Yepi hayoUnaweza thibitisha haya madai yako mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yepi hayoUnaweza thibitisha haya madai yako mkuu?
Madhara ya watu kuacha dini ni makubwa Sana kwenye Jamii, tutapata kizazi kisichojua jua kutenganisha mabaya na mema. Kupata Jamii isiyo na maadili,Jamii isiyo na maadili utoa viongozi wabovu.
Wao sio sisi, mfumo wao wa malezi na maadili yao tu ni dini tosha.View attachment 2458368
Ume iona hii chart, je hayo uliyo andika kama madhara ya watu kuacha dini yapo kwa kiwango gani katika hayo mataifa ?
Vipi na sisi taifa lililo na watu wengi wenye dini hayo mambo uliyo orodhesha yapo kwa kiwango gani ?
Hao ni watu wa mataifa mbalimbali kila moja lina dini imedominate, uislamu, Ukristo,uyuda,shinto,bhudha, nk. Kupata mlinganisho ni hadi upate picha kuhusu hali yao kimaadili ipoje.Unaji kanganya kupitia maelezo yako ya awali na sasa.
Kuwa na siku njema.
Hakuna. Usihukumu usije ukahukumiwaJe Mungu wa hizo dini ndie anaye toa maagizo hayo yatekelezwe na wafuasi wake ?
Hayo kuwa Uislamu ulianzishwa na ukatoliki ili kuitawala Arabia.Yepi hayo
Mbona lipo wazi,mfano chek tu mafundisho yaliyomo kwenye Quran imekopi kutoka yaliyopo kwenye Biblia yaani vitabu vya Injili,taurat na zaburi.Hayo kuwa Uislamu ulianzishwa na ukatoliki ili kuitawala Arabia.
Andiko lime jikita katika dini na vita zake sio ukoloni na vita za ukombozi, kwa kua hizi vita ulizo orodehesha hapa zina tutoa nje ya andiko.Majimaji war 1905-07
Algeria war of independence 1954-62
Kagera war 1967-69
Ukraine war 2022-
Chinese civil war 1945-49
WWI 1914-18
WWII 1939-45
Hii ni baada ya wote Yesu na Muhammad (PBUH) kuishi na kufa lakini sababu za vita hapo juu haikuhusisha dini yoyote ile na orodha ni ndefu sana siwezi andika yote hapa.
Kufuata dini kikamilifu ni kufanya nini ? Na kivipi unasema hao hawakufuata dini kikamilifu wakati walihusika katika usambazaji na uteteaji wa dini mpaka kufika maeneo mbalimbali ?Hii inatokea pale wanaodai wanafuata dini fulani (hizo tatu ulizotaja) hawafuati kikamilifu.
Dini sio tu mfumo wa maisha, dini ina husisha swala la kuabudu kitu kiitwacho na wana dini Mungu au Muungu. Mfumo wa maisha haukamiliki kuitwa dini kama hausishi swala la kuabudu.Maana ya dini ni; Dini ni mfumo wa maisha ya wanaadamu, kwa maneno mengine ni muenendo mzima wa maisha ya mwanaadamu ndiyo dini.
Dini hizi ktk ile hali ya uhalisi wake kama alivyokuja nayo Mussa (AS), Yesu(AS) na Muhammad (PBUH) hazina shida kabisa na zilikua ktk misingi na lengo lake.
Anhaa kumbe halalishwa kwa vitu maalumu tu ? Kwa nini usihalalishwe upendo kwa vitu vyote na sio dini kuchukua uamuzi huo ?Dini ktk uhalisi wake hakuna kushika mapanga, haya mapanga ya akina Anti Baraka, Al Qaeda, Alshabaab, Lord Resistance Army na wenzao wako kinyume kabisa na mafundisho ya dini zote tatu.
Mathalani, Uislam unahalalisha vita endapo moja ya sababu ya kuingia vitani ni pale ambapo jamii itapokonywa ardhi yake, na hata katika vita hivyo kuna sheria za kufuatwa ikiemo kutokata miti bila sababu, kutoua watoto, wanawake, wazee wala walemavu na hata wakishinda vita basi ni dhambi kulazimisha maadui wao kusilimu wala kubomoa makanisa na masinagogi wala kuua wachungaji, marabi na watumishi wa dini.
