Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Je, dini ni upendo au ni chuki? Vita na mauaji yaliyokithiri

Habari za saa wanachama natumai ni njema.

Mjadala wa leo kupitia maswali umejikita katika kufahamu,je upi msingi wa hizi dini zilizopo hapa duniani kwa sasa hasa hasa hizi dini kubwa tatu maarufu ukristo, uislam na uyahudi ni nini?. kutokana na wanayo ya hubiri na wanayo ya tenda.

Ukiifuatilia historia ya hizi dini[ ukristo, uislam na uyahudi] uchipuaji wake hapa duniani ume gubikwa na matukio mengi sana ya kutisha, kuhuzunisha na hata kukasirisha.

Hata ukuaji na usambazwaji wake duniani ulikua katika namna ya tofauti sana jambo linalo tilia shaka juu ya yale yanayo pambwa nje na yaliyo ndani ya hizo dini.

Kwa asilimia kubwa dini hizi katika historia zake za uanzishwaji na ukuaji zimetawaliwa na mauaji, chuki, visa , utumwa, vita na vifo vya watu wengi sana na hata vitabu vya hizi dini vinavyo itwa vitabu vitakatifu kwa hao wafuasi wake navyo vime hararisha baadhi ya hayo mambo niliyo orodhesha kwa sifa na utukufu wa huyo wanaye muabudu.

Hizi hapa ni baadhi ya vita zilizo mwaga maelfu na maelfu ya damu zilizo piganwa na hizi dini kubwa maarufu nizi zungumziazo huku zikivishwa kiremba cha “vita takatifu”sifa na utukufu kwa huyo wanaye muabudu:-
i, First crussade, 1096
ii, Second crussade, 1145-1149
iii, Third crussade,1189
iv, Fourth crussade, 1202-1204
v, Fifth crussade, 1213
vi, Sixth crussade, 1228
vii, Jerusalem massacre, 1099
viii, Children's crussade, 1212
 ix, Spanish christian - Muslim war, 912- 928
x, Spanish christian- Muslim war, 977- 997
xi, Spanish christian- Muslim war, 1001- 1031
xii, Spanish christian- Muslim war, 1172- 1212
xiii, Spanish christian - Muslim war, 1230- 1248
Xiv, Christians- Donatists war, 317
xv, Christians- Estonians war, 1208- 1224
xvi, Battle of Badr, 624 AD
xvii, Battle in Uhud, 625
xviii, Battle in Mecca, 630
ix, Battle in Hunayn, 630
x, Battle in Khandaq, 627
xi, Jihad wars in west Africa, 19th century
Na vita zengine nyingi sana hizi dini zili husika katika umwagaji wa damu mkubwa.

Maisha ya hawa watu wenye hizi dini kubwa kwa asilimia kubwa yame tawaliwa na majungu, chuki, visasi na masengenyo kwa wale wasio wafuasi wao, ustaarabu kwa asilimia kubwa kwa jamii ya wana dini umekosekana haya unaweza ukaya shuhudia pia kupitia jaziba na michango yao humu majukwaani iliyo jaa chuki, hasira na lugha chafu.

Makundi ya kigaidi mengi yanayo sambaza hizi dini kwa njia ya upanga na mauaji ya kutisha kwa wale wasio fungamana nao, huu umekua utamaduni wa usambazaji wa hizi dini kwa njia iliyo ya mabavu ya kutisha toka kale.
Maswali:
1.Lengo hasa la uwepo wa hizi dini hapa duniani ni nini ? [ hasa hasa hizi dini kuu tatu ukristo,uislam na uyahudi ] na je mpaka sasa hizi dini zipo ndani ya lengo au zipo nje ya lengo ?

2. Kwa nini hizi dini zina imba wimbo wa amani huku zikiwa zimeshika mapanga?

3. Kwa nini hizi dini zina endekeza ubaguzi, chuki, masengenyo na uharibifu mkubwa kwa wale wasio wa amini ?

4. Je hizi dini zina abudu Mungu wa upendo au zina abudu Mungu wa Vita, chuki, visasi, ubaguzi na masengenyo ?

5. Je hizi dini zime shindwa kustaarabika ?

6. Kwa nini vita za umwagaji mkubwa wa damu zilitwa vita takatifu? Je zilikuwa ni maigizo ya huyo Mungu wao kuzi tekeleza kwa watu ?

