Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Swali je yote waliyotenda hayo yapo kwenye maamrisho ya vitabu vyao yaani kwenye Torah vitabu vya Wayahudi, Biblia Wakristo na Quran waislamu. Kama hayapo kwenye miongozo ya vitabu hivyo vitatu hayo yalifanywa kwa mwamvuli wa dini na sio maagizo ya dini.

Hakuna dini inayoruhusu kuua ktk dini hizo.
Dini ni utumwa wa kifikra na chuki baina ya wanadamu..Mungu hana DINI
 
Hawa walipigania dini lakini sio maagizo ya dini.
Hizi vita dini iliingizwa Ili kulinda himaya.
Crusade, Wakatoliki walitembeza majambia hatari kwa waislamu Ili kuwablock wasienee ulaya.Kumbuka wakatoliki ndio walioanzisha Uislamu Ili kuwatawala waarabu ndani ya mfumo mmoja ( Islam ).
Hi Dunia Ina wajinga wengi sana badala mfundishwe wakatiliki walianzisha dini ya ukristo badala yake mnafundishwa kuwa eti katoliki walianzisha dini ya uislam na kwa ujinga wenu mnakubali

Waroma walianzisha dini ya ukristo miaka 50 baada ya Yesu kupaa mbinguni kupitia Dora yao ya Roman empire na ndio maana dhehebu la kwanza kabisa la dini ya ukristo ni Romani katoliki

Baadae waingereza wakajitenga na kuanzisha dhehebu lap la Anglican na ujuremani pia wakajitenga wakaanzisha dhehebu lao la Rutheran

Na pia kulikuwa na mwanamke mmoja ana kilema katika pua akajitenga akaanzisha dhehebu la Sabato
 
Swali je yote waliyotenda hayo yapo kwenye maamrisho ya vitabu vyao yaani kwenye Torah vitabu vya Wayahudi, Biblia Wakristo na Quran waislamu. Kama hayapo kwenye miongozo ya vitabu hivyo vitatu hayo yalifanywa kwa mwamvuli wa dini na sio maagizo ya dini.

Hakuna dini inayoruhusu kuua ktk dini hizo.
Story ya Daud alipomtungua na jiwe Goliath ipo kwenye Biblia au imetungwa ?
 
Story ya Daud alipomtungua na jiwe Goliath ipo kwenye Biblia au imetungwa ?
SAsa kama alimtungua Goliath ndio maagizo ya Wakristo wawatungue maadui zao kwa mawe? Lile ni funzo la kiroho zaidi kuliko funzo la kimwili.
Mengine yameandikwa kwa mfano wa mwili yakimaanisha utendaji Kazi wa kiroho wenye utokeo wa kimwili.
 
Hi Dunia Ina wajinga wengi sana badala mfundishwe wakatiliki walianzisha dini ya ukristo badala yake mnafundishwa kuwa eti katoliki walianzisha dini ya uislam na kwa ujinga wenu mnakubali

Waroma walianzisha dini ya ukristo miaka 50 baada ya Yesu kupaa mbinguni kupitia Dora yao ya Roman empire na ndio maana dhehebu la kwanza kabisa la dini ya ukristo ni Romani katoliki

Baadae waingereza wakajitenga na kuanzisha dhehebu lap la Anglican na ujuremani pia wakajitenga wakaanzisha dhehebu lao la Rutheran

Na pia kulikuwa na mwanamke mmoja ana kilema katika pua akajitenga akaanzisha dhehebu la Sabato
Yanayoendelea duniani unayajua au nawe ni mfata mkumbo.
SAsa Kati ya Ukatoliki na uislamu ipi dini iliyotangulia
 
