Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?

Umepiga penyewe mkuu....inahtaji uwe empty headed (unintelligent and foolish) kuwachagua hao wahuni from North
Duh north?? Huku kwetu kalinzi tunaisupport chadema ingawa sio wa kaskazini!!! Je majiji makubwa yote kasoro mwanza mbona yapo chini ya upinzani hasa chadema je huko kuna wakaskazini pia???
 
Mr Mayala kajitahidi kuweka Hoja zake mezani kama Mwanajukwaa Huru Katika Jukwaa Letu Pendwa la Siasa, Were We Dare To talk Openly.
Kwa mantiki ya Andiko lake anapaswa kujibiwa kwa Hoja na si kumwambia ake Kimya kama ndivyo hakuna Sababu ya Kuwa na Jukwaa hili kila mtu angekaa na hoja yake moyoni mwake, na kumwambia akae kimya au hana sababu ya kutueleza anachofikiri ni Dalili za Udiktekta.
Nimesoma na kukuelewa kwa Upana Mayala,
Nishauri yafuatayo Kwa CHADEMA
1.waboreshe mfumo wa mawasiliano ndani ya chama.
2.wawe na semina elekezi kwa Viongozi na wawakilishi wa wananchi (w/viti Mitaa,Madiwani na Wabunge)
3.Migogoro ya Ndani itatuliwe.
4.Ruzuku ipelekwe majimboni ili shughuli za Chama zitekelezeke.
5.Ilani ya Chama itekelezwe kwa Vitendo kwenye Majimbo na Halmashauri wanazoziongoza.
6.Wawaandae Vijana watakaokipokea Chama (Leader Materials) wakuzwe na ikiwezekana waanzishe chuo Cha uongozi ili kuwafua.
7.Waboreshe mifumo ya ulinzi.
8.Wapeleke Vifaa vya uenezi kwenye Maeneo Husika Kadi, Bendera N.k
9.Kuwe na uwazi katika Rasilimali za Chama na ziwanufaishe wote kwa Usawa.
Naamini Wananchi wanahitaji mabadiliko ya Kiuchumi,Kisiasa na Kijamii.
Nafikiri Waanze Majimboni kuwa na Wabunge Wengi kwanza walishike Bunge
Points za msingi sana hizo. Text derives to katibu Mkuu Mashinji.
 
Yote uliyosema kama ushauri kwa chadema ni sahihi lkn cha kuingezea ni kwamba.
Chadema inatakiwa ifanye tafiti sehemu mbalimbali duniani ili kujifunza mengi kabla haijatoa semina elekezi kwa viongozi wake na haijafundisha vijana kuadopt mfumo wa chama.

Baada ya ku install system wafanye evaluation performance ya kile walichoki install na kuamua on time whether kuboresha au kubadilisha as long wata access efficiency
 
Duh north?? Huku kwetu kalinzi tunaisupport chadema ingawa sio wa kaskazini!!! Je majiji makubwa yote kasoro mwanza mbona yapo chini ya upinzani hasa chadema je huko kuna wakaskazini pia???
Fubusa asingepigwa chini kama hiyo support ingekuwepo.
 
Mkuu kabla ya kujibu hoja zako naomba ujibu zangu nilizouliza........ je wananchi wakiamua kuipa kura upinzani afu wakaingia barabarani kudai ushindi wao je system watazuia???

Mkuu hebu acha kuongea nadharia basi..Wananchi wa nchi gani hao? Tanzania? Watanzania hawajalelewa katika utamaduni huo....Na hata kama itatokea wafanye hivyo..Ni baada ya kukiamini chama kilicho makini na kuamini kuwa kinaweza kuwaletea maisha bora......na chama hicho sio CHADEMA kwa sasa ...kwa sababu CHADEMA imeshindwa kushawishi wananchi..achilia mbali system....ndio maana haitakaa ipewe kura za kuchukua dola....kwa lugha nyingine system ipo kulinda maslahi ya nchi.....na maslahi ya nchi lazima yalindwe kwa namna yoyote ile.