7. Kwa nini usambazaji wa hizi dini uliji kita katika vita na utiaji wa hofu kuliko upendo na amani kama wasemavyo wao kupitia picha ya nje ya dini zao ?

8. Je waamini wake wana zifahamu historia ya hizi dini zao kwa kina ni wapi zimetoka, zipo na ziendako au wame baki kuwa waamini tu ?

9. Kwa nini hizi dini kuu tatu zili kua hatarishi kimatendo na bado mpaka sasa ni hatarishi kwa dini zengine zisizo shabihiana kiutendaji ?

10. Ipi nafasi ya mwafrika katika hizi dini ?

Mwenye swali la ziada una weza ongeza, karibuni wadau.
Umri wako?
 
Kabla ya kuitipia lawama dini husika kuhusu vita na umwagaji damu inatakiwa kwanza tuangalie Sababu ya hizo vita......kwa upande wa uislamu vita vingi viliivyopiganwa zilikuwa na lengo la kulinda na kutetea amani ya waislamu na sio kusambaza dini kama mtoa madam ulivyoongea japokuwa vita hivyo ilikuja na hiyo impact (kuenea kwa dini) lakini haikuwa lengo la Vita.
Maelezo yako haya yana onesha kuwa umeielewa thread kwa kina.

Asante kwa kuni thibitishia hilo.
 
Dini ni siasa,dini ni power of people,dini ni slavery,dini ni brainwashing device,dini ni prestige,dini ni unnatural,dini ni division,dini ni hate,dini chaos,dini ni treasury,dini ni fear of mind illusion,dini haiku transform ina kuchange,dini inakupa false identity.

The only truth is inside you if you stop that Ego,thought,greedyness,knowledge,future,desire,then your are free Awaken hence utaexperience the inner joy,true heaven,God and eternal/timeless freedom.
Jifunze kwa ndege ,miti na mito just enjoy life just live everything happens itself,ukihangaika unakimbia ukweli wewe ni ukweli then enjoy it.
 
Kama ulianza na hao walitumia nguzo gani.Ili uwe Muislamu ni lazima uwe na nguzo tano.
Nani aliyekuambia kuwa waislam wote waliotangulia ilikuwa lazima wafuate nguzo Tano?

Hata hao waislam wa kipindi Cha mtume Muhammad wapo waliokufa kabla amri ya nguzo Tano za kiislam haijakuja
 
Above 18 . Kwa nini ume uliza hivyo ndugu ?
Kutokana na aina ya hoja zako. Ni kama vile umetoka sekondari juzi juzi. Labda nikuulize swali dogo tu, hivi unadhani dunia ingekuwa bila dini, yaani full atheism ambao wewe unawaona ndio wenye ufahamu mzuri kungekuwa na maisha ya furaha, amani na upendo? Kwamba watu wangeishi kwa raha na kula Bata tu, huku kila mmoja akiwa na mali nyingi wala hakuna umaskini, vita, magonjwa, njaa nk kwa sababu haya yote yameletwa na dini?
 
Kutokana na aina ya hoja zako. Ni kama vile umetoka sekondari juzi juzi. Labda nikuulize swali dogo tu, hivi unadhani dunia ingekuwa bila dini, yaani full atheism ambao wewe unawaona ndio wenye ufahamu mzuri kungekuwa na maisha ya furaha, amani na upendo? Kwamba watu wangeishi kwa raha na kula Bata tu, huku kila mmoja akiwa na mali nyingi wala hakuna umaskini, vita, magonjwa, njaa nk kwa sababu haya yote yameletwa na dini?
Hujasoma andiko kwa makini, andiko halizungumzi atheist,atheism na wala sijasema kuwa dunia ikiwa na atheist ndio ina kuwa dunia iliyo bora kuishi.

Sija andika mada hii kuisifia atheism sipo hapa kutangaza mazuri ya atheism.

Pia sija andika mada kuonesha kuwa mabaya yote hapa duniani yame letwa na hizo dini maarufu tatu soma tena andiko upya kuanzia kichwa cha andiko mpaka hitimisho.

