MrfursaTZA
Member
- Jul 26, 2024
- 29
- 94
Ningependa kujua, je, inawezekana kuwa Rais wa nchi wakati wewe si Raia wa nchi hiyo?
Pia ningependa kufahamu, Mungu ni wa dini gani? Je, ni Muislamu au Mkristo?
Kwa nini Masheikh na Wachungaji husema kwamba dini haiwezi kukufikisha Mbinguni?
Kama Dini haziwezi kutupeleka Mbinguni, basi kwa nini zipo? Kama Mungu yuko upande wa Wakristo, kwa nini hawapendelei?
Na kama Mungu ni wa Waislamu, kwa nini nao hawapendelei? Je, inamaanisha nini kusema kwamba Mungu ni wa kila mtu?
Kwa nini alitufanya tofauti kwa rangi? Na kwa nini alitufanya tofauti hata kwa jinsi tunavyoishi duniani au kwa kipato?
Kwanini aliumba shida na matatizo?
Na kusema kwamba alituumba kwa mfano wake, ningependa kujua, kama sisi ni mfano wa Mungu, je, hii inamaanisha kwamba Mungu anakula chakula, anaenda chooni, na pia anakabiliana na matatizo kama sisi?
Kama jibu ni hapana, kwa nini sisi, ambao ni mfano wa Mungu, tunateseka hivi wakati yeye ana uwezo mkubwa wa kutusaidia?