Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

Mizania ya demokrasia imepwaya sana ukizingatia kwa sasa kuna malalamiko kuhusu......

1. Uhuru wa vyama vya upinzani kufanya shughuli zao umekuwa ukilalamikiwa na vyama vya Siasa hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

2. Kumekuwa na malalamiko kuhusu uwanja wa ushindani wa kisiasa kutokuwa sawa, hasa wakati wa chaguzi yametokea toka uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2020 na 2025

2. Wanaharakati na vyama vya upinzani wamekuwa wakidai kukabiliwa na vitisho, vikwazo, kesi na shinikizo la kisiasa.

3. Hoja ya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na uwajibikaji wa taasisi imekuwa sehemu ya mjadala mkubwa, Chombo cha habari Clouds FM kiliwahi kufungiwa wiki moja na kikaamlishwa kutoa tangazo la kuiomba radhi serikali, Online TV ya Jambo ilifungiwa siku 90 na hata huu mtandao wa Jamiiforums ulifungiwa bila hata sababu za msingi.

Hapo utaona ni namna gani demokrasia imebaki kwenye vitabu na midomo ya watu lakini utekelezaji wake kwa vitendo haupo
Hoja zako zote zina uzito na baadhi ya watu wanaamini hivyo

Sasa tunatokaje hapa?
Wewe unadhani ni hatua gani za kufata ili kuondoa haya mambo
 
Mmepewa Treni bila Reli ngoma itakapo pasua ndio huko huko.
Demokrasia ina maana ya kufanikiwa hata kupitia gharama za watu wengine.

Maisha ya makundi matatu:
Mlia shida, Muwakilishi na Mbobevu anae Ekti kutwikwa mizigo ni ujinga mkubwa mno.

Nashauri CHAPANENI PASIKALIKE.
Ngoja tuone
 
Ni wazi kuwa demokrasia ya nchi yetu ni ya kusadikika hakuna demokrasia kabisa watawala wanaongoza nchi kwa misingi ya kimabavu na kidikteta, demokrasia ni kitu Cha kuumiza masikioni mwao, katiba mpya inapigwa danadana, tume huru hamna, uhuru wa kutoa maoni ni sifuri nk,

Cha kufanyika hapa ili nchi hii iwe ya kidemokrasia ni wazi step ya kwanza ijapokuwa haitakuwa suluhisho kwa asilimia 100 ni lazima CCM itoke madarakani tupate kwanza transition government itakayoshughulikia masuala yote muhimu katika kuelekea kwenye njia sahihi ya kidemokrasia at least

NB: Demokrasia siyo asili ya mtu mweusi, ila tunaweza kufikia hatua njema ya kuwa na taifa lenye misingi imara ya kuheshimu haki za watu na sheria bora
 
Tanganyika haijawahi kua na demokrasia , NI nchi inayoongozwa na watu wapumbavu, walafi, wakatili na mbumbumbu WA kiwawango cha lami wanaotumia propaganda za miaka ya 1960's kuongoza miaka ya 2020's..Siasa ya Tanganyika NI takataka
Aisee Asantee kwa maoni
 
Mara nyingi tunasikia baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zikijinasibu kuwa zinafuata mfumo wa demokrasia

Lakini swali langu ni hili: Je, demokrasia inaonekana kwa vitendo, au ipo kwenye maandishi tu?

Kwa uelewa wangu, demokrasia ya kweli ni pamoja na:

Wananchi kuwa huru kutoa maoni yao bila kubughudhiwa, ilimradi maoni hayo ni ya kujenga na yana tija
Sheria kufanya kazi bila kupindishwa(Mahakama huru)

Wananchi kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka(haki ya msingi)

Sasa mimi najiuliza hapa Tanzania kuna demokrasia?

Kama ndiyo, ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa demokrasia ipo?

Au ipo kwa kiwango kidogo sana?

Au hamna kabisa, na ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa hakuna demokrasia?

Swali la mjadala 👇

Unadhani ni nini kifanyike ili demokrasia isitoke kwenye kitabu tu bali ije kwenye vitendo?

Naona baadhi ya wananchi wamejaribu kutumia njia mbalimbali kupaza sauti zao, lakini hakuna matokeo positive

Wakajaribu kuandamana, sote tunajua nini kilitokea(October)

Juzi hapa kwenye Saba Saba waliweka nadhiri, mambo yakawa sivyo walivyotarajia

Nasikia tena wanapanga tarehe nyingine

Je, haya yote yanashindwa kufanikiwa kwa sababu hakuna demokrasia?

Au kuna sababu nyingine zinazofanya mambo haya yasiwe na matokeo?

Nini kifanyike ili taifa lipate utulivu, wananchi wasikike, na demokrasia iwe kitu kinachoonekana kwenye vitendo?

