hivyo naacha ulozi nafunga kilinge najiunga na CCM kugombea nafasi nyeti.

Jr[emoji769]
 

Hili ni swali tu ndugu zangu na wala halina uhusiano na jambo lolote lile.

Maana tumeanza kuona vyama vingine vya siasa vikiruhusu watia nia kujitokeza na kujitangaza.

Je, CCM nayo itafuata misingi ya demokrasia kama dunia na katiba ya nchi inavyoelekeza?

Thubutuuu!!! mpaka sasa kuna tetesi inasemekana kuwa hiyo nafasi hawaitoi wameamua kumteua huyo huyo aliopo
 
Back
Top Bottom