Anyway conclusion yangu ni whether upinzani utakomaa or not ccm haitowahi kutoka as long as dola haitofautishwi na chama kwa mfumo wa katiba hii ya sasa......... trust me huko TISS au jeshini kuna watu wamekunywa maji ya bendera kuilinda ccm kwa gharama yoyote je hao unafkiri hata chadema ikisimamisha malaika watamuachia eti kwa kuwa wamekomaaa?????
Unadhani katiba mpya au tume huru inakuja kama zawadi?
 
Pasko tegemea matusi, ila wanaokutukana ni mashahidi walio hai wa failure ya chadema
Naamini hata wao ukweli wanaujua ..

Chadema hakina uwezo wa kuongoza nchi .. Chadema ni Saccos ya watu flani flani ... Watuwezi kuwakabidhi nchi kwa wapiga dili
 
Pascal,

Hili ni bandiko murua kwa sababu linafikirisha. Kwa ufupi, jibu la swali lako ni hapana! Itakuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko Chadema kushinda uchaguzi wa 2020 katika hali ya maringira kama yalivyo kwa sasa . Na hapa sizungumzii katiba wala tume ya uchaguzi. Nazungumzia Chadema kukosa agenda na dira mbadala; hivi ndivyo vichocheo vikuu kwa wapiga kura kuchagua chama mbadala,

Ni kweli CCM imeshindwa kuongoza nchi kuelekea maendeleo endelevu katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii. Na haya ni matokeo ya CCM kukosa uongozi wenye maono pamoja na itikadi/dira ya maendeleo endelevu. Huu udhaifu wa CCM umejengeka kuwa utamaduni kwa hiyo Watanzania wasitarajie “kuona mwanga mwisho wa tanuru” chini ya utawala wa CCM!

Lakini ni lazima ieleweke kuwa udhaifu wa CCM pekee automatically hauipi Chadema unafuu (leverage) wa kisiasa utaoiwezesha kushinda uchaguzi. Ni lazima Chadema watafsiri itikadi yao katika sera mbadala ya zile za CCM na kuzieleza, kuzifafanua na kuzieneza (articulate and propagate) kwa wananchi. Na hiyo pekee haitoshi. Ni lazima Chadema waonyeshe kwa mifano halisi tofauti zao za kimsingi kimuonekano na kimwelekeo na CCM ni zipi. Kwa sasa hazionekani!

Mifano ya udhaifu wa CCM ni mingi. Nitaelezea miwili kwa leo.

Kwanza, chini ya utawala wa CCM elimu ya taifa imekuwa shaghalabaghala. Kuna mfumo wa kibaguzi wa utoaji elimu kulingana na matabaka ya watu na hakuna sheria inayoelekeza kutengwa kwa bajeti ya elimu kulingana na pato la taifa ili kuwe na uhakika wa kugharamia elimu inavyopaswa. Matokeo yake ni kutelekezwa kwa sekta ya elimu nchini na hivyo kushidwa ku-“maximize the intellectual potential of every Tanzanian child”; kitu ambacho kinapaswa kuwa lengo kuu la utoaji elimu katika karne ya 21. Je, Chadema wana sera gani mbadala ya elimu inayorekebisha udhaifu huu wa CCM? Kwa vile hatujaisikia ni kwamba haipo. Au hawataki tuifahamu na ilhali wanataka kura zetu?

