Je, CCM kama chama tawala kiliridhia na kubariki Mkataba wa Makubaliano na DP World?

Je, CCM kama chama tawala kiliridhia na kubariki Mkataba wa Makubaliano na DP World?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Mkataba wa Makubaliano (Mkataba wa awali) kati ya Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai tayari ulishapata baraka za Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.

Kwa baraka hizo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliingia katika Makubaliano ya awali na kampuni ya DP World (DPW) ya Dubai February 28, 2022.

Mkataba usio na kikomo.jpg
download (1).jpg

Rais Dr. Samia Suluhu Hassan pia ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM

Tetesi ni kwamba leo wabunge wa CCM watakutana chini ya Mwenyekiti wao Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuweka msimamo wa pamoja kwa kikao cha kesho.

Kinachosubiriwa sasa ni azimio la Bunge kupitisha Makubaliano hayo ya awali kitakachofanyika kesho Jumamosi, je tutegemee nini? Watanganyika CCM imetuuza!
 
CCM mnavyohangaika kuuza Bandari zote ili watanzania wakaishi wapi?
 
Samia hawezi kukiokoa hiki Chama kinajifia Natural Death.
 
Nimeuliza tu.

Mwenye majibu anijulishe tafadhali ili tujue cha kufanya ikifika 2025
 
Msimamo ni ndiyooooooooooooo

Paaa Paaa Paaa Paaa paaaa paaa
 
Hivi unaweza uliza msimamo wa CCM kwa Maana ya nini?

Huu ni mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya Uchaguzi 2025

Mwinyi IPTL
mkapa EPA
kikwete ESCROW
Na hii hapa mwenye akili utaelewa

CCM CHAMA KWANZA TAIFA BADAE
 
Sasa ni wakati wa kurudiwa mgombea binafsi .
2. Kuikataa ccm na matawi yske
3. Kama imeshindwa kusimamia bandari haiwezi kuongoza nchi
3. Masuala ya muungsno yabakie ccm wananchi waukatae.
 
CCM IMEJAWA NA VILAZA.

Kinachoniumiza sana ni KUONA WAJINGA wanawatawala na kuingiza WEREVU.
 
Back
Top Bottom