Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

wajua upinzania ulikuwa na bado wanayonafasi yakuonyesha mfano katika halimashauri na majiji wanayoongoza.... lakini je wanafanya hivyo kuja kuthibitisha au kulalamika kuhusu sisiemu kuwavuruga....??
 

hauko cdm wewe!
 

Pascal,

Hili ni bandiko murua kwa sababu linafikirisha. Kwa ufupi, jibu la swali lako ni hapana! Itakuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko Chadema kushinda uchaguzi wa 2020 katika hali ya maringira kama yalivyo kwa sasa . Na hapa sizungumzii katiba wala tume ya uchaguzi. Nazungumzia Chadema kukosa agenda na dira mbadala; hivi ndivyo vichocheo vikuu kwa wapiga kura kuchagua chama mbadala,

Ni kweli CCM imeshindwa kuongoza nchi kuelekea maendeleo endelevu katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii. Na haya ni matokeo ya CCM kukosa uongozi wenye maono pamoja na itikadi/dira ya maendeleo endelevu. Huu udhaifu wa CCM umejengeka kuwa utamaduni kwa hiyo Watanzania wasitarajie “kuona mwanga mwisho wa tanuru” chini ya utawala wa CCM!

Lakini ni lazima ieleweke kuwa udhaifu wa CCM pekee automatically hauipi Chadema unafuu (leverage) wa kisiasa utaoiwezesha kushinda uchaguzi. Ni lazima Chadema watafsiri itikadi yao katika sera mbadala ya zile za CCM na kuzieleza, kuzifafanua na kuzieneza (articulate and propagate) kwa wananchi. Na hiyo pekee haitoshi. Ni lazima Chadema waonyeshe kwa mifano halisi tofauti zao za kimsingi kimuonekano na kimwelekeo na CCM ni zipi. Kwa sasa hazionekani!

Mifano ya udhaifu wa CCM ni mingi. Nitaelezea miwili kwa leo.

Kwanza, chini ya utawala wa CCM elimu ya taifa imekuwa shaghalabaghala. Kuna mfumo wa kibaguzi wa utoaji elimu kulingana na matabaka ya watu na hakuna sheria inayoelekeza kutengwa kwa bajeti ya elimu kulingana na pato la taifa ili kuwe na uhakika wa kugharamia elimu inavyopaswa. Matokeo yake ni kutelekezwa kwa sekta ya elimu nchini na hivyo kushidwa ku-“maximize the intellectual potential of every Tanzanian child”; kitu ambacho kinapaswa kuwa lengo kuu la utoaji elimu katika karne ya 21. Je, Chadema wana sera gani mbadala ya elimu inayorekebisha udhaifu huu wa CCM? Kwa vile hatujaisikia ni kwamba haipo. Au hawataki tuifahamu na ilhali wanataka kura zetu?

Na pili, huko bungeni wabunge wamekuwa wanalia fedha za maendeleo ni kiduchu. Lakini chanzo kikubwa cha mapato ya serikali ni kodi. Na serikali ya CCM inakusanya chini ya asilimia 11% ya pato la taifa (GDP) kama mapato ya kodi. (Na huu ndio ukomo wa uwezo wake!). Wataalam wa uchumi wanatuambia kuwa serikali inayotegemea kujiendesha kwa mapato ya kodi (kama ya Tanzania) inapaswa ikusanye angalau 25% ya GDP kama kodi ili iweke kupanga bajeti zitakazotekelezeka. (Takwimu zinaonyesha nchi nyingi za Kiafrika zinakunyanya zaidi ya 20% ya GDP kama mapato ya kodi na za Ulaya zinakusanya wastani wa 40%). Serikali ya CCM inafanya vibaya katika eneo hili kwa sababu imeshindwa kurasimisha sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi nchini ili ziwe vyanzo vya mapato ya serikali. Je, Chadema wana sera yoyote inayorekebisha udhaifu kuu wa CCM? Mbona hatujaisikia?

Kuna mambo mawili makubwa ambayo Chadema inapaswa kurekebisha haraka ili iwe angalau na matumaini ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2020 hasa katika kuongeza idadi ya wabunge na madiwani.