Na pili, huko bungeni wabunge wamekuwa wanalia fedha za maendeleo ni kiduchu. Lakini chanzo kikubwa cha mapato ya serikali ni kodi. Na serikali ya CCM inakusanya chini ya asilimia 11% ya pato la taifa (GDP) kama mapato ya kodi. (Na huu ndio ukomo wa uwezo wake!). Wataalam wa uchumi wanatuambia kuwa serikali inayotegemea kujiendesha kwa mapato ya kodi (kama ya Tanzania) inapaswa ikusanye angalau 25% ya GDP kama kodi ili iweke kupanga bajeti zitakazotekelezeka. (Takwimu zinaonyesha nchi nyingi za Kiafrika zinakunyanya zaidi ya 20% ya GDP kama mapato ya kodi na za Ulaya zinakusanya wastani wa 40%). Serikali ya CCM inafanya vibaya katika eneo hili kwa sababu imeshindwa kurasimisha sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi nchini ili ziwe vyanzo vya mapato ya serikali. Je, Chadema wana sera yoyote inayorekebisha udhaifu kuu wa CCM? Mbona hatujaisikia?

Kuna mambo mawili makubwa ambayo Chadema inapaswa kurekebisha haraka ili iwe angalau na matumaini ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa 2020 hasa katika kuongeza idadi ya wabunge na madiwani.

Kwanza, waachane na tabia ya kulalamika. Kwa mfano, kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa hakupaswi kufanywe kisingizio cha kutokuikosoa serikali na kupeleka ujumbe wa sera mbadala kwa wananchi. Kuna njia njingi kinachotakiwa ni kujipanga tu. Kwa mfano, kunapaswa kuwe na baraza mawaziri kivuli (functional shadow cabinet) linalofanya kazi muda wote sambamba na serikali iliyoko madarakani. Hawa mawaziri kivuli ni wabunge wanaolipwa na pia vyama vyao vina ruzuku. Kwa sasa tunamsikia waziri kivuli mmoja tu: waziri kivuli wa sheria. Wengine wako wapi?
Nduguyangu tambua kuwa mikutano ya siasa ni nyenzo muhimu kwa vyama vya siasa kueleza malengo,sera, mipango na kila kitu. na ndio maana CCM wamekimbilia kuziba huo mlango hayo majukwaa mengine nafasi yake kuwafikia wananchi ni finyu mno.

Na suala la pili ni kwamba kama CCM ilivyoshindwa kuongoza nchi kuelekea maendeleo endelevu, ndivyo hivyo hivyo uongozi wa juu wa Chadema (hasa mwenyekiti) ulivyoshindwa kukiongoza chama katika kukabiliana na changamoto za udhaifu wa CCM na hivyo kushindwa kuongoza chama kuelekea mafanio ya uhakika wa ushindi pamoja na kuwa chama chenye nguvu ndani ya bunge. Uongozi wa juu wa Chadema unapaswa ubadilishwe mara moja. Kumbuka kushindwa katika mazingira endelevu ni utamaduni wa kushindwa.
 
Umeongea mambo ya msingi sana Bwana PASCHALL........to be honest kabsa ni ngumu sana kuiondoa CCM kwa kutegemea aina hii ya UPINZANI....hawa wapinzani wa nchi hii wanasikitisha sana......
Upinzani unaozungumzia mambo ya Shanga bungeni.

Upinzani unaozungumzia maswala ya Bashite kuliko matatizo ya Wananchi.

Upinzani unaoongoza kwa kususa..
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la tathmini kuihusu Chadema, seriousness yake, its abilities and the capabilities. Hivi CHADEMA, inawezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, na hata ikatokea ikashinda, jee inaweza kuendesha nchi?. Is it a Serious Party?, is it Credible?. Is it Muture Enough Opposition, Kuweza Kukabidhiwa Nchi yetu 2020?!.

Maswali haya ni kufuatia tathmini yangu jinsi Chadema inadeal na baadhi ya issues mbalimbali ikiwemo the current one ya uteuzi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la EALA.

Kutawala nchi sio jambo dogo au jambo la mchezo mchezo. Ikulu yetu haipaswi kugaiwa kwa majaribio bali kwa uhakika, tutakaye mkabidhi ikulu yetu ni lazima kwanza atuthibitishie amekomaa, na anawezo, mature enough with the abilities and capabilities, na sio tuu kumpa mtu ikulu yetu kwa kumjaribishia simply kwa sababu tuu CCM imeshindwa hili na lile na baadhi ya watu wameichoka sana CCM!.