Kuwa ita watu makafir sio chuki na ubaguzi?, Kuwa ita watu wapumbavu wasio amini wao sio ubaguzi na chuki ? Kuwaita watu wapotevu wale wasio kubalina na mafundisho ya dini zao sio chuki na ubaguzi ?Dini hizo zote zinahimiza upendo na ushirikiano baina ya watu wa imani tofauti.
Mathalan ukristo unahimiza watu kuwapenda majirani zao kama wanavyozipenda nafsi zao.
Uislam pia unahimiza kuwatendea wema majirani, na tafsiri ya ujirani ni nyumba arobaini toka nyumbani kwako hao wote wanahesabika kuwa ni majirani.
Uislam unaruhusu Muislam kumuoa Mkristo.
Uislam unaruhusu Muislam kula nyama ya mnyama aliyechinjwa na Myahudi ama Mkristo (sharti mchinjaji awe amemtaja mungu mmoja wakati wa kuchinja)
Kwahiyo Mafundisho ya dini hizi tatu hayafundishi chuki, ubaguzi wala uharibifu wowote bali kinyume chake.
Mungu wa upendo aliye amrisha Vita na chuki kwa wasio wafuasi wake si ndivyo ?Mafundisho ya dini hizi zote yanafundisha Mungu wa upendo.
Huo uharibifu ulio kuwepo kabla ya hizi dini ni upi ? Naomba uni orodhesheeHapana, kimsing jamii unayoiona hii leo ni matokeo ya wao kwenda makanisani na Misikitini, unadhani zimeharibika? Basi jaribu kuondoa hizi dini uone uharibifu ulio wa kweli.
Sababu za msingi ni zipi kuanzisha mauaji ya watu wakati hizo dini zime jiita dini za upendo na haki ?Zipo sababu za msingi ktk kuanziwha vita takatifu kwenye dini hizi.
Nitasemea uislam, kwenye Uislamu moja ya sababu ya jamii ya kiislam kuingia vitani ni kama kutatokea jamii nyingine itakayo lenga kuwapora ardhi yao.
Niamini mimi hata atikee mtu atake kukupora nyumba yako ni lazima huyo mtu utamuona ni shetani.
Vinakuwa vita vitakatifu kwa sababu; wakazi wa ile ardhi ni watu wa Mungu, wanaomuabudu na kufuata sheria zake kikamilifu… yeyote anayepanga kuharibu utaratibu huu mzuri wa Mungu huyo ni mharibifu na anapaswa kuonywa kuachana na chokochoko zake, ikiwa maonyo hayatafanya kazi basi ni lazima apigwe kikamilifu kwa msaada wake Mungu ili kuokoa sheria, utaratibu na watu wa Mungu.
Hata China Mao aliye kufa zaidi ya miaka 30 iliyo pita aliye ua watu kwa sera zake mbovu mpaka leo kuna watu wana muamini na wengine wana mchukulia mtakatifu kufa miaka mingi iliyo pita haifanyi makosa yasi sahihishwe.Wasambazaji halisi wa hizi dini Mussa (AS), Yesu (AS) na Muhammad (PBUH) walikuwa ni watu wema na mfano bora sana kwa watu wao na ndiyo maana walipata wafuasi wengi sana.
Pta picha Yesu(AS) amefariki miaka 2000 iliyopita lakini mpaka sasa kuna zaidi ya watu bilioni 2 wanamuamini na kufuata mafundisho yake
Pata picha Muhammad (PBUH) kafa zaidi ya miaka 1400 iliyopita lakni mpaka sasa kuna zaidi ya watu Bilioni 1.5 wanamuamini na kufuata mafundisho yake.
Ingekuwa watu walisambaziwa kwa hofu niamini wangekwisha achana na mafundisho yao.
Kwa maana aliyewatia hofu keshakufa yanini wabaki na mafundisho yao?
Wanapaswa kujifunza zaidi ili wawe huru kimaamuzi na kiimani na sio kuishi kama wafungwa au watumwa.Hapana, idadi kubwa ya waumini hawajui sehemu kubwa ya historia ya Dini zao.
