Je, Damu za Raia Ndiyo Ufunguo wa Kimamlaka Uongozi?

Je, Damu za Raia Ndiyo Ufunguo wa Kimamlaka Uongozi?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Kama Unavielewa Vile Vyama Vya Siri na Wanaoiiendesha Dunia Karibu Tujadili kwa Undani.
>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<
Niendelee kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopotezwa kwa kuuliwa kupitia askali waajiliwa wa government yetu.

Nimejiuliza kimya kimya ila jibu linakosekana ila matukio mengi huko nyuma na sehemu mbalimbali duniani yanaelekea kunioa jibu ila bado nakata tamaa kuamini.

Mara nyingi sana, mauaji kwa njia tofauti huwa yanatokea katika nchi ambayo inaemda kumpata kiongozi wa Taifa anayepigiwa kura.

Kwa mtizamo huo naona kuna muingiliano mkubwa wa kutoa fadhili kwa wanaotakiwa kukukabidhi madaraka na kuwalipa hesabu ya uongozi.

Kwa wenye kufuatilia na kujifunza kwenye ile hidden muscle of leadership from deep society wanaweza kunielewa.

Mfano, hata baada ya watu kufa na kujeruhiwa kuna matamko makubwa kutoka kwa mashirika ya kimataifa na vyama vyenye nguvu za kiushawishi duniani akiwemo Papa kuwa kilichotokea siyo sawa ila, hakutakuwa na comeback yoyote.

Kitakachofanyika huyohuyo kiongozi ataenda kwa hao wajuba kupeleka au kupewa honorary na maisha yaleeee, tunasahau.

Nawasilisha kutokea Singida.
 
Nadhani haya ndiyo makafara yenyewe kutoka kwa waabudu shetani kutimiza maagano yao ya kumwaga damu za raia ili utawala wao uimarike
 
Huku kuna wengine wana hirizi za ajabu sana! Ndani ya hirizi zao kuna mabaki ya wadudu wakali kama nge, manyigu, siafu, sungusungu, manyoya simba na chui, kana kwamba haitoshi wamekula kabisa na moyo wa simba ili waogopewe kama simba wanapoongea na kutoa maagizo! Kwenye ishu kama hizi kuna ibada za kishetani nyingi sana ili kufanikisha mambo yao
 
Back
Top Bottom