ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
Mara nyingi tunasikia baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zikijinasibu kuwa zinafuata mfumo wa demokrasia
Lakini swali langu ni hili: Je, demokrasia inaonekana kwa vitendo, au ipo kwenye maandishi tu?
Kwa uelewa wangu, demokrasia ya kweli ni pamoja na:
Wananchi kuwa huru kutoa maoni yao bila kubughudhiwa, ilimradi maoni hayo ni ya kujenga na yana tija
Sheria kufanya kazi bila kupindishwa(Mahakama huru)
Wananchi kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka(haki ya msingi)
Sasa mimi najiuliza hapa Tanzania kuna demokrasia?
Kama ndiyo, ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa demokrasia ipo?
Au ipo kwa kiwango kidogo sana?
Au hamna kabisa, na ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa hakuna demokrasia?
Swali la mjadala 👇
Unadhani ni nini kifanyike ili demokrasia isitoke kwenye kitabu tu bali ije kwenye vitendo?
Naona baadhi ya wananchi wamejaribu kutumia njia mbalimbali kupaza sauti zao, lakini hakuna matokeo positive
Wakajaribu kuandamana, sote tunajua nini kilitokea(October)
Juzi hapa kwenye Saba Saba waliweka nadhiri, mambo yakawa sivyo walivyotarajia
Nasikia tena wanapanga tarehe nyingine
Je, haya yote yanashindwa kufanikiwa kwa sababu hakuna demokrasia?
Au kuna sababu nyingine zinazofanya mambo haya yasiwe na matokeo?
Nini kifanyike ili taifa lipate utulivu, wananchi wasikike, na demokrasia iwe kitu kinachoonekana kwenye vitendo?
Karibuni kwenye mjadala
NB : Sina chama mimi mwana nchi ninaetamani kuona taifa bora sio bora taifa
ShesRise_1 ✋️