Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Pole sana Mpwa
 
Pale ni muda ambao una surrender halafu unaona kweli duniani hakuna inshu yaani kama ni mali umeacha unaona hazina maana nilikuwa nahangaikia za nini yaani hata upewe kalamu uambiwe andika wosia unapuuzia tu kama kusema Aahrk watajuana wao huko atakaepata apate mi sina haja nazo hazina faida yoyote.Unaweza ku assume hata wewe very simple.
 
Mimi ndio maana mali zangu nyingi anazijua mke wangu na watoto wNgu tu hata pale napoficha nyaraka zangu.
 
Dah mkuu pole sana aisee hayo maumivu yasikie tu dah yani navaa viatu vyako vinanipwaya yani nimeanzisha huu uzi ila sikutegemea kupata simulizi za kuhuzunisha kama hizi. Pole mkuu mungu akutie nguvu. Ndio maana sijakuona ukipost wala kukoment muda mrefu ID yako naijua sana hapa jamvini.
 
Wakati namuuguza akiwa isolation room KCMC kutokana na hali mbaya ya Uviko mwaka jana nilimfuata daktari nikiwa na hofu kubwa na kumuuliza daktari vipi hali ya mgonjwa? Doctor alinipa moyo na kuniambia twende umuone ht kwa umbali, ndipo daktari aliniambia nimfuate na nilipofika karibu na mlango aliniambia simama hapa na kumfuta akamwambia mwanao anakusalimia hebu mpungie mkono aamini kwamba unaendelea vizuri. Aliinuka na kunipungia mkono bila kusema chochote. Nilipata nguvu ya kuendelea kuzisaka dawa nilizoandikiwa na Daktari angalao niokoe roho yake, lakini punde tu baada ya kuzipata zile dawa nilirudi haraka sana ili nimkabidhi Daktari lakini Madtari walikua bize sana ndipo akili ikanijia hebu jisogeze bila kujali Sheria zilizowekwa kuzuia watu kuingia eneo la wagonjwa wa Uviko 19 kuona anaendeleaje,,, nilikiona kitanda kiko wazi hakuna mtu. Akili haikuwa tena yangu coz Kila nesi au daktari niliyemuona mbele yangu nilimuuliza simuoni baba yangu kulikoni ndipo mmoja wao akaniambia lisaa limoja lililopita hali ilibadilika ghafla na umauti ukamkuta. Ndipo nkakumbuka km vile alinipungia mkono kuniaga. RIP Daddy.
 
Wengine hawapati nafasi ya kuuona mwisho wao hustukia tu wamekufa na hawapo duniani. Tafakuri kifo cha maunda zoro au profesa ngowi vifo vya hivi karibuni kabisa vya hawa watu maarufu. Hawakujua kwamba safari zao kwa magari yao ndio safari zao za milele duniani.
 
Pole sana mkuu,Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu unachopitia.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana
 
Poleni Sana mpendwa
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]inauma sana

Pole sana,upo katika kipindi kigumu[emoji24]
 
Pole sana ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…