Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Asante kwa mchango wako ndugu, ningependa nijibu swali lako ulilo weka mwisho kama ifuatavyo.

Jibu langu ni hapana sipendekezi kuwa watu waache dini ila kama ni hiari yao kuacha basi ni sawa uhuru wao wa kimaamuzi nita uheshimu. Lakini je maisha watakao ishi hao watu baada ya kuacha dini yatakua bora au yata kuwa maisha yasiyo pendeza na ya hovyo sana ?

Majibu ya swali hilo ulilo niuliza ni haya na yenye maelekezo yake mafupi:-
1. Mtu akiacha dini na akaweza kuishi maisha yaliyo bora tofauti na maisha aliyo kua anaya ishi ndani ya dini atakua amefanya uamuzi ulio bora sana katika maisha yake, maisha bora nayo yazungumzia hapa ni maisha yaliyo jaa maadili bora yenye kuthamini na kuheshimu utu wa kila mtu aliye kuzunguka na ambaye yupo mbali nawe.

2. Mtu akichukua uamuzi wa kuacha dini na kuishi maisha yasiyo bora yaliyo jaa tabia mbovu zisizo na maadili katika jamii na zisizo thamini utu na heshima za wale wa mzungukao na wale walio mbali naye, tofauti na alivyo kuwa ndani ya dini basi huu ni uamuzi wa hovyo sana atakuwa amechukua katika maisha yake.

Mwisho ningependa kuhitimisha kwa kusema si kwamba mimi naitafsiri dini kwa kutawaliwa na maovu kila pande zote ndani yake la hasha nita kuwa naji ongopea mwenyewe dini pia ipo na mambo mengine mazuri tu ya kujifunza ambayo hata mimi kupitia vitabu vyake huwa nachukua muda na kujifunza na kupata maarifa.

Napenda wafuasi wa dini wenye uelewa wa kielimu kama wako ila ubaya ni kuwa katika dini mpo wachache sana, walio wengi dini zime watawala kwa kiwango kikubwa sana mpaka kuathiri uelewa wao wa mambo mbalimbali hii hali hasa hasa ipo kwetu huku Afrika.

Dini pasipo elimu bora ya kidunia [ maarifa bora ] ni mzigo mzito sana unao waumiza wengi.

Ningependa ndugu kama utaweza uni orodheshee hivyo vitabu ili nipate kuvisoma.
 
Mie Sina neno Ila Napenda sana watu wadadisi.Mie Naomba aliye na elimu ya nyota anisaidie
 
Mie Sina neno Ila Napenda sana watu wadadisi.Mie Naomba aliye na elimu ya nyota anisaidie
Sawa ndugu wenye hio taaluma watapatikana na kuku saidia.
Au kwa kuku saidia zaidi anzisha thread yenye kuhitaji msaada wa hilo jambo lako.
 
Religion is the Last devil secret weapon to destroy humanity. Ndo maana siku zile za mwisho wote tutakuwa dini Moja.... Guess hiyo dini Moja itatokeaje?? Hizo dini zoteeee tunazoziita za maana zitaungana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Agenda 30 halafu zikiunguna zinakufa ni mwendo wa goverment moja[emoji2]
 
Ukiangalia kwa makini utagundua dini ni vitisho tu!!mf. Moto wa milele, Mungu atachomaje watoto wake? Toa sehemu ya kumi tena kwa kulazimisha, Mungu anahitaji pesa? Hata ufufuko ni mchongo tu!
 
Kwahiyo ni kama alivyosema Machiavelli “The end will justify the means”.

Umenijibu vizuri na nimeridhika na majibu yako.

Kuhusu Vitabu soma “The Prince” kaandika Machiavelli mwenyewe, ni cha muda mrefu lakini mambo yote ni ya kweli kabisa.

Soma “The Laws of Human Nature” kaandika Robert Greene
 
8. Je waamini wake wana zifahamu historia ya hizi dini zao kwa kina ni wapi zimetoka, zipo na ziendako au wame baki kuwa waamini tu ?
Naomba nijibu swali hili,,,As Mkristo,,,, kama mwamini ninafahamu vizuri history kwa kina maana ipo wazi na haijafichika na pia najua hii imani imetokea wapi na ni nini kitakachokuja kwa siku zijazo,,na ni nini kitakachofuata baada ya kufa,,,Na mimi nimezaliwa mkristo na nimejiridhisha binafsi kwamba kama ninachokiamini ni sahihi au la....Kingine makusudio ya vita vya Crusade yalikuwa ni kujilinda na kukomboa maeneo yaliochukuliwa kwa nguvu au yaliokuwa yamelengwa kuchukuliwa kwa nguvu,,,na sio kwamba Crusade ilipiganwa kwa ajili ya kueneza ukristo....Kama utafuatilia dhulma waliofanyiwa wakristo katika bara la Asia utaona damu nyingi sana ilimwagwa kwa watu waliokuwa hawana hata fimbo kujilinda,,,Fuatilia historia ya genocide dhidi ya waarmenia,,,ndani ya uturuki na damu nyingi sana iliomwagika mpaka watu wakashtukia njama ya kufuta watu wote wenye kumuamini Kristo ndipo ikaanza Counter offensive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…