Really?😂
Wakatoliki ndio walioanzisha Uislamu Ili kuwaweka waarabu ndani ya utawala mmoja wa kiimani, kabla waarabu walikuwa wakiabudu miungu yao mbalimbali kupitia masanamu Ili iwe rahisi kuwatawala, Majasusi wa Shirika la Jesuit vatican wakaanzisha dini mpya itwayo islam,itakayowaunganisha waarabu wote kiimani mwaka 600 BC. Mapadre watano wa kikatoliki ndio walioandika kitabu cha Quran na kumtafuta mwanamke mfanyabiashara aitwae Bi Hadija na kumpa utajiri. Bi khadija ndie alimtafuta kijana aitwae Muhammad akamkabidhi kwa mapadre wa kikatoliki ndio waliomfunza Quran mapangoni.Ndipo Uislamu ukaenea kwa kasi Sana Katika nchi za kiarabu ambazo zamani zilikuwa ni nchi za Kikristo ukavuka mpaka na kutaka kuingia nchi za Ulaya mashariki kutokea Uturuki Ili kwenda kuiteka Vatican, Majasusi wa Jesuit wakaingia tena vitani wakarudisha nyuma kupitia vita vya msalaba waarabu wakala Sana panga toka vatican wakarudi nyuma, rejea vita vya msalaba na ottoman empire. Majuzi magaidi wa ISIS tokea iraq wakataka kuendeleza mpango ulioshindwa wa ottoman empire kuupenyesha utawala wa kiislamu Ulaya. Wakasambaratishwa na USA na NATO na kumuua Al baghad kiongozi wa ISIS. Huku kundi la ISIL tawi la ISIS Syria likipelekwa kuzimu na ndege za Putin.
Dini zote uzionazo duniani ni tawi la ukatoliki, maprostetant wote ni watoto wa katoliki.
 
Yanayoendelea duniani unayajua au nawe ni mfata mkumbo.
SAsa Kati ya Ukatoliki na uislamu ipi dini iliyotangulia
Uislam ndio ulianza kuanzia nabi Nuhu , Ibrahim, Musa hadi nabii wa mwisho kwa wana waisrael ambaye ni Yesu wote walikuwa waislam
 
Uislam ndio ulianza kuanzia nabi Nuhu , Ibrahim, Musa hadi nabii wa mwisho kwa wana waisrael ambaye ni Yesu wote walikuwa waislam
Kama ulianza na hao walitumia nguzo gani.Ili uwe Muislamu ni lazima uwe na nguzo tano.
 
Wakatoliki ndio walioanzisha Uislamu Ili kuwaweka waarabu ndani ya utawala mmoja wa kiimani, kabla waarabu walikuwa wakiabudu miungu yao mbalimbali kupitia masanamu Ili iwe rahisi kuwatawala, Majasusi wa Shirika la Jesuit vatican wakaanzisha dini mpya itwayo islam,itakayowaunganisha waarabu wote kiimani mwaka 600 BC. Mapadre watano wa kikatoliki ndio walioandika kitabu cha Quran na kumtafuta mwanamke mfanyabiashara aitwae Bi Hadija na kumpa utajiri. Bi khadija ndie alimtafuta kijana aitwae Muhammad akamkabidhi kwa mapadre wa kikatoliki ndio waliomfunza Quran mapangoni.Ndipo Uislamu ukaenea kwa kasi Sana Katika nchi za kiarabu ambazo zamani zilikuwa ni nchi za Kikristo ukavuka mpaka na kutaka kuingia nchi za Ulaya mashariki kutokea Uturuki Ili kwenda kuiteka Vatican, Majasusi wa Jesuit wakaingia tena vitani wakarudisha nyuma kupitia vita vya msalaba waarabu wakala Sana panga toka vatican wakarudi nyuma, rejea vita vya msalaba na ottoman empire. Majuzi magaidi wa ISIS tokea iraq wakataka kuendeleza mpango ulioshindwa wa ottoman empire kuupenyesha utawala wa kiislamu Ulaya. Wakasambaratishwa na USA na NATO na kumuua Al baghad kiongozi wa ISIS. Huku kundi la ISIL tawi la ISIS Syria likipelekwa kuzimu na ndege za Putin.
Dini zote uzionazo duniani ni tawi la ukatoliki, maprostetant wote ni watoto wa katoliki.
Dah 😂
Tatizo ni kubwa sana, hata kufikiri nako tunashindwa.
 