CCM inaendelea kuchaguliwa mwaka hadi mwaka, na itaendelea kuchaguliwa sio kwa sababu CCM is the best, au CCM imeweza au inauwezo kivile!, no!. CCM imeshindwa na ilishindwa siku nyingi na inaendelea kushindwa, kwa kufanya madudu mengi tuu lakini bado imekuwa ikiendelea kushinda kwa kuchaguliwa mwaka hadi mwaka kwa mazoea tuu kwa sababu, Tanzania bado hatuna mbadala muafaka wa kuiondoa CCM!.

Yaani Tanzania bado hatuna any serious and a credible opposition party ya kuwapa wapiga kura wa Tanzania a choice to choose from, hivyo CCM kujikuta ikiendelea kuchaguliwa na kushinda kwa ku sail through na upepo wa mazoea, kwa sababu ndio the only one iliyopo!, we have no any serious credible choice to choose from, hivyo we have no choice. Matokeo yake ni CCM inashinda kwa easy ride ya mazoea na itaendelea kushinda na kushinda tena na tena mpaka tutakapo pata a credible opposition such that we'll have a choice to choose from!.

Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.

CHADEMA ndio angalau angalau wameonyesha nia, na kiukweli wakiamua, wanaweza kabisa, ila natatizwa na haya madudu madogo madogo yanayo onyesha all signs za immaturity kwa upande wa Chadema, such that bado ni chama ambacho hakijaonyesha ukomavu wa kutosha enough to convince Tatanzanians kuikabidhi ikulu yetu comes 2020, waipige chini CCM na kuikabidhi Chadema Ikulu yetu ya Magogoni.

Jee kwa maoni yako, unaiona Chadema as a credible, serious opposition, iliyokomaa na kuwa mature enough with the ability and credibility ya kukabidhiwa ikulu yetu 2020?.

Kwa upande wangu, honestly, I don't think, ila kabla sijasema why I don't think and what should we do, naomba kupata mawazo yako, assuming uchaguzi wa Tanzania utaendeshwa kwa uhuru na haki, na chama kitakacho shinda kimeshinda kwa haki, Jee Chadema hata kikishinda, kinauwezo?. Kimeonyesha uwezo wa utayari wa kutawala nchi endapo kitashinda uchaguzi 2020?. Ila kabla hata hakijashinda huo uchaguzi wa 2020, kwa Chadema hii tunayoiona sasa, jee inao huo uwezo wa kushinda?.

Nawatakia Furahi Dai Njema.
Paskali.
Rejea.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - jamiiforums.com
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...
Kuelekea 2020: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2020: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2020, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi ...
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...
Watanzania ni ignorants au tumelogwa?

No Way. Chadema hawawezi kuaminiwa kupewa Nchi - sio credible opposition. Kuna nepotism ya hali ya Juu na Ukanda, watu hupewa ubunge wa viti maalum kwa kuwa walikuwa wasaidizi wa mwenyekiti au wanajuana na mwenyekiti (HILI NI LA UHAKIKA JAPO KUNA WATU WATATOA POVU HUMU)...... Kiufupi, chadema bado hakijawa na hadhi ya kuongoza dola, ni chama mediocre. Wasubiri Hadi Mwisho wa Enzi
 
