Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

In fact,
Tanzania,
demokrasia ipo theoretically na practically na inatekelezwa inavyostahili kama ilivyo kwenye maandishi ya wagunduzi wa demokrasia wa tangu enzi na enzi za mwanzo wa utawala na uongozi, na ndio maana Serikali kuu, Mahakama na Bunge vinatekeleza wajibu wao bila shinikizo za ndani au nje ya nchi, bali kulingana na matakwa na vipaumbele vya waTanzania wote.

Na kwa standards za kimataifa,
Demokrasia ya Tanzania inafanya vizuri zaidi duniani ukilinganisha na kwingineko ulimwenguni, na hii ikimaamisha kwamba hakuna haja kubwa sana ya maboresho ya kimuundo ambayo yanaweza kubadili tafsiri na maana ya demokrasia na chimbuko lake, ispokua ni muhimu zaidi kuimarishwa kwa namna ya kuimpact fikra na maana halisi ya demokrasia miongoni mwa wananchi ili hatimae waondokane na dhana potofu ya kua, eti demokrasia ni kulazimisha mambo kadiri ya mapenzi au matakwa ya wachache.

Kiujumla Tanzania ni tulivu kisiasa, kijamii na kiuchumi, na ndio maana hata tunajadiliana kwa uhuru na amani kama taifa, lakini pia kama watoto wa mama Tanzania.

Mahali ambako hakuna demokrasia tulivu kama ya Tanzania, hakuna uhuru wala amani kama tuliyo nayo waTanzania.

Kususa ni demokrasia, ila ni muhimu kufahamu kwamba ukisusa wengine wanasonga mbele bila kujivunga 🐒
Hizi sauti zinazosikika kutoka kila upande zikidai mabadiliko

Kwanini hizisikilizwi badala yake huzimwa kama mshumaa?

Hii ndio demokrasia unayozungumzia au kuna nyingine?

Au tusema labda kuna watu wana demokrasia na wengine hawana ndani ya taifa moja?
 
Kuna mambo yanahitaji demokrasia.
Kuna mambo Hayana Demokrasia.

Mambo kama ya Utawala, pesa, na Mapenzi hayanaga Demokrasia.
Ooh Mambo ya utawala nayo ni miongoni mwa mambo yasiyoitaji demokrasia

Kwahiyo sasa watu watulie si ndio?
 
Tanzania imewahi kuwa "hybrid regime" enzi za Mkapa na Kikwete. Tofauti na hapo haijawahi kuwa na demokrasia kabisa.
Mkapa na Kikwete mambo yalikua vuguvugu si moto si baridi

Asante mkuu kipindi hicho nilikua bado mdogo aisee
 
Ni kweli kabisa mkuu

Kama ni hivyo ni nini kifanyike walau tuonje ladha ya Democracy kwa mara ya kwanza
Maana umesema hatujawahi kabisa kua na Democracy hapo kabla
Mambo yatakayoleta demokrasia Tanzania ni CCM kupasuka na kugawanyika wakigombea madaraka au mapinduzi ya umma ya raia. Hilo la kwanza linaweza kutokea kirahisi miaka michache ijayo.
 
Mambo yatakayoleta demokrasia Tanzania ni CCM kupasuka na kugawanyika wakigombea madaraka au mapinduzi ya umma ya raia. Hilo la kwanza linaweza kutokea kirahisi miaka michache ijayo.
Ngoja tuone muhimu uzima uwepo muda utesema
 
Mkapa na Kikwete mambo yalikua vuguvugu si moto si baridi

Asante mkuu kipindi hicho nilikua bado mdogo aisee
Hiyo ndio inaitwa "hybrid regime". Ni mfumo ambao wapinzani wanaweza kushinda kwa kiasi fulani japo vikwazo vinakuwa vingi kwa vyama, vyombo vya habari na taasisi huru za kijamii na pia dola inatumika ila kwa kificho hivi kukibeba chama tawala.
 
Hiyo ndio inaitwa "hybrid regime". Ni mfumo ambao wapinzani wanaweza kushinda kwa kiasi fulani japo vikwazo vinakuwa vingi kwa vyama, vyombo vya habari na taasisi huru za kijamii na pia dola inatumika kisiri ila kwa kificho hivi kukibeba chama tawala.
Asante sana mkuu
hizo awamu mbili ilitumika akili kubwa kama ni hivyo
 
Hizi sauti zinazosikika kutoka kila upande zikidai mabadiliko

Kwanini hizisikilizwi badala yake huzimwa kama mshumaa?

Hii ndio demokrasia unayozungumzia au kuna nyingine?