Sikutoi nje ya mada najaribu kukuonesha kuwa si dini pekee iliyoleta vita, hata kabla ya dini zote vita na uharibifu vilikuwepo.

Na ukitaka kulifahamu vizuri Thomas Hobbes alieleza nadharia yake kuhusu ‘state of nature’ yaani kabla ya dola hali ilikuaje, anasema ilikuwa ni mbaya sana vita kati ya mtu na kila mtu, ustaarabu wala utaratibu haukuwepo kabisa.

Hizo vita za dini ulizotaja ni kasehemu kadogo sana ka picha kubwa ambayo hujataka kuionesha.



Mkuu kuna dhana ndogo sana naona zinakuchanganya, na hiyo ni sababu tayari una majibu yako kichwani (prejudice) kama unataka tuelewane nashauri ufungue akili yako, usitake kila jibu liendane na kile ambacho tayari unacho kichwani.

Umezisoma dini hizo tatu? Yaani mafundisho yake kutoka ktk vitabu vyake?

Na kusema kusoma sisemi kuwa umeona watu wanaodai kuwa wafuasi wa dini hizo wanavyoishi?

Kuna tofauti kati ya Mafundisho ya dini yanavyosema na Wafuasi wa dini tunavyoishi, ukielewa tofauti hii hili seali usingeuliza.

Kama ume ‘observe’ wafuasi wa dini wanavyoishi na hujajisumbua kufungua kurasa za Torati, Injili au Quran basi huwezi jibu hili swali, nashauri uzisome dini, usisome wafuasi wa dini mkuu.

Sisi waislam tunafafanua maana ya dini kuwa ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu.

Hilo suala la haukamiliki mpaka uhusishe Mungu hilo lako mkuu.


Hii maana ni yako mkuu, au una ‘scholary reference’?

Mkuu nauliza tena umesoma dini?

Maana unaandika ni kama vile umetazama wafuasi wa dini kisha ukaleta uzi hapa.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mafundisho ya Dini ambayo huwa yanaegea kwenye vitabu vya dini husika, ukitaka kukosoa DINI ni lazima ukosoe maandiko mkuu, ukitaka kukosoa watu hapo unakosoa wafuasi wa dini, kuna tofauti.

Leo hii Wafuasi wa dini wengi hawaishi kama dini zinavyotaka.

Ungesoma Mafunzo ya dini ungekuwa na jibu kuwa Upendo kwa kila mtu umehimizwa sana.

Na kama ungeelewa asili ya wanaadamu tulivyo usingeuliza kuhusu ‘prgamatic conditions’ iliyo ktk uislam inayohalalisha vita.

Hivi vitu ni rahisi mbona mkuu.

Mkuu umesoma Mafundisho ya Dini?

Ni wapi kwenye Quran na Hadith sahihi (Hizi ndizo nguzo na Mafundisho ya Uislam) wamesema Waislam wafanye kama wanavyofanya magaidi wa Afrika Magharibi?

Lete aya au hadith.

Kama huna maana yake hujasoma dini, ila umetazama wale wanaojiita wafuasi wa dini, kitu ambacho hakitoshi kuwa kipimo cha dini.

Kuna Dini na wafuasi wa Dini, tupo pamoja mkuu?

Ni wapi kwenye Quran imeamrisha hilo?

Nimekueleza sharti moja la vita ktk Uislamu na sharti za yepi haramu kuyafanya, je, hao unaosema wanafuata amri za Quran wametimiza sharti hizo?

Ukitaka kukosoa dini kosoa maandiko nasi tutafurahi kuja kujadiliana nawe, watu wamepewa ‘free will’ kufanya wanachotaka, hata wakisema ni wafuasi wa dini fulani ni jukumu lako kujiridhisha kama ni kweli wanafuata Mafundisho ya dini wanayoidai.

Na si iwe umekaa YouTube umeona mtu kavaa ninja anadai muislam nawe unahitimisha kuwa ni Muislam, ama unamuona mtu kavaa vazi la msalaba basi unahitimisha ati anamfuata Yesu (AS).