Jitahidi kusoma kwa makini upate kuelewa ili mchango wako uwe ndani ya mada na sio nje ya mada.
 
Nani aliyekuambia kuwa waislam wote waliotangulia ilikuwa lazima wafuate nguzo Tano?

Hata hao waislam wa kipindi Cha mtume Muhammad wapo waliokufa kabla amri ya nguzo Tano za kiislam haijakuja
Nje ya Quran Hakuna uislamu,SAsa hao walitumia muongozo upi kujifunzia,hali Quran kaja nao Mtume.
Walikwenda Hijji Macca ?.
 
Nje ya Quran Hakuna uislamu,SAsa hao walitumia muongozo upi kujifunzia,hali Quran kaja nao Mtume.
Walikwenda Hijji Macca ?.
Nani aliyekuambia kabla Quran hakukua na uislam?

Nabii Nuhu, Ibrahim na Musa walikuwa na dini gani ? Au walikuwa wapagani?

Vipi hizo Makala zako unazosoma na kukujaza ujinga zinasemaje au zinasema kuwa Nabii Nuhu, Ibrahim na Musa walikuwa wakatoliki?
 
Mtoa mada unachotakiwa kujua nikwamba hizi dini zote, zina operate chini ya hasira ya Mwenyezi MUNGU.

Napia MUNGU ni upendo wala hana dini, ukishalijua hili huwezi kusumbuliwa na hizi dini feki, ambazo waumini wake na viongozi wao wa dini wanaishi maisha ya kunafiki just they pretend to live in their religions principles while they are not.
 
Hujasoma andiko kwa makini, andiko halizungumzi atheist,atheism na wala sijasema kuwa dunia ikiwa na atheist ndio ina kuwa dunia iliyo bora kuishi.

Sija andika mada hii kuisifia atheism sipo hapa kutangaza mazuri ya atheism.

Pia sija andika mada kuonesha kuwa mabaya yote hapa duniani yame letwa na hizo dini maarufu tatu soma tena andiko upya kuanzia kichwa cha andiko mpaka hitimisho.

Jitahidi kusoma kwa makini upate kuelewa ili mchango wako uwe ndani ya mada na sio nje ya mada.
Unaposema imani zina mambo ya kuchukiza, huoni implication yake? Kwa hiyo unaandika mada halafu hata hujui mwelekeo wake? Umeandika si kwa lengo la kuuliza bali KUONYESHA jinsi gani dini ni za hovyo sana zinazoienga chuki kuliko upendo. Think big
 
Unaposema imani zina mambo ya kuchukiza, huoni implication yake? Kwa hiyo unaandika mada halafu hata hujui mwelekeo wake? Umeandika si kwa lengo la kuuliza bali KUONYESHA jinsi gani dini ni za hovyo sana zinazoienga chuki kuliko upendo. Think big
Ume hama tena kutoka kwenye atheist na atheism kuja kwenye maswala yako binafsi sifahamu tatizo nini hasa uelewa wa mada ume kuwa mdogo au nini shida? sifahamu.

Naomba uni jibie maswali yangu kama utapendezwa kufanya hivyo kama hauta pendezwa asante kwa ushiriki wako katika hii mada.
 
Nani aliyekuambia kabla Quran hakukua na uislam?

Nabii Nuhu, Ibrahim na Musa walikuwa na dini gani ? Au walikuwa wapagani?

Vipi hizo Makala zako unazosoma na kukujaza ujinga zinasemaje au zinasema kuwa Nabii Nuhu, Ibrahim na Musa walikuwa wakatoliki?
Kabla ya Muhamad mwaka 600 BC uislamu haukuwepo,acheni kudandia meli.
Hao walikuwa Wayahudi
 
Ume hama tena kutoka kwenye atheist na atheism kuja kwenye maswala yako binafsi sifahamu tatizo nini hasa uelewa wa mada ume kuwa mdogo au nini shida? sifahamu.

Naomba uni jibie maswali yangu kama utapendezwa kufanya hivyo kama hauta pendezwa asante kwa ushiriki wako katika hii mada.
Hakuna jipya, halafu imani haisomwi hivyo. Suala la atheism ni option uliyoiacha baada ya kushambulia dini. Hivyo litabaki hivyo
 
Hakuna jipya, halafu imani haisomwi hivyo. Suala la atheism ni option uliyoiacha baada ya kushambulia dini. Hivyo litabaki hivyo
Sawa asante kwa tafsiri yako juu yangu, kuwa na siku njema.
 
