Habari za Jioni Wakuu,
Naomba nitumie kiswahili na kiingereza ili kueleweka zaidi.
Mimi naji'consider ni atheist nayeamini zaidi katika facts more than hearsay , ila kuna swali limekua likinitatiza na kunivunja moyo kuhusu science.
Tafuta utafutavyo, Google uwezavyo lakini hutapata jibu straight. Je Firauni(Pharaohs ) of ancient Egypt walikua watu wenye rangi nyeusi au watu weupe?
Mzungu atakuambia ulimwengu (The Universe) ulivyoanza miaka billion 13.7 iliyopita. Atakuambia hadi rangi waliokuwa nayo Dinosaurs miaka million 65 iliyopita. Watakuambia hadi kuhusu kinachoendelea kwenye galaxies billions of light years away from us.
Lakini hawawezi kujibu swali ambalo linamuulizia mtu aliyeishi miaka 3500 iliyopita.
Wakuu mwenye jibu la uhakika kuweka conspiracy theories aside na emotions aside. Je Firauni(Pharaoh) alikuwa mtu mweusi au mweupe?