Karibuni kwenye mjadala

NB : Sina chama mimi mwana nchi ninaetamani kuona taifa bora sio bora taifa

ShesRise_1 ✋️
In fact,
Tanzania,
demokrasia ipo theoretically na practically na inatekelezwa inavyostahili kama ilivyo kwenye maandishi ya wagunduzi wa demokrasia wa tangu enzi na enzi za mwanzo wa utawala na uongozi, na ndio maana Serikali kuu, Mahakama na Bunge vinatekeleza wajibu wao bila shinikizo za ndani au nje ya nchi, bali kulingana na matakwa na vipaumbele vya waTanzania wote.

Na kwa standards za kimataifa,
Demokrasia ya Tanzania inafanya vizuri zaidi duniani ukilinganisha na kwingineko ulimwenguni, na hii ikimaamisha kwamba hakuna haja kubwa sana ya maboresho ya kimuundo ambayo yanaweza kubadili tafsiri na maana ya demokrasia na chimbuko lake, ispokua ni muhimu zaidi kuimarishwa kwa namna ya kuimpact fikra na maana halisi ya demokrasia miongoni mwa wananchi ili hatimae waondokane na dhana potofu ya kua, eti demokrasia ni kulazimisha mambo kadiri ya mapenzi au matakwa ya wachache.

Kiujumla Tanzania ni tulivu kisiasa, kijamii na kiuchumi, na ndio maana hata tunajadiliana kwa uhuru na amani kama taifa, lakini pia kama watoto wa mama Tanzania.

Mahali ambako hakuna demokrasia tulivu kama ya Tanzania, hakuna uhuru wala amani kama tuliyo nayo waTanzania.

Kususa ni demokrasia, ila ni muhimu kufahamu kwamba ukisusa wengine wanasonga mbele bila kujivunga 🐒
 
Ni wazi kuwa demokrasia ya nchi yetu ni ya kusadikika hakuna demokrasia kabisa watawala wanaongoza nchi kwa misingi ya kimabavu na kidikteta, demokrasia ni kitu Cha kuumiza masikioni mwao, katiba mpya inapigwa danadana, tume huru hamna, uhuru wa kutoa maoni ni sifuri nk,

Cha kufanyika hapa ili nchi hii iwe ya kidemokrasia ni wazi step ya kwanza ijapokuwa haitakuwa suluhisho kwa asilimia 100 ni lazima CCM itoke madarakani tupate kwanza transition government itakayoshughulikia masuala yote muhimu katika kuelekea kwenye njia sahihi ya kidemokrasia at least

NB: Demokrasia siyo asili ya mtu mweusi, ila tunaweza kufikia hatua njema ya kuwa na taifa lenye misingi imara ya kuheshimu haki za watu na sheria bora
Asante mkuu karibu tena
 
Mara nyingi tunasikia baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zikijinasibu kuwa zinafuata mfumo wa demokrasia

Lakini swali langu ni hili: Je, demokrasia inaonekana kwa vitendo, au ipo kwenye maandishi tu?

Kwa uelewa wangu, demokrasia ya kweli ni pamoja na:

Wananchi kuwa huru kutoa maoni yao bila kubughudhiwa, ilimradi maoni hayo ni ya kujenga na yana tija
Sheria kufanya kazi bila kupindishwa(Mahakama huru)

Wananchi kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka(haki ya msingi)

Sasa mimi najiuliza hapa Tanzania kuna demokrasia?

Kama ndiyo, ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa demokrasia ipo?

Au ipo kwa kiwango kidogo sana?

Au hamna kabisa, na ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa hakuna demokrasia?

Swali la mjadala 👇

Unadhani ni nini kifanyike ili demokrasia isitoke kwenye kitabu tu bali ije kwenye vitendo?

Naona baadhi ya wananchi wamejaribu kutumia njia mbalimbali kupaza sauti zao, lakini hakuna matokeo positive

Wakajaribu kuandamana, sote tunajua nini kilitokea(October)

Juzi hapa kwenye Saba Saba waliweka nadhiri, mambo yakawa sivyo walivyotarajia

Nasikia tena wanapanga tarehe nyingine

Je, haya yote yanashindwa kufanikiwa kwa sababu hakuna demokrasia?

Au kuna sababu nyingine zinazofanya mambo haya yasiwe na matokeo?

Nini kifanyike ili taifa lipate utulivu, wananchi wasikike, na demokrasia iwe kitu kinachoonekana kwenye vitendo?

Karibuni kwenye mjadala

NB : Sina chama mimi mwana nchi ninaetamani kuona taifa bora sio bora taifa

ShesRise_1 ✋️
inaumiza swali au Jibu?
 
Back
Top Bottom