Au tusema labda kuna watu wana demokrasia na wengine hawana ndani ya taifa moja?
those are just social media narratives and they have nothing to do with democracy, but kwa ground hakuna kitu kama hiyo na kwahivyo hakuna haja kupoteza wakati kuskiza porojo ambazo hakuna.

in fact,
dhana ya kujipa utakatifu na kudhani eti hiyo ndio demokrasia nadhani haiwezi kuwababaisha wanademokrasaia wanao ipractice.

hakuna haja kuinajisi demokrasia kwa kubadili misingi yake kwa kujaribu kuingiza dhana ya uspecia feki au kujivika utakatifu feki kwenye kukiuka demokrasia kwa lengo la kutafuta namna ya kuingiza haki za fedheha na zilizokinyume na utamaduni wetu hata kabla ya demokrasia.🐒
 
Asante kwa maoni
 
Tanzania ina constitutional democracy on paper tu.

Ukiangalia historia ya Tanzania, kila baada ya uchaguzi au kwenye masuala makubwa ya kisiasa, mjadala unaorudiwa mara kwa mara ni ule ule, uhuru wa kisiasa, uhuru wa kutoa maoni, nafasi ya vyombo vya habari, na namna taasisi za dola zinavyotekeleza majukumu yao, haya maswali yanayoendelea kujirudia kwa miaka mingii ni ishara tosha kwamba bado kuna maeneo yanayohitaji kuimarishwa.

Serikali yoyote inaweza kusema tuna demokrasia lakini kipimo halisi ni namna ambavyo raia anaweza kuikosoa serikali bila ya kuwa na hofu yoyote, namna upinzani unavyoweza kufanya siasa kwa uhuru na namna taasisi zinavyofanya kazi bila kuonekana kuwa na upendeleo , hapa ndipo actions speak louder than words.

Ukiwa na sheria nzuri lakini utekelezaji wake unategemea nani anahusika kwanza, hapa ndipo demokrasia inabaki kuwa maandishi tu kwenye vitabu.
Rule of law inapaswa kumlinda kila mtu siyo wale tu wanaokubaliana na mamlaka pekee.
 
Kwahiyo myaka nenda rudi linajadiliwa jambo lile lile hakuja agenda mpya
Inasikitisha

Ni nini kifanyike ili tupate demokrasia ya kweli sio hii ya kwenye maandishi
 
CCM SIO CHAMA ,FIKIRIA KWA SASA TCRA INAFUNGA MITANDAO WATU WASIONGEE LEO HII HUPATI ,OTP KWA APP MBALIMBALI YAANI UNAJITENGA NA DUNIA
 
Hoja zako zote zina uzito na baadhi ya watu wanaamini hivyo

Sasa tunatokaje hapa?
Wewe unadhani ni hatua gani za kufata ili kuondoa haya mambo
Nadhani Mawaziri wakuu wa jumuiya ya madola wameshatoa maagizo na ushauri ndani ya siku 90 kuna mambo Serikali iyafanyie kazi na ipeleke repoti ya utekelezaji wake kama Watawala wataamua kuyafanyia kazi nadhani huo ndio utakuwa mwanzo mpya
 
Kwahiyo myaka nenda rudi linajadiliwa jambo lile lile hakuja agenda mpya
Inasikitisha

Ni nini kifanyike ili tupate demokrasia ya kweli sio hii ya kwenye maandishi
Demokrasia ya kweli inajengwa kwa namna sheria zinavyotekelezwa, ili uione kwa vitendo, ni lazima.

Sheria zisimtazame mtu wala chama, zitumike kwa usawa kwa wote.

Mahakama na taasisi nyingine ziendelee kuimarishwa ili ziaminike kuwa zinafanya maamuzi kwa uhuru.

Wananchi wawe na nafasi ya kutoa maoni, kufanya mikutano na maandamano ya amani kwa mujibu wa sheria, huku usalama wa wote ukilindwa.

Uchaguzi uwe wa kuaminika kiasi kwamba anayeshinda ashinde kwa ridhaa ya wananchi, na anayeshindwa akubali matokeo.

Serikali ikubali ukosoaji wa kujenga, na wananchi nao wakosoe kwa hoja badala ya matusi au vurugu.

Kwa kifupi, tunapaswa kujenga mfumo unaoheshimu sheria.
 
Nadhani Mawaziri wakuu wa jumuiya ya madola wameshatoa maagizo na ushauri ndani ya siku 90 kuna mambo Serikali iyafanyie kazi na ipeleke repoti ya utekelezaji wake kama Watawala wataamua kuyafanyia kazi nadhani huo ndio utakuwa mwanzo mpya
Sawa tu upe muda nafasi
Asante kwa maoni yako mkuu na karibu tena
 
Back
Top Bottom