Na hili ni tatizo kubwa.
Kwa wale ambao hawakuwa wafuasi wake toka kale mfano upaganiNi hatarishi kivipi? Sijaelewa
Kwa hiyo mwafrika ni shabiki tu katika uwanja wa hizi dini ?Mwafrika si mtumwa tena, Mwafrika ni mtu mwerevu mwenye maarifa ha mazingira yake.
Mwafrika ana uwezo na utambuzi wa kugundua kuwa Mungu yupo na ili tuishi ktk jamii yenye maadili na maendeleo ni lazima tufuate sheria zake.
Ziko dini nyingi ila ni jukumu la Mwafrika kutafiti na kujua ni ipi dini ya kweli ili aifuate.
Sijasema kuwa chanzo cha machafuko hapa duniani ni dini pekee la hasha usini nukuu vibaya .Kwahiyo sababu ya uharibifu hapa duniani si Dini, sababu ni mwanaadamu mwenyewe.
Maana uharibifu tuliuanza hata kabla ya dini hazijaja na tunauendeleza angali dini zipo na tena tunazitumia kama kichaka cha kufichia dhamira zetu ovu.
Dini ni kama kisu, Jikoni kinakata nyanya vitani kinatoa uhainwa mtu.
Je, tunathubutu kusema kisu ni kiovu?
Hapana, mtumiaji wa kisu ndiye ana hiyari akitumie kwa uovu au kwa wema.
Kwahiyo mfanano wa mafundisho ndiyo sababu ya kuwa Ukatoliki umeanzisha Uislamu?Mbona lipo wazi,mfano chek tu mafundisho yaliyomo kwenye Quran imekopi kutoka yaliyopo kwenye Biblia yaani vitabu vya Injili,taurat na zaburi.
Maelezo ya kina yapo ukisearch google utapata. Mfano. Did Roman Catholic creat islam?,
Uislamu ni ukatoliki. Nk utapata link mbalimbali. Hata JF upo uzi huo.
Kwa hiyo huyo Mungu ana amrisha wafuasi wake kwenda kuuwa watu wasio upande wake hivyo ndivyo anavyo hukumu sio ?Hakuna. Usihukumu usije ukahukumiwa
Ambaye anajua hana dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe huyu kijana. Wote tuna dhambi huwezi kumhukumu mwenzako ikiwa wewe una dhambi. Mungu ndiyo anahukumu.
Mungu hana dini.
Zipo ajenda nyingi nje ya mfananoKwahiyo mfanano wa mafundisho ndiyo sababu ya kuwa Ukatoliki umeanzisha Uislamu?
Nashauri kama jambo huna ushahidi nalo, hujalisoma, huna uhakika nalo usiliseme mkuu.
Maana yake.Kwa hiyo huyo Mungu ana amrisha wafuasi wake kwenda kuuwa watu wasio upande wake hivyo ndivyo anavyo hukumu sio ?
Mbona hautaji na vita na mauaji yaliyo kuwa yana tekelezwa kwa maamrisho ya huyo Mungu ?Maana yake.
Kipindi Yesu akihubiri, wakatokea watu wanataka kubeba mawe wamponde mwanamke kahaba. Yesu akawajibu
"Ambaye hana dhambi awe wa kwanza kumrushia huyu mwanamke jiwe" hakuna aliyethubu kwa maana hiyo Mungu ndiye anahukumu.
Mfano hai Sodoma na Gomora
Mungu hana dini wala Yesu hana diniMbona hautaji na vita na mauaji yaliyo kuwa yana tekelezwa kwa maamrisho ya huyo Mungu ?
Na kwa nini huyo Mungu ahukumu kwa mauaji ya kutisha wakati yeye na dini zake wameji tanabaisha kuwa ni wa upendo vifo vya kutisha ni upendo ?
Sikutoi nje ya mada najaribu kukuonesha kuwa si dini pekee iliyoleta vita, hata kabla ya dini zote vita na uharibifu vilikuwepo.Andiko lime jikita katika dini na vita zake sio ukoloni na vita za ukombozi, kwa kua hizi vita ulizo orodehesha hapa zina tutoa nje ya andiko.