Kwanza, waachane na tabia ya kulalamika. Kwa mfano, kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa hakupaswi kufanywe kisingizio cha kutokuikosoa serikali na kupeleka ujumbe wa sera mbadala kwa wananchi. Kuna njia njingi kinachotakiwa ni kujipanga tu. Kwa mfano, kunapaswa kuwe na baraza mawaziri kivuli (functional shadow cabinet) linalofanya kazi muda wote sambamba na serikali iliyoko madarakani. Hawa mawaziri kivuli ni wabunge wanaolipwa na pia vyama vyao vina ruzuku. Kwa sasa tunamsikia waziri kivuli mmoja tu: waziri kivuli wa sheria. Wengine wako wapi?

Na suala la pili ni kwamba kama CCM ilivyoshindwa kuongoza nchi kuelekea maendeleo endelevu, ndivyo hivyo hivyo uongozi wa juu wa Chadema (hasa mwenyekiti) ulivyoshindwa kukiongoza chama katika kukabiliana na changamoto za udhaifu wa CCM na hivyo kushindwa kuongoza chama kuelekea mafanio ya uhakika wa ushindi pamoja na kuwa chama chenye nguvu ndani ya bunge. Uongozi wa juu wa Chadema unapaswa ubadilishwe mara moja. Kumbuka kushindwa katika mazingira endelevu ni utamaduni wa kushindwa.
 

Ninakupinga mpaka asubuhi,SHEMEJI hebu for once acheni kufikiri kwamba wanawake hawawezi.!Hivi hawa akina Mama wakija kuonyesha uwezo wao kuliko mtoto wa Magembe utakuja kutomba radhi??

Mlisema waweke akina Mama wamaweka unataka CDM wafanye nini??Ninavyojua ni kwamba UKADA pia unao SHEMEJI yangu,na ukiangalia na ile Bendera pale kwa Baba Mkwe mh!

Shemeji yangu mpendwa ni nani alikuleta duniani kama siyo Mama?Je bila Mama ungekuwepo leo??Kuna akina Bibi Titi,Bibi Matola,hawa walikuwa wanajua kusoma na kuandika tu,lakini waliweza kufanya makubwa enzi za kutafuta Uhuru wetu,unataka kutuambia hawakufanya majukumu yao kama akina Sozigwa,Kawawa na wengineo??

Tumewaona waliolelewa na JKN ni waovu kupita maelezo,wala rushwa,mafisadi wakubwa,majangili na bado system inawaona ni WATUKUFU je si wanawake??

CCM ilimuacha Mbunge mzuri sana SHyrose Bhanji ikamteuea mwenye degree ya Sheria aliyosoma mwaka mmoja,sifahamu kama sheria ulisoma mwaka mmoja lakini aliweza kusoma mwaka mmoja na ana cheti.!

Tumemuona yule wa CUF ambaye hata kiinglish alishindwa kujieleza lakini ndiye CCM waliomchagua?

Unadhani hata wangempeleka Malaika CDM wangeweza kumpitisha??Ujue walioteua weak candidates kama wapo basi ni WABUNGE TOKA CCM.
 
Unaongozwa na unafiki katika Uzi huu uliouandika, na unafiki ukizidi huondoa busara,hekima na akili Bali huelekea matamanio ya moyo wako,Pasco umekuwa kigeugeu sana ndio maana hata mheshimiwa Rais alikupuuza akasema Mayala ni nini?usiache jina lako likutese kutumikia tumbo,Naomba nikiri ulikuwa ni mmoja kati ya waandishi wa habari niliowapenda sana hata kipindi cha uanzishwaji wa TVT nilifuatilia sana vipindi vyako. Ila njaa imeingia kwako na umekuwa mwanasiasa. Naomba nikiri mie sio mwanachama wa chama chochote lakini sala yangu ni ccm iondoke madarakani pasipo hilo kutendeka hata raisi awe nani kupitia ccm nchi hii haitofanikiwa. Katika ulimwengu wa roho kuna maagano yamefunga mafanikio ya nchi hii kupitia ccm, Swala la chama kukomaa ni ujinga usio na mashiko kuwadanganya watu ni ccm tu ndio wanaweza kuongoza nchi, hata Act wazalendo wakipewa nchi Leo wataiongoza vizuri sana, nchi inaongozwa na katiba na mfumo ndio maana hata Dr Magu hujawahi kuwa raisi lakini sasa hivi anaongoza tena kwa namna ya tofauti na mlivyozoea, ila tutoe ujinga wakuaminishana kuwa bila ccm nchi itakwama. Tuipende Tanzania zaidi kuliko vyama na njaa zetu na kwa hakika bila kuitoa ccm madarakani hakika tutabaki kuimba nchi hii ni tajiri huku tunatembeza bakuli kuomba misaada hata kwa nchi zilizokuwa na vita na matatizo zimejipanga zikasimama. Kuwa mzalendo Tanzania kwanza
 