Do your homework mkuu:

Kwani nini maana ya kafiri? Usijekuwa unachukia ilhali ni kweli wewe ni kafiri.

Ni sawa mtu ni mjinga, ukimuita mjinga anachukia japokuwa ni kweli yeye ni mjinga.
Mjinga ni mtu asiyejua jambo.


Mfano bibilia inasema Zaburi 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema”.
Kwahiyo hapa Mpunbavu ni yule anaeamini hakuna Mungu, na kama wewe unaamini hakuna Mungu kwa maana hii ya kifungu hiki wewe sio Mpumbavu?

Kwa kiswahili Mpumbavu ni mtu asieyeelewa kile alichofundishwa, je, kama utafundishwa jambo na ukashindwa kuelewa wewe si Mpumbavu?

Mamluki ni askari wa kukodiwa, Je, wewe ukawa ni askari na ukakodiwa wewe si Mamluki?

Nadhani ktk hili ni watu kukataa nafasi walio nazo tuu.

Wakati mwingine ukiitwa Kafir uliza maana ya kafir, kisha jitathimini kama unaendana na maana hiyo, kama ndiyo basi wewe ni kafir.

Tumeelewana mkuu?

Vilevile, kwani mpotevu maana yake nini?

Hapo hakuna chuki wala ubaguzi ni kwamba mtu kaambiwa ukweli na amekasirika.

Sasa rejea kwenye vifungu vya dini vinasemaje, kama vinahamasisha upendo hata kwa asiyeaminj basi suala la kuwaita wana wa shetani ni uzushi wa wafuasi wa dini na hilo halihusiani na Dini.

Soma dini, achana na wafuasi wa dini.

Siyo asiye muislam, ni aliye Ahluh kitaab yaani aidha Mkristo au Myahudi.

Sio waislam wa wapi, hiyo ruhusa imetoka ktk Quran suuratil Maaidah:5

Tazama dini inasemaje? Soma Quran soma Biblia soma Taurati

Kama ulikusudia kuwakosoa Wafuasi wa dini basi ungewalenga hao, nimeingia kwenye uzi huu nikijua zinakosolewa dini.

Ni wapi kwenye Biblia au Quran inahamasishwa chuki?

Ni wapi chuki imeamrishwa? Nukuu kifungu.

Kuhusu vita kwenye Uislam zipo sababu ‘legitimate’ za kuanzisha vita, na zipo sheria za nini cha kufanya na nini si cha kufanya.

Kama unaijua asili ya wanaadamu katu huwezi kuondoa uwezekano wa vita, kufanya hivyo ni kuota.

Nitolee mfano mmoja wa jamii iliyostawi pasina vita au hata ‘elements’ zake.

Uko ‘serious’ hujui?
Mauaji, Ubakaji, Wizi, Rushwa, Uzinzi, Vita, Uchawi, Ulevi, Ufiraji, Kamari, Utumwa n.k

Mkuu Nakushauri hebu soma Human Nature kitabu kaandika Robert Greene,

Hobbes's Doctrine of the State of Nature kaandika Charles Edward Merriam kwa kuanzia.​


Tatizo ni kuwa hauna taarifa za kutosha za mambo unayozungumzia.

Wengi kama wewe huwa mnadhani suala la Dini ni suala jepesi lakini mnasahau kabisa asili ya Binaadamu na umuhimu wa hizi dini.

Mkuu unajua chochote kuhusu asili ya Binaadamu? Au walau Saikolojia zetu?

Nashauri soma hivyo vijitabu hapo juu walau wakati mwingine usiulize seali rahisi kama hili.

Kwenye Uislam mauaji ni halali kwa sharti maalum.

Moja mtu huyo aliua mtu au watu wengine pasina hatia.
Pili, mtu huyo alibaka na kusambaza fitna ktk ardhi.

Nikuulize swali; Leo akatokea mtu akambaka na kumlawiti mama yako, dada yako, mkeo na binti yako kisha akawa anajisifia kuhusu hilo

Ni adhabu gani utampa?

