Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Mimi ni Mtu wa Afya Nimeshuhudia Mara nyingi mtu akikata Roho mbele yangu.

1..Nikiwa wodi ya wanawake mwaka 2018 kuna Client aliugua Sana Kwa Muda mrefu na Kiutaaramu Tukiweza kujua Huyu ni ngumu kutoboa Labda Mungu Tu..siku nimeingia Night nakuta client ana Furaha Tofauti na Siku zote aisee kufika saa nane Usiku Tayari Nimeshapeleka mwochwali.

2.Huyu alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha sita ameanguka kwenye Chumba cha mtihani wa Taifa kaja Kituo cha Afya chetu tukaanza Huduma za Kwanza Faster Sana ..Ila Hapa Napo kutoboa Tulihisi ngumu Kwa watu wa Afya wanaelewa hii Baada ya Kuhakikisha fluid kama sita za IV fluconazole nimezitembeza nikasema ngoja nikanywe chai kurudi client ananiambia naomba tuombe alikata Moto mbele yangu huyu Nilimfumba macho na mdomo mwenyewe Ila niliumia Sana Hasa dogo Amepotea ndoto zake mapema hawa mabinti wanaua Sana wadogo zetu japo kuanzia form five aligoma Kutumia dawa kijana wa watu na Sijui Nani alimpa.

Aisee matukio ni MENGI WATU wa Afya tunakutana na mengi na ndio maana Tunakuwa na Roho Fulani tunazijua Wenyewe
 
Dah!!!, Kweli kabisa Mkuu ukiwa Daktari lazima ukute na mengi.Mungu awabariki sana wataalamu wetu wa Afya.
 
Poleni na hongereni sana kwa kazi ngumu
 
Kifo kinatisha sana

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Mwanafalsafa wa zamani wa Kigiriki aliyejulikana kwa jina la EPICURUS aliwahi kusema hivi kuhusu Kuogopa kifo; "Usiogope kifo kwa kuwa bado unaishi hivyo bado hakijakupata,na ukifa utakuwa umeshakufa huwezi kufa tena ". Huyu jamaa alitaka kumaanisha kuwa huwezi Kuogopa kifo ili hali hakijakupata bado,sasa unaogopaje kitu ambacho hujawahi kutana nacho?,na kikikupata unakuwa umeshakufa hivyo huwezi kufa tena.
 
Nimeuchukua huu msemo mkuu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Amen! Ni hali mbaya sana ambayo mtu anaweza kuipitia,kuna mwanangu mdogo anaongea kama cherahani,kila muda ananiambia"Baba nipe pochi yangu mi nataka kwenda hoskwitali(hospitali) kumsalimia mamaa" hapo ndiyo ananianzishia msiba upya.
So sad
 
Watu wa afya,ni km hawaigopi,unaweza fikiri ni katili Ila ni jinsi kazi zenu zilivyo.endeleeni kufanya kazi ,kazi yenu ni njema
 
Mungu gan na yeye ndio mnadai ndio mungu ??
Watu mmeelewa ila wagumu kuelewa. Sio kwamba hujui,unajua huyo ni MUNGU MWANA. Hapo alikuwa anamaanisha mkuu,ambaye ni babaake pia.
 
Dah. Mungu wangu. Pole sana capt Tamar
 
Poleni sana wafiwa. Hakuna kitu kinauma kama kuondokewa na uwapendao. Ni kumbukumbu isiyofutika akilini..... Mimi mwenyewe nikikumbuka nakosa ata nguvu ya kuelezea. Acha tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…