Mkuu kuna dhana ndogo sana naona zinakuchanganya, na hiyo ni sababu tayari una majibu yako kichwani (prejudice) kama unataka tuelewane nashauri ufungue akili yako, usitake kila jibu liendane na kile ambacho tayari unacho kichwani.Kufuata dini kikamilifu ni kufanya nini ? Na kivipi unasema hao hawakufuata dini kikamilifu wakati walihusika katika usambazaji na uteteaji wa dini mpaka kufika maeneo mbalimbali ?
Sisi waislam tunafafanua maana ya dini kuwa ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu.Dini sio tu mfumo wa maisha, dini ina husisha swala la kuabudu kitu kiitwacho na wana dini Mungu au Muungu. Mfumo wa maisha haukamiliki kuitwa dini kama hausishi swala la kuabudu.
Hii maana ni yako mkuu, au una ‘scholary reference’?Ndio maana sio kila mfumo wa maisha ni dini.
Mkuu nauliza tena umesoma dini?Anhaa kumbe halalishwa kwa vitu maalumu tu ? Kwa nini usihalalishwe upendo kwa vitu vyote na sio dini kuchukua uamuzi huo ?
Mkuu umesoma Mafundisho ya Dini?Vile Vita vya kijihad vilivyo sambaza uislam west Africa vili kuwa nini kwako ?
Ni wapi kwenye Quran imeamrisha hilo?Kwa hiyo wayafanyayo hayo makundi kwa kutumia maamrisho ya Quran hawapo sahihi ?
Kwani nini maana ya kafiri? Usijekuwa unachukia ilhali ni kweli wewe ni kafiri.Kuwa ita watu makafir sio chuki na ubaguzi?,
Mfano bibilia inasema Zaburi 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema”.Kuwa ita watu wapumbavu wasio amini wao sio ubaguzi na chuki ?
Vilevile, kwani mpotevu maana yake nini?Kuwaita watu wapotevu wale wasio kubalina na mafundisho ya dini zao sio chuki na ubaguzi ?
Sasa rejea kwenye vifungu vya dini vinasemaje, kama vinahamasisha upendo hata kwa asiyeaminj basi suala la kuwaita wana wa shetani ni uzushi wa wafuasi wa dini na hilo halihusiani na Dini.Wana wapendaje watu wasio na dini wakati wame wapachika jina la wana wa shetani, waovu, wachawi kila jambo lisilo faa wana pachikwa.
Siyo asiye muislam, ni aliye Ahluh kitaab yaani aidha Mkristo au Myahudi.Wewe ndugu muislam ana ruhusiwa kula nyama iliyo jinjwa na mtu asiye muislam ?
Sio waislam wa wapi, hiyo ruhusa imetoka ktk Quran suuratil Maaidah:5Waislam wa wapi hao ?
Tazama dini inasemaje? Soma Quran soma Biblia soma TauratiImekwisha sahau vurugu zilizo tokea katika ya waislam na wakristo hapa nchini kuhusu hilo swala ?
Ni wapi kwenye Biblia au Quran inahamasishwa chuki?Una semaje mafundisho ya hizo dini haya ruhusu chuki wakatik kwa matendo na maneno chuki zina zihirishwa na hizo dini.
Ni wapi chuki imeamrishwa? Nukuu kifungu.Mungu wa upendo aliye amrisha Vita na chuki kwa wasio wafuasi wake si ndivyo ?
Uko ‘serious’ hujui?Huo uharibifu ulio kuwepo kabla ya hizi dini ni upi ? Naomba uni orodheshee
Mkuu Nakushauri hebu soma Human Nature kitabu kaandika Robert Greene,Sababu za msingi ni zipi kuanzisha mauaji ya watu wakati hizo dini zime jiita dini za upendo na haki ?
Mkuu unajua chochote kuhusu asili ya Binaadamu? Au walau Saikolojia zetu?kwa hiyo maamrisho ya mauaji yame haralishwa katika uislam je upendo na amani hapo upo wapi ?