Kama utamsamehe ni kiasi gani cha watu utakuwa unawahamasisha kufanya kama alivyofanya wakijua watasamehewa na hakuna kitu watafanywa?

Panya fikra, tazama kwa mapana zaidi mkuu.

Unajua chochote kuhusu Peace building au peace keeping mkuu?

Umefutilia walau michakato ya kupatikana amani sehemu zenye mitafaruku?

Kama ndiyo hutauliza swali hilo.

Narudia mkuu soma asili ya Binaadamu, uhalisia wake sio kuota.



Mkuu nisamehe najibu maswali yako kwa kuuliza swali.
Unajua lengo kuu la kuwepo dola?
Nikusaidie tu, ni ‘its survival’ na ukileta suala la ‘survival’ basi vita ‘isn’t an option’

Dini hutumika ktk kuunganisha watu wanaoitwa pamoja kupigania ardhi yao.
Rejea ‘Spanish colonization of South America’

Mkuu ukitaka kuunganisha watu katika lengo moja unatumia nini?mwalimu miaka ya ‘60 alitumia utaifa wetu kutuunganisha dhidi ya Uganda.

Wayahudi wanatumia Uyahudi wao kuunganisha watu na Wakristo kutetea ardhi wanayodai kuwa ni yao.

Wewe utatumia ninj, au ushapata picha kuongoza taifa au jamii hali huwaje?

Mtu akuporae nyumba yako, akambaka na kumlawiti mama yako, mkeo, dada yako, bintiyo utamuona ni mkombozi? Au ?

Vizuri, sisi tunaishi duniani, Mungu katupa akili, muongozo na uwezo wa kuyakabili mazingira yetu. Ni juu yetu kufuata muongozo kufanya hivyo na kufanikiwa.

Maisha hapa duniani si chochote ila mtihani kwetu sisi, mungu katupa vyote hivyo ili wenyewe tujioime na tuone tunastahiki ufalme wa mbingu au la.

Na wapo wengi hawakuua mtu mmoja lakini hii leo hakuna wanaomkumbuka, Yesu (as), Muhammad (PBUH) na Mussa (as) wamefanya mengi makubwa ambayo wewe binafsi na akili ulizonazo huwezi fanya hata kufikia theluthi.


Hiko ni kigezo kizuri sana, leo hii hakuna mtumwa wala hakuna anaeshikiwa panga kwenda msikitini au kanisani au kumwamini Mungu lakini tazama ni wangapi wanamuamini.


Naam watu waliridhia wakaenda vitani kupigana kulinda ardhi zao, mama zao, binti zao na wake zao.

Siifahamu Age of Reasoning hebu nielimishe mkuu.

Naam ni sahihi kabisa, mkuu ulitaka iweje?

Naam nakubaliana nawe, sifurahii watu walio waumini wa dini fulani kufuata imani hiyo kibubusa. Ninaamini kila mmoja anapaswa kuifuatilia imani yake kiundani kisha kufikia hatma yake mwenyewe.

Nukuu kifungu cha chuki toka kwenye misahafu.

Achana na watu, tujikite kwenye misingi ya imani hizo.

Hayo umesema wewe, hakuna mahali nimesema hivyo mkuu.

Vizuri, nami nikakuonesha jambo ambalo hukutaka kulionesha kuwa hayo machafuko ya dini ni kijisehemu kidogo tu cha sehemu kubwa ya vita na machafuko yaso na kichwa wala miguu.



Ni kweli, ila elewa asili ya wanaadamu, Dini ni chombo tu kama utaifa kinachotumiwa na baadhi ya watu kufanya yale yasofaa.

Tena hivi ndivyo vimeichafua dunia kwa sehemu kubwa kuliko hata dini.
Sitaweza kutenganisha na kujibu maswali yako yote , Ila nacho shukuru umekiri kua kwenye uislam kuna maamrisho ya Vita za kimauaji kwa sababu maalamu na hili ndilo lengo la thread toka mwanzo kama umeisoma vizuri?

