Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Sijasema kwamba ubora wa maandishi yangu unatakiwa kuwa sahihi wakati wote, hili nalikubali. Hapa naongelea kitu tofauti.
Naongelea standards na applications zake. Naongelea "Noblesse Oblige". Naongelea "To whom much is given, much is required". Hizi ni basic principles. Huwezi kumpa mtoto wa darasa la pili mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper, utaonekana unachekesha.
Unayosema ni sahihi kabisa. Ila ni sahihi kwenye nyanja tofauti na hapa tulipo. Hapa JF hakuna haja ya kuwa too keen na maandishi tunayoyatoa. Sababu ni kuwa hapa tunafanya discussion tu.
Mkuu, ni vigumu kunishawishi kuwa hapa JF panafanana kwa namna yoyote na chumba cha mtihani. Ungeweza kufananisha majadiliano ya kawaida kati ya mwanafunzi wa darasa la pili na mtu wa chuo kikuu. Katika maongezi ya kawaida, hakuna tofauti kubwa kati ya alie chuo kikuu na alie katika shule za chini.Mimi kwa kazi ninayofanya na dhamana yake kwa maisha ya kila siku kwa wananchi wa Tanzania ni kama mtoto wa darasa la pili. Dr. Slaa kazi anayofanya na hususan anayoiomba ya urais, dhamana yake kwa maendeleo ya taifa ni kama mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper. Kutupa mimi mtoto wa darasa la pili na Dr. Slaa mtu anayeandika research paper ya chuo kikuu standards zile zile na mtihani ule ule itakuwa ni utovu wa maarifa.
Mimi si Dr, Slaa ni Dr. Mimi siko katika uongozi wa kisiasa wa Tanzania ngazi ya taifa, Slaa yumo, mimi sijaomba dhamana ya kupigiwa kura na wananchi hata ujumbe wa nyumba kumi, Slaa kashaomba na sasa anaomba kura za mamilioni ya Watanzania nchini kote.
Utawezaje kutuweka katika fungu moja?
Japokuwa hata ufananisho wako hapo juu si sahihi. Siamini kuwa huwezi kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais. Level hiyo naamini umeifikia. Tofauti yako nae ni maamuzi, uthubutu na nia ya kuomba kuchaguliwa tu. Inawezekana usiwe na exposure ya matatizo ya msingi ya Taifa kama alivyo yeye. Hiyo inaweza kuwatofautisha zaidi.
Vyovyote iwavyo, mapungufu hayo si ya msingi sana kwa taasisi ya Rais, maana ana watu wa kutosha kuhakikisha kuwa nyaraka zake zote ziko sahihi.