Kimsing tatizo la CDM kwa sasa ni mbowe, kwa ule upuuzi wa wale wadada wa EALA kuwa ndo krim ya CDM ni ishara tosha kuwa mbowe amefika kikomo cha kichwa chake.

Nilishasema mara kadhaa sasa ni wakati wa CDM kuongozwa na Tundu Lissu kwa ajili ya kujiandaa kuwa raisi wa Tz 2020, nje ya hapo tutaendelea kusoma numbers
 
Kimsingi kuna maeneo nakuunga mkono bwana Paskal na kuna sehemu natofautiana na ww. Kitendo cha cdm kumchukua EL kuwa kiongozi wao na mgombea wao wa urais wakati hakuwa anaishi itikadi ya chama hicho ule ulikuwa ni udhaifu wa hali ya juu sana. Kitendo kile kiliniacha na shaka kubwa kuhusu uwezo wao wa kuongoza nchi.

Ila iwapo kitateuliwa kuongoza nchi hilo nadhani wataweza lakini sina hakika kama wataiongoza kwa mafanikio. Iwapo ccm imeweza muda wote huo tena kwa mafanikio hafifu ni kipi chama kingine kitashindwa? Nijuavyo mimi sehemu kubwa ya nchi inaendeshwa na wataalamu na kazi ya chama cha siasa ni kusimamia sera tu. Hadi sasa wataalamu wapo hivyo ni swala la kuwa flexible tu kushirikiana na wataalamu kuendesha nchi.
 
as·sume
əˈso͞om/
verb
  1. 1.
    suppose to be the case, without proof.
    "you're afraid of what people are going to assume about me"
    synonyms: presume, suppose, take it (as given), take for granted, take as read, conjecture, surmise, conclude, deduce, infer, reckon, reason, think, fancy, believe, understand, gather, figure
    "I assumed he wanted me to keep the book"
  2. 2.
    take or begin to have (power or responsibility).
    "he assumed full responsibility for all organizational work"
    synonyms: accept, shoulder, bear, undertake, take on/up, manage, handle, deal with
    "they are to assume more responsibility"
    Mkuu nafikiri unaelewa maana ya neno assume


 
Swali kwako mwenyewe: Are you a serious, able, capable, credible and mature enough ANALYST to provide a sound take on this topic? Mkuu Pascal, hilo unalouliza hapa sio swali wala suala sahihi la mada kuu iliyo mezani leo hii nchini. Swali lenyewe ni: je, Tanzania na Watanzania wanao uelewa, uwezo, uadilifu, utimilifu na ukomavu wa kusimamia na kuchukuana na siasa za vyama vingi? Usipoteze muda na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kabla hilo swali halijajibiwa. Na bado sijaona hasa kwa nini umevutiwa kuichagua CHADEMA kama lengo (focus) la bandiko. Hao hawana chao; hata waje kama malaika Gabrieli. Huhitaji kufahamishwa kuwa mazingira yaliyopo nchini hayaruhusu anasa ya mjadala "feki" kama huu unaotaka kuutumia kuchokoza "makada" hapa. Labda kama lengo pekee ni utani na "makamanda".

Bila shaka wewe unao uwezo mzuri sana wa kutambua "genius" aliyotumia Mwalimu JKN kuisuka Tanzania na CCM kiasi cha kuacha "wenye ndoto zao" wakiendelea bila kuchoka kuinyatia CCM kwa nyuma kama mafisi wakijiaminisha kuwa mkono unakaribia kumdondoka binadamu waambulie ulaji! Usifikiri waliopania kumfanya JKN "mtakatifu" wamekurupuka tu. He was a "real genius" kwa namna yake; utake usitake. Atakayekuja na mkakati wa kuufumua huo "msuko" alioudarizi Mwl. JKN ndiye atakayetuwezesha kujadili hicho unachokusudia hapa - that is if you, Sir, yourself are genuine and credible.
 