Kama Chadema ilimuita yule jamaa yako fisadi lakini alipohamia kwao akageuzwa kuwa jembe tena bila ridhaa ya wanachama sitegemei chama hiki kiwe serious kupewa nchi.
Bado kuna maswali mengi na changamoto kedekede kwa CHADEMA, nahisi wanajiona kama kampuni zaidi kuliko chama, kweli hakijakomaa, na kianze na katiba yao kuwa na mwenyekiti wa kudumu, kisipokee waliochafuka toka vyama pinzani, kiwe na vyanzo vya mapato na hata matumizi yasiwe kwa kuangalia sura ya mtu, mwisho viongozi waamuwe kama wanasiasa au wafanyabiashara..
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la tathmini kuihusu Chadema, seriousness yake, its abilities and the capabilities. Hivi CHADEMA, inawezo wa kushinda uchaguzi wa 2020?, na hata ikatokea ikashinda, jee inaweza kuendesha nchi?. Is it a Serious Party?, is it Credible?. Is it Muture Enough Opposition, Kuweza Kukabidhiwa Nchi yetu 2020?!.

Maswali haya ni kufuatia tathmini yangu jinsi Chadema inadeal na baadhi ya issues mbalimbali ikiwemo the current one ya uteuzi wa wawakilishi wake kwenye Bunge la EALA.

Kutawala nchi sio jambo dogo au jambo la mchezo mchezo. Ikulu yetu haipaswi kugaiwa kwa majaribio bali kwa uhakika, tutakaye mkabidhi ikulu yetu ni lazima kwanza atuthibitishie amekomaa, na anawezo, mature enough with the abilities and capabilities, na sio tuu kumpa mtu ikulu yetu kwa kumjaribishia simply kwa sababu tuu CCM imeshindwa hili na lile na baadhi ya watu wameichoka sana CCM!.

CCM inaendelea kuchaguliwa mwaka hadi mwaka, na itaendelea kuchaguliwa sio kwa sababu CCM is the best, au CCM imeweza au inauwezo kivile!, no!. CCM imeshindwa na ilishindwa siku nyingi na inaendelea kushindwa, kwa kufanya madudu mengi tuu lakini bado imekuwa ikiendelea kushinda kwa kuchaguliwa mwaka hadi mwaka kwa mazoea tuu kwa sababu, Tanzania bado hatuna mbadala muafaka wa kuiondoa CCM!.

Yaani Tanzania bado hatuna any serious and a credible opposition party ya kuwapa wapiga kura wa Tanzania a choice to choose from, hivyo CCM kujikuta ikiendelea kuchaguliwa na kushinda kwa ku sail through na upepo wa mazoea, kwa sababu ndio the only one iliyopo!, we have no any serious credible choice to choose from, hivyo we have no choice. Matokeo yake ni CCM inashinda kwa easy ride ya mazoea na itaendelea kushinda na kushinda tena na tena mpaka tutakapo pata a credible opposition such that we'll have a choice to choose from!.

Kwa Zanzibar hakuna ubishi kuhusu uwezo wa CUF as a credible opposition kuweza kutawala Zanzibar, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara, bado kabisa hatuna any serious and a credible opposition ya kuiondoa CCM na kuikabidhi Ikulu yetu.

CHADEMA ndio angalau angalau wameonyesha nia, na kiukweli wakiamua, wanaweza kabisa, ila natatizwa na haya madudu madogo madogo yanayo onyesha all signs za immaturity kwa upande wa Chadema, such that bado ni chama ambacho hakijaonyesha ukomavu wa kutosha enough to convince Tatanzanians kuikabidhi ikulu yetu comes 2020, waipige chini CCM na kuikabidhi Chadema Ikulu yetu ya Magogoni.

Jee kwa maoni yako, unaiona Chadema as a credible, serious opposition, iliyokomaa na kuwa mature enough with the ability and credibility ya kukabidhiwa ikulu yetu 2020?.

Kwa upande wangu, honestly, I don't think, ila kabla sijasema why I don't think and what should we do, naomba kupata mawazo yako, assuming uchaguzi wa Tanzania utaendeshwa kwa uhuru na haki, na chama kitakacho shinda kimeshinda kwa haki, Jee Chadema hata kikishinda, kinauwezo?. Kimeonyesha uwezo wa utayari wa kutawala nchi endapo kitashinda uchaguzi 2020?. Ila kabla hata hakijashinda huo uchaguzi wa 2020, kwa Chadema hii tunayoiona sasa, jee inao huo uwezo wa kushinda?.