Na kitu kingine nilicho gundua kwako una yaweka makosa ya dini ni kama tu yalivyo makosa mengine yafanywayo na jamii zengine kua ni mfumo wa watu ndivyo ulivyo, sasa hapo ni utofauti gani dini imeleta kama ina endeleza taratibu zile zile kama za jamii zile zilizo zikuta ?

Ningependa tuzungumzie makosa ya dini kama yalivyo makosa yake na siyo kuya fananisha na makosa ya yatendwayo jamii zingine ili kuharalisha makosa ya dini kuonekana ni swala ya kawaida watu kutenda hata kabla ya dini ? Kwa hiyo dini imeshindwa kuleta utofauti ?

Ukilisoma andiko langu kwa makini mwanzoni kabisa limezungumzia dini, Mungu wa hizo dini na wana dini kwa hiyo hakuna sababu ya mimi kuwaweka kando wanadini katika huu mjadala labda kama ujasoma andiko langu .

Unasema Mungu wa hizo dini hajaamrisha chuki na mauaji, umesoma namna alivyo kuwa anawapatia maamrisho wayahudi kwenda kufanya mauaji pasipo kuacha hata kiumbe hai ardhini je hayo unaya fahamu ? Vipi kuhusu mafundisho ya taurati ya Mussa ? Vipi kuhusu Jihad ni nini ?

Unaposema nijifunze kuhusu dini ni ushauri bora kabisa ili nielewe nacho zungumza na ninge penda ufahamu dini huwa najifunza kadiri navyo pata nafasi ili nielewe nacho zungumza.

Unaposema fikra zangu nime funga utakuwa haupo sahihi, kwanza kama ningekuwa fikra zangu zime funga nisinge chukua hata uamuzi wa kujifunza yaliyo ndani ya dini Ni sawa na mwanadini umuambie ajifunze Yale yaliyo ndani ya uchawi au elimu ya uchawi sidhani hata ata endelea kusikiliza. Kuhusu najifunza na nafahamu nafasi yake katika jamii ni ipi ndio maana napo kuja na kuzungumza mambo ni kua nimejifunza.

Naona pia una shindwa kuiweka dini mbalimbali na mfumo wa kisiasa wa kidunia, ndio maana swali langu la mwanzo lili uliza lipi hasa ni lengo la dini ? Naomba urejee swali hilo ?

Sio kwamba dini ime tawaliwa na mabaya pande zote sio kweli ni mtu pekee aliye weka kiburi moyo wake anaweza sema hivyo yapo baadhi yaliyo ni bora, lakini andiko langu lina zungumzia namna dini iliyo jitanabaisha kwa picha ya upendo na amani huku ikiwa imetawaliwa na vita fujo ndani yake tofauti na huo upendo na amani kutawala pande zote.
 
Biashara ya dawa za kulevya.
Kwa hiyo dini hizi hazina tofauti na biashara haramu za madawa ya kulevya ?

Ndugu una ungana na Karl Marx katika tafsiri hiyo ya dini hizi ?
images-2-2(0).jpeg
 
Kabla ya kuitipia lawama dini husika kuhusu vita na umwagaji damu inatakiwa kwanza tuangalie Sababu ya hizo vita......kwa upande wa uislamu vita vingi viliivyopiganwa zilikuwa na lengo la kulinda na kutetea amani ya waislamu na sio kusambaza dini kama mtoa madam ulivyoongea japokuwa vita hivyo ilikuja na hiyo impact (kuenea kwa dini) lakini haikuwa lengo la Vita.

Hata ukijaribu kufuatilia history ya hizo vita mfano crusade wars, Spanish christian- Muslim war , na vita vya badr,uhud na zingine nyingi utaona vita nyingi zilipiganwa waislamu ndio wanakuwa wamevamiwa na zote hazikuwa na lengo la kusambaza dini.

Dini imekuja kuwakumbusha watu kumuabudu mungu mmoja na kutenda mema ndio maana Quran imesema " walio amini na kutenda mema ndio wataingia peponi"
 
Back
Top Bottom