Kwanza nianze kwa kusema hakuna misingi ya aina moja ya demokrasia duniani kote, hata huko nchi zilizo endelea ambazo ndio huwa kioo chetu cha kujitazamia pia nako hawana demokrasia ya aina moja.
Utakuta nchi hii imefaulu katika hili na kufeli katika hili,ingawa tunaweza sema kwa asilimia kubwa wana jitahidi, juzi hapa tumeona Trump hakufuata sheria juu ya swala zima la kuanzisha vita na Iran,lakini alijiamlia tu,kwahiyo utaona hata huko hawako salama asilimia Mia.
Sasa ukija Afrika usitarajie utakuta demokrasia kama ya huko ughaibuni,hapa napo kuna demokrasia yetu,na ndani ya nchi zetu pia tunatifautiana utekelezaji wake, hiyo ilikuwa ni general overview
Sasa tuje hapa Tanzania, kwa mtazamo wangu huwezi sema kabisa hii nchi haina demokrasia,kwa sababu tuna vipengele ambavyo vinashiria uwepo wa demokrasi ingawa havitekelezwi kwa asilimia mia moja
Vipengele kama Uhuru wa kutoa maoni, uwepo wa haki za binadamu,uwepo wa mahakama ,uhuru wa vyombo vya habari, ,uwepo wa uchaguzi na kadhalika
Ila mambo yote haya hayatekelezwi kwa asilimia mia,maana ukisema hakuna demokrasia kabisa inamaa hivi viashiria havipo kabisa kitu ambacho sio kweli
Kuna nchi ambazo unaweza sema huko hakuna demokrasia kabisa kwa maana hakuna hizo elements ambazo ni viashiria vya demokrasia,nchi kama hizo ndio unaweza sema hazina demokrasia.
Sasa mtoa mada anauliza je nini kifanyike kwenye mazingira kama haya?
Wote tunajua kwenye mazingira ambayo yapo nchini kwetu kwa sasa hakuna cha kufanya au kuwafanya watawala watekelezwe matakwa yetu,shinikizo pekee litatoka huko kwenye jumuiya za kimataifa,kwasababu wao wanaweza kutuwajibisha kwakuwa tunahitaji misaada yao,kuna ambao wametoa siku 30 mpaka 90 kwa watawala kufanya mabadiliko kadhaa,ngoja tuone muda utaongea