Nawatakia Furahi Dai Njema.
Paskali.
Rejea.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - jamiiforums.com
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 | Page 7 ...
Kuelekea 2020: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2020: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2020, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi ...
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision ...
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye ...
Watanzania ni ignorants au tumelogwa?

Mkuu Paschali

Salute, and welcome back on board.

Comparatively, CCM and Chadema trustworthiness measured on credibility, dependability and confirmability components point out that CCM excels against CHADEMA by far margins. This is a bitter pill. But a very solid fact.

I'm glad you've been consistently authoring and simulating various models attempting to draw CHADEMA next to CCM. Nevertheless reading through your informative articles, it remain clear that the later, despite her extensive drawback in design, coordination and delivery of her election manifesto, it is highly organized system. Hence illustrates exemplary trustworthiness.

If CHADEMA were to restore her trustworthiness to compete with the old defunct CCM, it has to focus on subtle yet critical constitutional changes which are claimed to favour CCM. But reflecting on what, why and how CHADEMA makes internal decisions, I repeat: reflecting on CHADEMA processes of making internal decisions and its short, mid and long term implications, I strongly feel that CHADEMA isn't ready to rule this resource-rich yet very poor country.

I submit.
 
You have touched everything that Magufuli and his stooges would like to hear. My advice to you is to continue doing what you are doing and, very soon, your name will be mentioned in the coming teuzi.
 
Ukweli Chadema mwanzo niliona wanaweza ama wanatosha kuongoza nchini, lakini baada yakitendo chao cha kumleta Lowasa kugombea urais huku miaka yote wametuimbia nifisadi binafsi naona hapana.

Pili kuna mamilioni walipewa na sabondo kwa ajili ya visima pamoja na maji nayo yakayeyuka kimya mpaka leo.hivyo inanifanya nisiwaamini pia.

Siasa zao za sasa hivi ndo zimekua za matukio hata sidhani kama zitamsaidia mtu wa kijijini hivyo tupe muda labda miaka 20 uko.
 
Serikali hiyo itakuwa hivi:

Rais:Lowassa au Sumaye
Wazuri Mkuu :Aikael mbowe

Speaker :tundu lisu
Naibu spika :mnyika
Makamu Wa rais :from Zanzibar
Mawaziri
1.halima mdee:
2.waziri Wa habari :Sugu
3.waziri Wa sheria na katiba?
4.waziri Afya ?
5.waziri Wa mambo ya ndani:lema
Nk

Sasa Pima uwezo Wa hao then njoo na comment tuone kama wanaweza kupewa nchi
Duuuh!Naogopa![emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Me nazani ili swali watu watabishana mpaka asubuhi ila na jaribu kujiuliza maswali kazaa nahisi yanaweza kutupa njia?
chama kinachopewa nchi kina kazi gani?
kwani chama kinaenda kufanya kila kitu chenyewe?
Nadhani tutachelewa sana kama tunataka kuona kama vile chama ndo kitaenda kuwa jeshi chama kitaenda kuwa dr na kila kitu,na hiki ndo kitu ambacho ccm wanawa aminisha watu!!
NCHI INAENDESHWA NA WATALAM WAKISIMAMIWA NA SERIKARI ILIYO CHINI YA CHAMA
Tunahitaji tufike sehemu tuwe na kiongozi atae ruhusu wataalamu wa fani mbali mbali kuisaidia nchi kwa taaluma zao na si nchi iendeshwe kwa porojo za wana siasa kama tunavyo fanya sasa na kama atutapata mtu wa hivyo tanzania maendeleo kwetu ni ndoto,na sikulazimishi kuamiani!!
Niliambiwa nisipende kusikiliza maneno na ushauri wa mwendawazimu.Sorry!
 
Back
Top Bottom