Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

Je, Demokrasia Tanzania ipo kwa vitendo au ipo kwenye maandishi tu?

ShesRise_1 natoa ofa kwako,kama utakuwa na hamu ya kujua hili fekero ni la nani, omba maombi rasmi pm nitakwambia🤣🤣

Vinginevyo endelea kuinjoy na hii I'd ya mchongo hahaha
 
Huu ni mtego na ukataa na kuutegua katika jina la Yesu amen

Acha niendelee ku enjoy hili fekero mkuu na wote tuseme amen
🤣🤣 dah umenifanya nicheke kwa tabasamu kubwa sana,,,kama ingekuwa hivyo ningezama mwenyewe pm bila kukuarifu, siku ukija kunijua japo kwa bahati mbaya utakuja kuniomba radhi kwa hii dhana yako kwangu

Eneweizi let's have funny na hili fekero na ofukozi ukinijua hakuna mizuka tena,ngoja mizuka iendelee, pamoja sana

Keep tagging me when necessary, nitakaribia,chao!
 
🤣🤣 dah umenifanya nicheke kwa tabasamu kubwa sana,,,kama ingekuwa hivyo ningezama mwenyewe pm bila kukuarifu, siku ukija kunijua japo kwa bahati mbaya utakuja kuniomba radhi kwa hii dhana yako kwangu
PM ipo closed wewe unadai ungetaka ungekuja PM how kwamba tumewahi kuwasiliana?
Eneweizi let's have funny na hili fekero na ofukozi ukinijua hakuna mizuka tena,ngoja mizuka iendelee, pamoja sana
Baaasiiiiiiii
Keep tagging me when necessary, nitakaribia,chao!
Sawa nitafanya hivyo
 
Demokrasia ni bidhaa ya watawala inayowasaidia watawala,,,
Toka lini Bepari akakuletea bidhaa ya kuweka usawa kwenye jamii..
 
Mara nyingi tunasikia baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zikijinasibu kuwa zinafuata mfumo wa demokrasia

Lakini swali langu ni hili: Je, demokrasia inaonekana kwa vitendo, au ipo kwenye maandishi tu?

Kwa uelewa wangu, demokrasia ya kweli ni pamoja na:

Wananchi kuwa huru kutoa maoni yao bila kubughudhiwa, ilimradi maoni hayo ni ya kujenga na yana tija
Sheria kufanya kazi bila kupindishwa(Mahakama huru)

Wananchi kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka(haki ya msingi)

Sasa mimi najiuliza hapa Tanzania kuna demokrasia?

Kama ndiyo, ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa demokrasia ipo?

Au ipo kwa kiwango kidogo sana?

Au hamna kabisa, na ni mambo gani yanakufanya uamini kuwa hakuna demokrasia?

Swali la mjadala 👇

Unadhani ni nini kifanyike ili demokrasia isitoke kwenye kitabu tu bali ije kwenye vitendo?

Naona baadhi ya wananchi wamejaribu kutumia njia mbalimbali kupaza sauti zao, lakini hakuna matokeo positive

Wakajaribu kuandamana, sote tunajua nini kilitokea(October)

Juzi hapa kwenye Saba Saba waliweka nadhiri, mambo yakawa sivyo walivyotarajia

Nasikia tena wanapanga tarehe nyingine

Je, haya yote yanashindwa kufanikiwa kwa sababu hakuna demokrasia?

Au kuna sababu nyingine zinazofanya mambo haya yasiwe na matokeo?

Nini kifanyike ili taifa lipate utulivu, wananchi wasikike, na demokrasia iwe kitu kinachoonekana kwenye vitendo?

Karibuni kwenye mjadala

NB : Sina chama mimi mwana nchi ninaetamani kuona taifa bora sio bora taifa

ShesRise_1 ✋️
IPO kwenye makaratasi,hata viapo vipo mdomoni,matendo ni ziro!
 
Democrasia ni uwanja mpana sana Wanaosema hamna democrasia ndo wanatumia democrasia kusema hamna democrasia hivo tu
Sawa hebu nipe uelewa wako japo kidogo mi nataka kujifunza

Mf: hapo umesema wanaosema hakuna demokrasia
Wanatumia hiyo demokrasia kusema haipo

Njoo kaka
 
Back
Top Bottom