Nimekusoma comrade
 
Ukichukua mda kuangalia utagundua kuwa Seriousness, abilities and capabilities. Hivi vitu vipo ndani ya CHADEMA,na kinauwezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, isipokuwa wapinzani wao CCM wamechukua hatua zifuatazo kuzuia jambo hilo lisitokee:-
  1. Baada ya kuona mwamko wa wananchi kwenye uchaguzi 2015 na kupungua kwa kura za ushindi kwa asilimia kubwa kulinganisha na chaguzi zilizopita waliamua kudhibiti undeshaji wa shughuri za kisiasa kwa wapinzani wao.
  2. kutoa makatazo bila kujari haki za kiraia,kisheria na kikatiba kuzuia BUNGE LIVE MIKUTANO YA HADHARA na kudhibiti uhuru wa kutoa mawazo kupitia mitandao ya kijamii,vitisho, na mambo mengi tu unayoyaona sasa sababu kubwa ni jinsi CCM ilivyonyanyasika 2015.
  3. CCM hawana uhakika kama wana mda mrefu kusalia madarakani endapo wataacha mambo hayo no 2 yafanyike kwa uhuru, hofu ni kubwa kwani wanajua mafanikio ya CHADEMA yalitokana na kukitangaza chama chao kwa mda wa miaka 5 mfululizo baada ya uchaguzi 2010
  4. PASCO kumbuka kuwa waanasiasa huwa hawaendeshi shughuri za kila siku za serikali wao huwa ni nadharia tu ya kiutawala iliyozoeleka kuweka wawakilishi wa wananchi kwenye utawala wa nchi lakini ukiondoa wanasiasa wote serikalini ukamteua pengine jaji mkuu awe mkuu wa nchi kwa kushirikiana na watendaji wengine wa serikari huenda nchi ikatawaliwa na kuendeshwa vizuri kuliko pengine hata uwepo wa wanasiasa serikalini. Hoja yangu ni kuwa hata bila wanasiasa watumishi wa umma wapo na ndio huwa watendaji.
  5. chama chochote cha siasa kinaweza kutawala bila kujari weredi,wa watu waliomo ndani ya vyama hivyo. kumbuka wakati tunapata uhuru nchi ilikuwa na watu wa aina gani na kwa nini waliweza kuiongoza nchi.KUONGOZA NCHI HAINAGA UZOEFU, BALI NI MAONO BUSARA,HEKIMA NA UTU.hata std 7 anaweza( ref;Zuma,Tramp)
 
w

wewe ebu acha kuongea PUMBA mkuu.....ni wananchi wepi hao wa kuingia barabarani????wangekuwa wanataka kuingia BARABARANI wangesihakuwa wameingia siku nyingi sana.........Ila sisi wananchi tunajiuliza tuingie barabarani kisa nani????
Ndo maana nikasema mpaka siku wananchi wawe aggressive kma wakenya!!! Maana zanzibar waliweza ila shida ni udogo wa nchi yao ila kma spirit ile ya waxenji ingekuwa kwa wabara tungekuwa tushaitoa ccm.

Shida wananchi watz bado waoga hawapo agressive kma congo ama kenya lasihivyo tungeongea mengine hapa

Hoja yangu ni kwamba je hyo system au kitengo kinachoamua rais ikitokea wananchi wameingia barabarani kma kenya 2002 watazuia?????
 
Chadema ukiipima tu kwa wabunge ilio nayo madiwani na ma meya waweza kabisa ku predikti wakiwa na serikali kutatokea nini. Hatuwaoni wakiwa na wananchi kwenye habari za maendeleo ama kwa kubuni wao au kwa kuendeleza walio yakuta. Wamekuwa watu wa kutafuta lawama tuu.

Itizame Dar, iko chini ya upinzani hatuoni wakija na majibu kwenye matatizo ya miundombinu. Zaidi wanatafuta walipoharibu ccm ili wapige kelele kuliharibiwa. Sasa imagine ndio wana nchi nzima si ndio itakuwa balaa.

Waoneshe mfano kwenye maeneo wanayoyasimamia ili watu tuone tofauti yao na CCM kwa maana ya mabadiliko kimaendeleo. Sio kilawama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…