Unajua chochote kuhusu Peace building au peace keeping mkuu?Kwani matumizi ya njia za amani haiwezekani ?
Mkuu nisamehe najibu maswali yako kwa kuuliza swali.Na kwa nini dini ihusike kupigania ardhi kwa vita ?
Mtu akuporae nyumba yako, akambaka na kumlawiti mama yako, mkeo, dada yako, bintiyo utamuona ni mkombozi? Au ?Nita muona shetani kwa misingi ipi ?
Vizuri, sisi tunaishi duniani, Mungu katupa akili, muongozo na uwezo wa kuyakabili mazingira yetu. Ni juu yetu kufuata muongozo kufanya hivyo na kufanikiwa.Kwani huyo Mungu wa hiyo dini hawezi kuirudisha hiyo ardhi kwenu kwa njia ya amani bila kuwa amrisha wafuasi wake kupigana vita vya umwagaji damu ?
Na wapo wengi hawakuua mtu mmoja lakini hii leo hakuna wanaomkumbuka, Yesu (as), Muhammad (PBUH) na Mussa (as) wamefanya mengi makubwa ambayo wewe binafsi na akili ulizonazo huwezi fanya hata kufikia theluthi.Hata China Mao aliye kufa zaidi ya miaka 30 iliyo pita aliye ua watu kwa sera zake mbovu mpaka leo kuna watu wana muamini na wengine wana mchukulia mtakatifu kufa miaka mingi iliyo pita haifanyi makosa yasi sahihishwe.
Hiko ni kigezo kizuri sana, leo hii hakuna mtumwa wala hakuna anaeshikiwa panga kwenda msikitini au kanisani au kumwamini Mungu lakini tazama ni wangapi wanamuamini.Kuwa na wafuasi wengi sio kigezo kuwa hicho kitu ni bora kila pande na hakina madoa.
Naam watu waliridhia wakaenda vitani kupigana kulinda ardhi zao, mama zao, binti zao na wake zao.Kwa hiyo hivyo vita vitakatifu vilikua upendo na sio hofu kuridhia mafundisho kwa shingo uapande, una ifahamu Age of reason in Europe kili tokea kitu gani ?
Naam ni sahihi kabisa, mkuu ulitaka iweje?Bado mafundisho yaliyo rithishwa vizazi na vizazi yana watia hofu wafuasi wake kuhusu adhabu watakazo pata siku wa mwisho endapo wakijitenga na hizo dini na huyo Mungu wa hizo dini.
Naam nakubaliana nawe, sifurahii watu walio waumini wa dini fulani kufuata imani hiyo kibubusa. Ninaamini kila mmoja anapaswa kuifuatilia imani yake kiundani kisha kufikia hatma yake mwenyewe.Wanapaswa kujifunza zaidi ili wawe huru kimaamuzi na kiimani na sio kuishi kama wafungwa au watumwa.
Nukuu kifungu cha chuki toka kwenye misahafu.Kwa wale ambao hawakuwa wafuasi wake toka kale mfano upagani
Hayo umesema wewe, hakuna mahali nimesema hivyo mkuu.Kwa hiyo mwafrika ni shabiki tu katika uwanja wa hizi dini ?
Vizuri, nami nikakuonesha jambo ambalo hukutaka kulionesha kuwa hayo machafuko ya dini ni kijisehemu kidogo tu cha sehemu kubwa ya vita na machafuko yaso na kichwa wala miguu.Sijasema kuwa chanzo cha machafuko hapa duniani ni dini pekee la hasha usini nukuu vibaya .
Ni kweli, ila elewa asili ya wanaadamu, Dini ni chombo tu kama utaifa kinachotumiwa na baadhi ya watu kufanya yale yasofaa.Nimezungumzia dini kama chombo kinachoitwa chombo cha amani na upendo huku kikiwa kimejaa Vita za kutosha zilizo gharimu mauaji makubwa ya watu , chuki , masengenyo, utumwa, ubaguzi n.k
Tena hivi ndivyo vimeichafua dunia kwa sehemu kubwa kuliko hata dini.Chanzo cha machafuko dunia pia ukabila una husika, ukanda, siasa, tamaduni, falsafa n.k