Wakatoliki ndio walioanzisha Uislamu Ili kuwaweka waarabu ndani ya utawala mmoja wa kiimani, kabla waarabu walikuwa wakiabudu miungu yao mbalimbali kupitia masanamu Ili iwe rahisi kuwatawala, Majasusi wa Shirika la Jesuit vatican wakaanzisha dini mpya itwayo islam,itakayowaunganisha waarabu wote kiimani mwaka 600 BC. Mapadre watano wa kikatoliki ndio walioandika kitabu cha Quran na kumtafuta mwanamke mfanyabiashara aitwae Bi Hadija na kumpa utajiri. Bi khadija ndie alimtafuta kijana aitwae Muhammad akamkabidhi kwa mapadre wa kikatoliki ndio waliomfunza Quran mapangoni.Ndipo Uislamu ukaenea kwa kasi Sana Katika nchi za kiarabu ambazo zamani zilikuwa ni nchi za Kikristo ukavuka mpaka na kutaka kuingia nchi za Ulaya mashariki kutokea Uturuki Ili kwenda kuiteka Vatican, Majasusi wa Jesuit wakaingia tena vitani wakarudisha nyuma kupitia vita vya msalaba waarabu wakala Sana panga toka vatican wakarudi nyuma, rejea vita vya msalaba na ottoman empire. Majuzi magaidi wa ISIS tokea iraq wakataka kuendeleza mpango ulioshindwa wa ottoman empire kuupenyesha utawala wa kiislamu Ulaya. Wakasambaratishwa na USA na NATO na kumuua Al baghad kiongozi wa ISIS. Huku kundi la ISIL tawi la ISIS Syria likipelekwa kuzimu na ndege za Putin.
Dini zote uzionazo duniani ni tawi la ukatoliki, maprostetant wote ni watoto wa katoliki.
Wakatoliki ni zao la freemasonry.
 
Dini ni chili na majivuno ni miongoni mwa mambo machafuzi na mabaya kuliko mengine ukiacha sasa. SI KITU KIZURI NA HUCHANGIA SANA BAADHI YA UOVI.
 
Sitaweza kutenganisha na kujibu maswali yako yote , Ila nacho shukuru umekiri kua kwenye uislam kuna maamrisho ya Vita za kimauaji kwa sababu maalamu na hili ndilo lengo la thread toka mwanzo kama umeisoma vizuri?
Ndiyo vita imeruhusiwa kwa sharti maalum.
Na kitu kingine nilicho gundua kwako una yaweka makosa ya dini ni kama tu yalivyo makosa mengine yafanywayo na jamii zengine kua ni mfumo wa watu ndivyo ulivyo, sasa hapo ni utofauti gani dini imeleta kama ina endeleza taratibu zile zile kama za jamii zile zilizo zikuta ?
Dah mkuu ndiyo maana nakusisitiza usome, ukifuatilia uzuri jamii ilikuaje wakati Mussa (AS) anakuja na Torati, Yesu (as) anashua na Injili na Muhammad (PBUH) anashuka na Quran swali hili ungepata jibu.

Kujibu swali lako nikuwa hao wote walikuja kubadili mabaya ya jamii zao.
Ningependa tuzungumzie makosa ya dini kama yalivyo makosa yake na siyo kuya fananisha na makosa ya yatendwayo jamii zingine ili kuharalisha makosa ya dini kuonekana ni swala ya kawaida watu kutenda hata kabla ya dini ? Kwa hiyo dini imeshindwa kuleta utofauti ?
Mkuu samahani hivi unajua hali ilivyokuwa kabla ya dini?

Maana unasema ni kama vile hakuna tifauti kipindi cha dini na kabla ya dini.

Kwenye Uislamu kuna zama tunaziita zama za ujahiliya, pitia uone waarabu walikuwa wakiishije halafu uone kama dini imeendeleza au kukomesha mabaya.
Ukilisoma andiko langu kwa makini mwanzoni kabisa limezungumzia dini, Mungu wa hizo dini na wana dini kwa hiyo hakuna sababu ya mimi kuwaweka kando wanadini katika huu mjadala labda kama ujasoma andiko langu .
Nimesoma na ndiyo maana najutahidi kukujibu kwa mwamvuli wa dini zote mkuu.
Unasema Mungu wa hizo dini hajaamrisha chuki na mauaji, umesoma namna alivyo kuwa anawapatia maamrisho wayahudi kwenda kufanya mauaji pasipo kuacha hata kiumbe hai ardhini je hayo unaya fahamu ? Vipi kuhusu mafundisho ya taurati ya Mussa ?
Nimesoma mkuu, Mungu haswa anavyoelezwa kwenye Uislamu ni mungu aliye ‘pragmatic’ upendo unaouhubiri wewe una mipaka kwake, kwa sababu wanaadamu tunaishi duniani ambako kuna kanuni za kuishi na Binaadamu huwezi leta upendo kwa kila mtu kama hutaki kuangamia.

Upendo una mipaka na unakuja na wajibu vilevile mauaji yana sababu maalum.

Nimekuuliza swali dogo sana Mtu akimbaka na kumlawiti mamayo, dadayo, mkeo na bintiyo utampenda na kumhubiria upendo?

Mtu akikuondoa ktk ardhi yako utamhurubia upendo?

Haya maswali ndiyo yanayijibiwa na dini kuwa uovu si wa kuuvumilia.

Ndiyo maana Mungu anatuambia adui akitutoa kwenye ardhi yetu tumpige pasina kumuonea huruma mpaka atakapoiacha ardhi yetu, ila mtu akitujia kwa wema nasi tuwe wema zaidi kwake.

Mwizi akiiba akatwe mkono wake, ila masikini akija kuomba msaada tumsaidie kwa tulicho nacho.

Upendo una mipaka yake.
Vipi kuhusu Jihad ni nini ?
Nimekujibu karibia mara tatu,
Unaposema nijifunze kuhusu dini ni ushauri bora kabisa ili nielewe nacho zungumza na ninge penda ufahamu dini huwa najifunza kadiri navyo pata nafasi ili nielewe nacho zungumza.
Vizuri sana, usijifunze dini pekee sasa jifunze na historia, siasa na saikolojia itakusaidia sana.

Unaposema fikra zangu nime funga utakuwa haupo sahihi, kwanza kama ningekuwa fikra zangu zime funga nisinge chukua hata uamuzi wa kujifunza yaliyo ndani ya dini Ni sawa na mwanadini umuambie ajifunze Yale yaliyo ndani ya uchawi au elimu ya uchawi sidhani hata ata endelea kusikiliza. Kuhusu najifunza na nafahamu nafasi yake katika jamii ni ipi ndio maana napo kuja na kuzungumza mambo ni kua nimejifunza.

Naona pia una shindwa kuiweka dini mbalimbali na mfumo wa kisiasa wa kidunia, ndio maana swali langu la mwanzo lili uliza lipi hasa ni lengo la dini ? Naomba urejee swali hilo ?
Dini huwezi itenganisha na siasa, ni makosa kufikiri hilo linawezekana.

Mathalan uislam ni dini iliyokuja pamoja na kanuni za kisiasa, Uislam umekwisha ongoza dola na himaya.

Huwezi tenganisha dini na siasa mkuu.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu, lengo lake ni kutoa muongozo wa namna ya kuyaendea maisha kwa wanaadamu.
Sio kwamba dini ime tawaliwa na mabaya pande zote sio kweli ni mtu pekee aliye weka kiburi moyo wake anaweza sema hivyo yapo baadhi yaliyo ni bora, lakini andiko langu lina zungumzia namna dini iliyo jitanabaisha kwa picha ya upendo na amani huku ikiwa imetawaliwa na vita fujo ndani yake tofauti na huo upendo na amani kutawala pande zote.
Vizuri Kwa kulijua hilo.

Soma vile vitabu nilivyovipendekeza kwako mkuu, vina msaada mkubwa sana.

Nikuulize swali mkuu;

Unapendekeza iweje tuachane na dini tuwe na mfumo gani?
 
Back
Top Bottom